Kwanini nyumba nyingi Dar hubanduka rangi nje na ndani?

Ndani ya nyumba hizo watucwanakesha wababanduana..so kubanduka kwa rangi ni true reflection ya mambo ya ubanduzi ndani ya nyumba hizo hasa bedrooms
 
Kuna sababu nyingi kwa rangi kubanduka toka kwenye ukuta. Kama rangi inatoka na kuacha plaster ikiwa intact, hilo linakua ni tatizo la uandaaji wa ukuta yaani ukuta unakua na vitu ambavyo ni loose (haukupigwa msasa vizuri) au rangi iliyotumika si nzuri kwa maeneo husika. Kama ni nje Weather guard emulsion paint na ndani Silk vinyl emulsion paint zinafaa zaidi kwa sababu zinaweza kupambana na mazingira tofauti, kuliko kutumia hizi normal emulsion paint.(ingawa bei za rangi hizo nilizozitaja ni expensive - three times ya hizi za kawaida!!!). Kama rangi inatoka na plaster, hilo ni tatizo la chumvi (salinity) ambalo hasa kwa maeneo kama ya Dar lipo zaidi. Kinga yake ni ngumu kidogo kwani unatakiwa ku-add some additives kwenye udongo wa plaster wakati wa kupiga lipu/plaster, ingawa haisaidii kwa muda mrefu sana, kwa msaada zaidi unaweza kuwaona NABAKI Africa, wanaweza kukupa maelezo zaidi hapo kwenye additives. Tatizo litakalokuwepo bado ni mchanga ambao bado utakua ni huohuo uliochimbwa sehemu zenye chumvi kama Dar, pia kutakua na suala la maji utakuta yana chumvi pia. Huwa inafika wakati inalazimu ku - check hata kiwango cha chumvi kwenye maji na hata kuosha mchanga au kupata mchanga toka sehemu ambazo hazina asili ya chumvi (hiyo ghalama utaona afadhali kujenga hivyo hivyo ili maisha yasonge mbele).

mkuu hizo weather guard na silk vinyl emulsion ni za kampuni gani? Au kila kampuni ina aina hizo za rangi? Msaada please...
 
another problem ni proper waterproofing wakati wa ujenzi. watu huwa hawaweki damp proof membrane kabla ya kumwaga jamvi... jambo hilo husababisha maji kufyonzwa na kuta za msingi kutoka ardhini na husambaa mpaka kuta za juu hence causing rangi kubanduka.

mkuu damp proof membrane ni nini?

Je kwenye slub unaweza kuweka nini ili maji ya mvua yasinyonywe kwenye tofali na kuharibu gypsum board za ndani pia na vibarazani kwa juu?

Hivi kwenye misikiti huwa wanaweka nini kwa juu kuepuka maji kunyonywa kwenda chini ya slub?
 
mkuu hizo weather guard na silk vinyl emulsion ni za kampuni gani? Au kila kampuni ina aina hizo za rangi? Msaada please...

Haswa! kila kampuni zina hizo rangi. wewe chagua kampuni unayoipenda utapata hizo.
 
Kweli swala la chumvi dar es salaam limekuwa tatizo....na ndilo huoelekea kumomonyoka kwa udongo na rangi kwa ujumla.....kilimanjaro ukishushaa mjengo ndo mpango.
 
Haswa! kila kampuni zina hizo rangi. wewe chagua kampuni unayoipenda utapata hizo.

Katika kampuni za rangi tulizonazo hapa Tanzania, unaweza kuzi rate namba moja mpaka tatu kwa ubora wake. Hii itatusaidia tusifanye makosa tena mkuu.
 
Katika kampuni za rangi tulizonazo hapa Tanzania, unaweza kuzi rate namba moja mpaka tatu kwa ubora wake. Hii itatusaidia tusifanye makosa tena mkuu.
Kuzi-rate kampuni ambazo zinazalisha bidhaa aina moja na zilizo kwenye ushindani kibiashara ni kosa. Ukifika madukani unaweza kusaidiwa rangi za makampuni mbalimbali na hata wanaweza kwenda mbali zaidi wakakueleza kampuni ipi rangi zake ni bora zaidi.
 
Ok ni PM namba yako Mkuu ntakucheki mwezi wa January mambo yakiwa vizuri..nataka ugonge plaster ya ukweli kwenye kibanda changu mitaa ya Mbezi Msakuzi..
 
Wadau hebu tushauriane kuhusu masuala ya rangi za nyumba na sababu zipi zinafanya rangi ziwe zinabanduka tena ndani ya muda mfupi tu. Je ni mafundi wetu hawajui namna ya kuandaa kuta kabla ya kupaka rangi au ni ubora wa rangi zetu? Karibu kila nyumba ninazotembea hapa Dar zimeathiriwa na tatizo hili. Unaweza kukuta nyumba ni nzuri sana lakini ukiitizama kwa makini unaona baadhi ya maeneo rangi imeanza kubanduka. Maeneo sugu yanayoathiriwa sana na tatizo hili ni kama vile kuta za jikoni, bafuni, kwenye slubs n.k. Je wadau mafundi wetu wanakosea wapi? Ili kuepuka tatizo hili tufanyeje?

Utapeli mwingi uko kwenye rangi...tunauziwa rangi zenye ubora hafifu na ndo maana kuta hupauka na rangi humeguka baada ya muda mfupi sana.
 
mkuu kuna vitu ving vinachangia hio pamoja na jypsum praster inaposhika maji lazma ibanduke na memgine mengi mimi ni mtaalam wa finishing nitafute.

Ok mkuu ni PM namba yako nataka unigongee plaster ya ukweli kwenye Kibanda changu Pale Mbezi Msakuzi..
 
Kama hukuweka dump proof wakati unaanza kujenga kuna uwezekano wa kupata soln ya kuzuia kuta kufyonza unyevunyevu??
 
Kwangu naona hili tatizo limeanza. Naombeni permanent solution maana nimepia huu uzi na bado sijapata.
Nilienda Manyara nikakuta mtu kuzuia hili tatizo ameweka tiles ukutani kote.
 
Tukiwa tunaongelea rangi, hivi rangi zinazouzwa Tanzania zinadhibitiwa na kuhakikiwa kwamba hazina madini ya risasi (lead)?

Nchi nyingine zimepiga marufuku rangin zenye risasi kutokana na "lead poisoning".

Testing for and Removing Lead Paint
Udhibiti wa madini ya risasi katika bidhaa za rangi upo vizuri na hivi karibuni kuna viwango vingi vimeboteshwa katika eneo hilo na vile vile testing facilities zipo. Cha msingi ninkushirikiana na mamlaka za udhibiti.
 
Dodoma mjini hapo ndio majanga hakuna mfano unakuta nyumba msingi wote umelika mpaka unashangaa hiyo nyumba imesimama vipi!! chumvi ya dodoma ni balaaaa
 
mkuu damp proof membrane ni nini?

Je kwenye slub unaweza kuweka nini ili maji ya mvua yasinyonywe kwenye tofali na kuharibu gypsum board za ndani pia na vibarazani kwa juu?

Hivi kwenye misikiti huwa wanaweka nini kwa juu kuepuka maji kunyonywa kwenda chini ya slub?
Hapo hakikisha slab haijaziba mara kwa mara maana kama maji yakitoka -- hayataweza kufyonzwa
 
Back
Top Bottom