Kuna sababu nyingi kwa rangi kubanduka toka kwenye ukuta. Kama rangi inatoka na kuacha plaster ikiwa intact, hilo linakua ni tatizo la uandaaji wa ukuta yaani ukuta unakua na vitu ambavyo ni loose (haukupigwa msasa vizuri) au rangi iliyotumika si nzuri kwa maeneo husika. Kama ni nje Weather guard emulsion paint na ndani Silk vinyl emulsion paint zinafaa zaidi kwa sababu zinaweza kupambana na mazingira tofauti, kuliko kutumia hizi normal emulsion paint.(ingawa bei za rangi hizo nilizozitaja ni expensive - three times ya hizi za kawaida!!!). Kama rangi inatoka na plaster, hilo ni tatizo la chumvi (salinity) ambalo hasa kwa maeneo kama ya Dar lipo zaidi. Kinga yake ni ngumu kidogo kwani unatakiwa ku-add some additives kwenye udongo wa plaster wakati wa kupiga lipu/plaster, ingawa haisaidii kwa muda mrefu sana, kwa msaada zaidi unaweza kuwaona NABAKI Africa, wanaweza kukupa maelezo zaidi hapo kwenye additives. Tatizo litakalokuwepo bado ni mchanga ambao bado utakua ni huohuo uliochimbwa sehemu zenye chumvi kama Dar, pia kutakua na suala la maji utakuta yana chumvi pia. Huwa inafika wakati inalazimu ku - check hata kiwango cha chumvi kwenye maji na hata kuosha mchanga au kupata mchanga toka sehemu ambazo hazina asili ya chumvi (hiyo ghalama utaona afadhali kujenga hivyo hivyo ili maisha yasonge mbele).