gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,283
- 3,274
Vipo viashiria lukuki ambavyo kimsingi vinahitaji kujipa muda ili tuweze kuupata ukweli wa mambo ulivyo ila siku upinzani ukistuka patakua kumesha kucha.Nalisema hili kama chanzo cha kuamsha hisia na mijadala huwenda ikawa chanzo cha kuupata ukweli.
Alivyo ni kama mdudu sondo anapekecha ndani kwa ndani,ukweli hujulikana pale mti unapo anguka ndipo unaweza kutambua ni nini chanzo cha tatizo.
Hivi kati ya sasa na kabla ya ujio wake upinzani,hali ya NCCR mageuzi ilikuaje?.Ukiachilia mbali NCCR kupoteza wabunge karibia wote lakini ukitizama mwenendo wa Mbatia utagundua ni kama mtu anayeburuzwa na kitu fulani nje ya yeye mwenyewe kwani kwa sasa NCCR imekua kama branchi ya Chadema.
Sasa tunaona CUF kunafukuto kubwa,lakini maswali ya msingi hapa ni kipi chanzo cha hili fukuto linalotokea sasa?Kama huu ujio usingekuepo je hiki kinachojitokeza CUF leo kingekuepo?Ni nini itakua hatma ya haya yanayoendelea?
Nadiriki kusema hata CDM inastahili pongezi kwa walau kuwa hai hata leo ila dira ilionesha kusambaratika mapema mara tu mwanasiasa huyu alipotinga upinzani.
Jaribu kutizama baadhi ya matukio yaliokua yakijitokeza na kauli za baadhi ya watu na hapa ningependa tujikumbushe maneno yaliopatwa kutamkwa na baadhi ya watu mashughuri nchini,
"Chadema kusambaratika kabla ya uchaguzi ujao".Haya ni maneno ya Steven Wasira ambayo kwa sasa yanaonekana kama vile Wasira aliropoka,lakini kwa matukio yaliojitokeza CDM na hata sasa je ni kweli wasira aliropoka ama ndani yake upo mkakati juu ya kile alichokisema?
"Chadema kuna kirusi,je unakijua kirusi hiki ni nani?.Na the motive behind".Hii ilikua ni thread iliokwisha wahi anzishwa humu na mwana jf mkongwe Pasco 6/4/2013.Lakini chanzo cha Pasco kuanzisha thread hii ilikua ni maneno ya ZZK ambapo alitahadharisha wakati ule akisema;
"kuna kirusi ndani ya Chadema ambacho kinakitafuna Chadema ndani kwa ndani kwa mtindo wa Kikulacho!".
Japo kirusi hiki kilicho wekwa wazi wakati huo kwa mtindo wa lugha ya picha na mwana JF pasco wakati huo kwa sasa kilisha ondoka ila ni nataka niwakumbushe CDM wakae wakijua imekua ni kama Mkombozi wetu ambaye wakati anaondoka hakutaka kutuacha hivi hivi ila alituachia roho wa kweli ili lililo pangwa lipate kutimia.
Niwakumbushe kurusi hiki kilichozungumzwa wakati ule kilitokea CCM na wakati wote kikiwa ndani ya CDM kilionekana ni shujaa wa kweli kikirusha madongo na makombora ya kila aina kwa serikali,lakini ilikua ni mkakati makini ambao kwa kipindi chote haukuweza kujulikana.
Lipo swali la msingi sana kila mmoja anapaswa kujiuliza,kabla ya hotuba ile ya mwisho pale hotelini ni wangapi walitambua kwamba nguli yule alikua na kazi mahususi tangu siku ya kwanza anavalishwa kombati na kuonekana amesha asi kule alipotoka?
Nichokumbuka baada ya pale tuliwasikia baadhi ya viongozi wakitaka aulizwe kama ile live press conference iligharimu zaidi ya 60m ni nani aligharimia?Lakini mnakumbuka majibu ya muhusika labda niwakumbushe,"Safari karibia zote zakichama za nje ya nchi nilikua nikizigharimia mwenyewe,mbona hamkuuliza wakati ule?".
Leo yupo mtu anaweza kumwaga pesa ma milioni kwa mamilioni lakiniakiulizwa anasema amezipata kwa marafiki zake,hao rafiki zake ni wepi?
Jambo lipi linakufanya uamini kwamba huu ugeni wa sasa ni salama wakati mtindo wa mwanzo ni huu huu ambao unaendelea sasa?
Ni jambo la muda tu lakini ninacho weza kusema,siku litakapokumbukwa shuka kutakua tayarikumesha kucha.