Kwanini ofisi hizi zipo kimya kipindi hiki cha utumbuaji majipu?

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Sijaelewa kwanini wakati huu wa utumbuaji majipu zile ofisi nyeti zinazohusika na kazi hiyo zipo kimya kuliko ilivyokuwa hapo awali?
ofisi ya CAG, PCCB, TISS na PAC (kamati ya bunge) zimepiga kimya cha hali ya juu, sijaelewa kwanini?

kuna faida kubwa sana tunapofanya kazi kwa kutumia taasisi kuliko kumtumia mtu mmojammoja, kwa maana collective decisions huleta transparency ktk utendaji wa viongozi wa taasisi, whistle blowers wanakuwa huru Zaidi maana wanawasiliana na taasisi badala ya individuals, lkn pia wale waliokosa huwajibishwa na mifumo na sio mtu mmoja mmoja.

kwa ilivyo sasa, viongozi wetu wa kitaifa wanalaumiwa sana, wanaambiwa wanatenda mambo kibabe etc (ref. mabandiko kadhaa ktk social media). haya yote hata kama hayana ukweli lakini mazingira ya watu wachache kufanya maamuzi yote wao kweli kama issues za kitaifa bado si picha inayopendeza sana kwa mustakabali wetu.

kesi ya reli (mpya), kesi ya UDART, kesi za makontena, kesi ya bandari bagamoyo, kesi ya kuficha sukari etc, hizi ni kesi kubwa sana ambazo kwa kweli zilipaswa kuwa mikononi mwa taasisi na muendelezo wake ukabidhiwe bunge la jamhuri ili kutoa mtazamo wa wananchi nao tusikie wana maoni gani?

Deal la 7bil USD, sidhani kama limeshawahi tamkwa popote ktk miaka 52 ya uhai wa nchi yetu, ni kitu kikubwa sana! mikataba kadhaa imefutwa mingine bila ya kubarikiwa na bunge,

Sasa je ikila kwetu nani ataidhinisha bajeti ya kulipia deni, kama wabunge kupitia PAC hawakushiriki ktk kuua hiyo mikataba? nani atakayetoa formal report kama PCCB na CAG si sehemu ya wazi ktk michakato husika?

Anyway, naomba kujuzwa kuhusu upembuzi yakinifu wa jinsi tulivyoweza kugundua haya madudu na jinsi hizo taasisi husika zilivyo-play role na ushiriki wa bunge.
najua nimekuwa muandishi mbaya, ila lengo ni kuuliza Zaidi ya kukosoa!
 
Serikali ya awamu ya tano inataka kufanya kazi baada ya kuingia madarakani na si siasa.

Taasisi zote ziko chini ya Rais na hakuna siasa huko.

Wewe tunga tu mada zako uonekane umeandika kitu JF ktk kumsema Rais Magufuli kwa maneno kama 'kutumia MTU mmoja mmoja' au 'individuals' ukifikiri hujulikani unasema nani.

Acha Rais afanye kazi kama anavyofanya na hizo Taasisi zinafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria zao kazi.

Nchi inachohitaji ni Maendeleo na Huduma kwa Wanainchi bila ufisadi full stop.
 
Kesi hizo zimefika mahakama ya mafisadi? Vipi escrow, lugumi,
 
Serikali ya awamu ya tano inataka kufanya kazi baada ya kuingia madarakani na si siasa.

Taasisi zote ziko chini ya Rais na hakuna siasa huko.

Wewe tunga tu mada zako uonekane umeandika kitu JF ktk kumsema Rais Magufuli kwa maneno kama 'kutumia MTU mmoja mmoja' au 'individuals' ukifikiri hujulikani unasema nani.

Acha Rais afanye kazi kama anavyofanya na hizo Taasisi zinafanya kazi kwa mujibu wa taratibu na sheria zao kazi.

Nchi inachohitaji ni Maendeleo na Huduma kwa Wanainchi bila ufisadi full stop.
Hivi unajua kuwa pesa za umma zinatumika katika kuendesha hizi taasisi?
kama tunaweza kufanya kazi bila ya uwepo wa zote, tunaweza ku-merge tu zikawa chini ya idara moja!
ant-fraud unit chini ya TISS ingeweza kupewa wigo mpana na ikaua ofisi ya PCCB, CAG hivyo tungepunguza kurugenzi.
lakini pamoja na yote, kiongozi anaheshimika sana akiweza kujenga taasisi kuliko kufanya kazi kama mtu mmoja!
mfano ktk maisha halisi:
Baba yako anaweza akawa anawapangia katika majumba mazuri sana (best apartments in town) lakini haja-invest ktk project yeyote, siku akiondoka duniani mnaanza upya kabisa, je ungewish kuwa na mzazi wa aina hiyo?
vipi kuhusu baba aliyeanzisha miradi kama mashamba, biashara na ujenzi, hata kama utoto wenu mlikuwa mnaishi - katika jengo lisilokamilika lkn baba akiondoka, si mtakuwa na pa kuanzia!

mimi ninachosisitiza hapo ni mifumo na sio individuals, lkn kama ungekuwa sio mpenda majungu, si raisi pekee anayefanya sole decisions, wapo wakuu wa mikoa, wilaya na maafisa wengi wa ngazi za juu wamefanya maamuzi mengi ambapo kwa jicho la kawaida unaona kama wao ndio engineers!

all in all, nilikuwa nauliza na kushauri!
swali liko palepale, je hizo taasisi zimebadili mtindo, au hazipewi nafasi ya kutosha?
kama hazipewi nafasi ya kutosha- ushauri wangu ni kuwa wanaotawala watazame upya, ni vema tukaziboresha na kuzirejeshea mamlaka hizo taasisi.
Mfano wa ujenzi mzuri wa taasisi - Rejea serikali ya Marekani
US hata iweje frauds utazisikia tu ziko chini ya CIA/FBI na watakaa tu senates kuamua hatma ya hiyo fraud kama itahitaji decision ya state. huu ni mfumo mzuri kwa kuwa kila uamuzi unapitia machineries zenye kutazama mambo kwa kina!

najua natwanga maji kwenye kinu: tayari akili zako umeshaweka ktk mpambano wa kisiasa, usichojua ni kuwa raia wana haki ya kushauri, bila ya kukashifu au kutumia lugha za kukera, raia tuna haki ndio maana nilipaswa kupiga kura hiyo maana yake inanipa haki ya kutaka kupewa mrejesho juu ya jinsi ninavyoongozwa lkn kushauri ninapohisi hapaendi sawa in my opinions, ktk demokrasia kama maoni yangu ni ya kibwege basi yaachwe tu!
 
Hizo sehemu ndio zimekithiri kwa rushwa kwa mtazamo wa pogba,ila wizara ya ujenzi haswa tanroad wanaishi malaika hakuna ufisadi wowote wala rushwa jamaa wanachapa kazi tu
 
Back
Top Bottom