Kwanini nyumba nyingi Dar hubanduka rangi nje na ndani?

Brooklyn

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
1,459
284
Wadau hebu tushauriane kuhusu masuala ya rangi za nyumba na sababu zipi zinafanya rangi ziwe zinabanduka tena ndani ya muda mfupi tu. Je ni mafundi wetu hawajui namna ya kuandaa kuta kabla ya kupaka rangi au ni ubora wa rangi zetu? Karibu kila nyumba ninazotembea hapa Dar zimeathiriwa na tatizo hili. Unaweza kukuta nyumba ni nzuri sana lakini ukiitizama kwa makini unaona baadhi ya maeneo rangi imeanza kubanduka. Maeneo sugu yanayoathiriwa sana na tatizo hili ni kama vile kuta za jikoni, bafuni, kwenye slubs n.k. Je wadau mafundi wetu wanakosea wapi? Ili kuepuka tatizo hili tufanyeje?
 
Kutakua na tatizo la kiufundi sio bure....maana sidhani hali ya hewa inawezakua chanzo...mayb
 
Ni kweli aisee..na mimi nimeshuhudia sana hii hali kwenye nyumba yangu..ila kuna mtu ameniambia kuwa wakati mafundi wanafanya finishing walitumia Gypsum Powder badala ya White Cement ndo maana imebanduka...
ILA NAOMBA WADAU WANIPE CONTACT YA FUNDI MZURI AYEWEZA KUFANYA FINISHING HASA PLASTERING YA NYUMBA..
 
Kuna sababu nyingi kwa rangi kubanduka toka kwenye ukuta. Kama rangi inatoka na kuacha plaster ikiwa intact, hilo linakua ni tatizo la uandaaji wa ukuta yaani ukuta unakua na vitu ambavyo ni loose (haukupigwa msasa vizuri) au rangi iliyotumika si nzuri kwa maeneo husika. Kama ni nje Weather guard emulsion paint na ndani Silk vinyl emulsion paint zinafaa zaidi kwa sababu zinaweza kupambana na mazingira tofauti, kuliko kutumia hizi normal emulsion paint.(ingawa bei za rangi hizo nilizozitaja ni expensive - three times ya hizi za kawaida!!!). Kama rangi inatoka na plaster, hilo ni tatizo la chumvi (salinity) ambalo hasa kwa maeneo kama ya Dar lipo zaidi. Kinga yake ni ngumu kidogo kwani unatakiwa ku-add some additives kwenye udongo wa plaster wakati wa kupiga lipu/plaster, ingawa haisaidii kwa muda mrefu sana, kwa msaada zaidi unaweza kuwaona NABAKI Africa, wanaweza kukupa maelezo zaidi hapo kwenye additives. Tatizo litakalokuwepo bado ni mchanga ambao bado utakua ni huohuo uliochimbwa sehemu zenye chumvi kama Dar, pia kutakua na suala la maji utakuta yana chumvi pia. Huwa inafika wakati inalazimu ku - check hata kiwango cha chumvi kwenye maji na hata kuosha mchanga au kupata mchanga toka sehemu ambazo hazina asili ya chumvi (hiyo ghalama utaona afadhali kujenga hivyo hivyo ili maisha yasonge mbele).
 
Wadau hebu tushauriane kuhusu masuala ya rangi za nyumba na sababu zipi zinafanya rangi ziwe zinabanduka tena ndani ya muda mfupi tu. Je ni mafundi wetu hawajui namna ya kuandaa kuta kabla ya kupaka rangi au ni ubora wa rangi zetu? Karibu kila nyumba ninazotembea hapa Dar zimeathiriwa na tatizo hili. Unaweza kukuta nyumba ni nzuri sana lakini ukiitizama kwa makini unaona baadhi ya maeneo rangi imeanza kubanduka. Maeneo sugu yanayoathiriwa sana na tatizo hili ni kama vile kuta za jikoni, bafuni, kwenye slubs n.k. Je wadau mafundi wetu wanakosea wapi? Ili kuepuka tatizo hili tufanyeje?
zina banduka kwa sababu ZINABANDULIWA
 
Pia kwa hapa dsm maeneo mengi chini yana unyevunyevu sas unapopanda juu unatoa plasta na rangi...yan ukigusa ukuta ata kwa kidole mchanga unapukutika
 
Mimi hili tatizo kwangu halijatokea ila mtaaalamu wa rangi alinishauri nje nisiweke gypsup powder kwa sababu ukipata maji rangi yote inaharibika / banduka badala yake niweke white cement ila ndani niliweka gypsum powder na tatizo hilo sijaliona na huu ni mwaka wa 5 tangu nipake rangi

ila tatizo pia linaweza uwa ni wataalamu wa rangi

kitu ambacho nimeexperince ni rangi wa bati. Kupauka
 
another problem ni proper waterproofing wakati wa ujenzi. watu huwa hawaweki damp proof membrane kabla ya kumwaga jamvi... jambo hilo husababisha maji kufyonzwa na kuta za msingi kutoka ardhini na husambaa mpaka kuta za juu hence causing rangi kubanduka.
 
Ni kweli aisee..na mimi nimeshuhudia sana hii hali kwenye nyumba yangu..ila kuna mtu ameniambia kuwa wakati mafundi wanafanya finishing walitumia Gypsum Powder badala ya White Cement ndo maana imebanduka...
ILA NAOMBA WADAU WANIPE CONTACT YA FUNDI MZURI AYEWEZA KUFANYA FINISHING HASA PLASTERING YA NYUMBA..

mkuu kuna vitu ving vinachangia hio pamoja na jypsum praster inaposhika maji lazma ibanduke na memgine mengi mimi ni mtaalam wa finishing nitafute.
 
maeneo yote ya pwani yanakumbwa na hili tatizo,.

Sababu ni chumvi iliyopo ardini mkuu ndiyo inayopelekea hali hii!!

Mara nyingi wanashauri kabla ya kuanza kupandisha ukuta ni vizuri ukatenganisha msingi na kuta zinazopanda kuelekea juu kwa mifuko ya plastiki ili kupunguza makali ya chumvi iliyopo ardhini!!
 
ukitaka rangi isibanduke, do not skim coat before painting.

wakiisha maliza kuweka plasta we tandika rangi moja kwa moja, ukuta unakua sio soft kivile lakini rangi haibanduki, na kwa wengine hata muonekano wanaupenda zaidi
 
another problem ni proper waterproofing wakati wa ujenzi. watu huwa hawaweki damp proof membrane kabla ya kumwaga jamvi... jambo hilo husababisha maji kufyonzwa na kuta za msingi kutoka ardhini na husambaa mpaka kuta za juu hence causing rangi kubanduka.

sidhani kama watu wametilia mkazo post yako.....lakini tatizo linalokabili wengi ni DAMP.....mafundi wengi as u said hawafanyi proper waterproofing ambayo mojawapo ni kuweka damp proof membrane na matokeo yake rangi kuvimba,kubadilika rangi na hatimae kubanduka......
 
maeneo yote ya pwani yanakumbwa na hili tatizo,.

Sababu ni chumvi iliyopo ardini mkuu ndiyo inayopelekea hali hii!!

Mara nyingi wanashauri kabla ya kuanza kupandisha ukuta ni vizuri ukatenganisha msingi na kuta zinazopanda kuelekea juu kwa mifuko ya plastiki ili kupunguza makali ya chumvi iliyopo ardhini!!

Kaka kwa hii issue ya kutenganisha ukuta na msingi kwa kutumia Nylon kwa namna fulani kuna kaukweli hapo.
 
Mkuu umechemka aisee, huu uzi ni wa kuelimisha zaidi ya jokes. Sio vibaya kusoma na kupita tu if you are not interested.
Ungemwona anavyoona haya hivi sasa utamuhurumia,hajui hii post imewagusa watu kiasi gani,au kwa sababu yeye ana miliki nyumba /chumba kwa mwezi halafu anahamia kwingine? watu tumejaaliwa kujenga na hii issue tumei- overlook sasa inatutesa ,atupishe tupeane maarifa !
 
Tukiwa tunaongelea rangi, hivi rangi zinazouzwa Tanzania zinadhibitiwa na kuhakikiwa kwamba hazina madini ya risasi (lead)?

Nchi nyingine zimepiga marufuku rangin zenye risasi kutokana na "lead poisoning".

Testing for and Removing Lead Paint
 
Najifunza kitu hapa,je hili tatizo lipo hata kwa nyumba za tofari za kuchoma
 
Najifunza kitu hapa,je hili tatizo lipo hata kwa nyumba za tofari za kuchoma

Long live JF na ubarikiwe sana mleta uzi unafikiria sana kiongozi, uzi mtamu sana huu unapozidi kupitia comments za wadau unazidi kupata kitu fulani kichwani na kikakufaa sana. Mie sio mjuzi sana ktk angle hii so hapa nacomplement tu afu ntarudi tena baada ya mda kuja kuchukua ujuzi wanaoongezea wadau.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom