Kwanini Pacome hakumuachia Max Nzengeli ile penati?

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
1,914
6,033
Jana kuna tukio lilitokea na kujirudia kama lilivyotokea miaka 11 iliyopita.

Miaka 11 iliyopita Simba ilimgaraza Yanga magoli 5-0. Emanuel Okwi akiwa kashatupia goli mbili, Simba wakapata penati katika hali ya kushangaza penati ile akapewa Kaseja na akafunga. Ikamnyima Okwi hat-trick.

Jana Max Nzengeli akiwa tayari kashafunga bao mbili Yanga wakapata penati na kama ilivyotokea miaka 11 iliyopita, Nzengeli akanyimwa kuandika hat trick yake katika derby ya Kariakoo na badala yake akapewa Pacome.

Je, kuna namna hawataki rekodi ya Kibadeni ivunjwe? Abdallah Kibadeni anabakia mchezaji pekee kuwahi kufunga hat trick katika derby ya Kariakoo.
 
Nadhani ujanja ni kupiga goli 3 tatu bila kulilia penalt wala Faul.

Timu nyingi Duniani zinakuwa na specialist wa penalt na Faul.

Yanga walikiwa na Juma shaban na Dikson Job.

Pakome alikuwa mpigaji Penalt Asec nadhani ndio mwenye jukumu la kupiga penalt za yanga kwa sasa.
Lakini huu ujinga mlifanya msimu uliopita kwa Saido
 
Du! Rekodi ya Hat-trick ya Kibaden kumbe nayo ilikuwa ivunjwe jana!

Pacome naye angekuwa makini Rekodi ya Goli 7 ilikuwa inawekwa jana...
Pacome kakosa yeye na kipa
Zengeli naye baada ya kupata goli kapata clear chance akamlenga Manula akaicheza.
Kuna counter attack moja ilikuwa matata sana baada ya wachezaji wa Yanga kuwin mpira zikagongwa pasi chache za haraka haraka kisha mpira ukapigwa mpaka alipo Mzize, ikawa ni one against one ilikuwa Mzize atumie maarifa tu akamsalimie Manula ila akapokonywa mpira.
 
Ile ya Mzize angetumia akili kidogo tu lilikuwa goli lile, angeiminya pembeni kidogo Kisha aachie bonge la mshuti.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom