Kwanini nimekuwa mwanachama wa CCK?

Kalunguine

JF-Expert Member
Jul 27, 2010
2,543
134
Ukisoma tamko la mwenyekiti wa chama cha kijamii Constantine Akitanda kipengele cha tano,amezungumzia suala la kufutwa kwa ruzuku zinazopewa vyama vya siasa, na ukijaribu kutazama vyama vyenyewe havizidi vitatu au sita kama kweli, lakini a millions of our kod zinakwenda kwenye vyama hivi ambavyo havina wanachama zaidi ya milioni kumi wakati nchi ina zaidi ya watu milion 45, ina maana kuna zaidi ya watu milion 30 ambao mgao huu wa ruzuku hauwagusi moja kwa moja.

Mgomo wa madaktari leo usingekuwapo kama CUF,CCM,CHADEMA na wenzenu mngesema ruzuku nooooo1 HAINA MAANA AKINA Zitto kukataa posho ya shilingi 3300000/= pale bungeni wakati chama chake kinaendeshwa kwa ruzuku ya mamilioni ya kila mwezi ambazo pia pesa hizo hutumika kumuhudumia Zitto kama naibu katibu mkuu wa chama, sikwambii akina January Makamba na Hamis wa Nzega, kwa ajili hii basi migomo ya madaktari,madai ya waalimu kuboreshewa maslahi yao.

Na hata wafanyakazi wa sekta mbalimbali za umma wasingekuwa wanalalamikia serikali kama sote kwa pamoja tungesema NOOOOOO KATIKA RUZUKU! angalia mgawanyo huu tena ni kwa mwezi tu na ujaribu kuzisambaza pesa hizi kwa watumisha na then angalia kama kungekuwa na migomo ya ajabu ajabu!

CCM.........................Tshs 800million kwa mwezi..................

Chadema.......................Tshs 200 Million kwa mwezi........................

Cuf...................................Tshs 110 kwa mwezi..................


Kama wewe ni mpenda demokrasia wa kweli,karibu Katika chama hiki kwa pamoja tupambane na ufisadi huu wa ruzuku ambayo haitusaidii kukuza demokrasia bali migogoro ya kimaslahi ndani ya vyama na ushindani usio sawa hasa kipindi cha chaguzi kwani chama kama CCM kinapata ruzuku kubwa ambayo pia hutumika kununua shahada za wapiga kura.
naomba kuwasilisha
 
Mkuu una sura nyingi kweli. Maana post karibu zote za ccj/cck unaanzisha wewe ila ukiwa katika maumbo tofauti tofauti.
 
Investing in democracy is like laying a foundation for good governance; which as a result improves peoples' lives.
 
Kumbe kilichokufanya ujiunge cck ni ruzuku 2" kweli wanasiasa uchwara mmevamia humu jf.
 
Umezungumzia tamko la Costatine Akitanda uko sawa lakini Akitanda huyo huyo alitamka vile vile kuwa wao hawana uadui na vyama vingine vya upinzani ila chama tawala
sasa mimi nadhani ukamwulize je haoni kwamba haya matamko yake asiyoyapima yanaweza leta uadui manake kama akianza na hilo la ruzuku basi tayari ashakuwa na uadui na wenzie Vyama visipewe ruzuku vijiendeshe vipi???? Aache unafiki na ajue watu wanafikiri beyond borders hilo ni moja!

La pili mimi jibu langu kwako umejiunga na hicho Chama kwa kuwa ni haki yako uliyo nayo Kikatiba period hayo maelezo mengine yawe ya nyongeza.
 
Umezungumzia tamko la Costatine Akitanda uko sawa lakini
Akitanda huyo huyo alitamka vile vile kuwa wao hawana uadui na vyama
vingine vya upinzani ila chama tawala
sasa mimi nadhani ukamwulize je haoni kwamba haya matamko yake
asiyoyapima yanaweza leta uadui manake kama akianza na hilo la ruzuku
basi tayari ashakuwa na uadui na wenzie Vyama visipewe ruzuku
vijiendeshe vipi???? Aache unafiki na ajue watu wanafikiri beyond
borders hilo ni moja!
La pili mimi jibu langu kwako umejiunga na hicho Chama kwa kuwa ni haki
yako uliyo nayo Kikatiba period hayo maelezo mengine yawe ya
nyongeza.
sidhan kama unasoma na kuzngatia ya wenzako,acha kukurupuka
 
sidhan kama unasoma na kuzngatia ya wenzako,acha kukurupuka

This is very unbecoming, friend you wanna be a Judge of your own cause yani wewe utoe post halafu wewe uanze kucriticise mmmh hii kali sasa! Anyway you deserve to be where you are manake umeshadhihirisha wewe ni mtu wa namna gani. Ndo mana ukakimbilia huko bila kukaa na kusoma hilo tamko between lines.......... Mimi nimekurupuka ni kweli ila wewe utakuwa umekurupuliwa!!!!
 
cck-chama cha kanisa

This is not fair at all. Umeishawapatia propaganda radio Imaan, hasa kama chama hiki kinakuja pata umaarufu kama wa CDM in the futute. Japo wengine wa upande wa pili nao wanaweza sema maana yake ni 'chama cha kiislam'
 
Back
Top Bottom