Kwanini rais Kikwete haendi Mtwara?!

Kwanini rais Kikwete haendi Mtwara?!

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,395
Reaction score
13,273
Matukio ya mauji na uharibifu wa mali vimetokea Mtwara wakati rais akiwa katika safari zake za kuizunguka dunia. aliporudi akaishia kutoa hotuba ya redioni na Tv baada ya kudanganywa kuwa 'hali sasa Mtwara ni shwari' Sasa hivi mambo yameharibika tena. Wananchi wanapinga gesi kupelekwa Dar na mauji, utesaji na uharibifu mkubwa wa mali unaendelea. Hivi karibuni akiendelea na ziara zake za kuizunguka dunia nasikia eti alikatisha ziara yake ambayo kusema kweli ilikuwa imekwisha huko uarabuni baada ya bomu kutupwa kanisani huko Arusha ingawa sikusikia kuwa alikwenda.

Ninacho shindwa kuelewa mpaka sasa ni kwanini rais haendi Mtwara kujionea hali halisi badala ya kutegemea kusikiliza kutoka kwa wasaidizi wake ambao wanamdanganya? Hivi hiyo gesi ikibaki huko huko Mtwara nchi itapata hasara gani? Kama kuna mahali sikuwa na taarifa sahihi mtanirekebisha. Mimi nadhani ni muhimu kwa rais kwenda Mtwara akapambane na wananchi yeye mwenyewe asimtume Pinda wala mkewe maana naye sasa amekuwa kama waziri mkuu wa kupita wilayani na mikoani kupokea taarifa za serikali!
 
Muda huu c wakati muafaka JK kwenda Mtwara asubir upepo upite!
 
Back
Top Bottom