Kwanini ni vigumu watu kupata wenzi wa maisha?

Jpinduzi

Senior Member
Feb 26, 2011
136
68
Wadau habar zenu!natumaini wazima!katika pitapita yangu leo nimevutiwa na ujumbe ufuatavyo!kama ulishawahi kupostiwa hapa JF niwieni radhi!
Hakika Mugu ni mkubwa anaweza kila kitu chini ya jua, pilika pilika zote za walimwengu, zinafanyika kwa sababu ya kudura zake, bila yeye hata moja lisingewezekana.

Hivyo basi tumshukuru kwa hisani anazozielekeza kwetu na tujiapize kutokukufuru hat mara moja, kwani kwa kufanya hivyo kutatufanya tuendelee kuwa wasafi mbele yake.
KUTOKUWA WAAMINIFU
Hii ni changamoto nyingine ambayo huwasababishia watu wengi kukosa wenzi wao wa maisha kila mtu anapenda kuwa na mpenzi anayeaminika ambaye hatompa jakamoyo la kila mara.
Staili ya maisha ya baadhi ya watu, yamewafanya kushindwa kuaminika, wanaishia kudharauliwa na kuonekana kama daraja Fulani ambalo linaweza kulinganishwa na wahuni,

Hivyo basi, kama unataka ikuchukue wepesi kupata mwenzi wa maisha huna budi kujiangalia mwenendo wako ujiatathimini hatua kw ahatua kwa umakini wa hali ya juu mno. Je umepata jawabu gani? Watu wanakuonaje? Hawakuamini?

Jibu ndiyo? Basi jirekebishe mara moja jiheshimu na uishi katika misingi inayokubaika ili jamii ikuamini kama wewe ni kiruka njia maisha yako hayaeleweki, utaendelea kutazamwa kama katuni isiyo na tafsiri.

Hujulikani unafanya kazi wapi wewe ni mjanja mjanja tu, kila siku unaonekana na mpenzi mpya, watu wanakuhisi ni jambazi, muonekano wako ni wa kihuni, hali hiyo inakujengea mazingira magumu ya kpata mwenzi.

UONGO
Wengi wamekuwa wakitumia gia tofauti kupata wapenzi hii huwatokea zaidi wanaume ingawa kuna baadhi ya akina dada nao huwa hawajambo kwa kusema uongo ili kujisafisha mbele ya viburudisho vyao.

Lakini ukweli umethibitisha kuwa njia ya muongo ni fupi au ndege mjanja huanaswa na tundu bovu pia wahenga walisema mbio za sakafuni huishia ukingoni.

Hivyo basi, utadanganya wawili watatu wa mwanzo, kwa ajili ya kukidhi matakwa yako, baadaye itakuwa wazi kila mtu atajua ‘janja’ unayotumia, akishakubaini mmoja, elewa jamii yote itakujua, kwakuwa habari husambaa.
Watu wakishaambiana, jua na thamani yako itashuka tu, kuporomoka kwa thamani ni wazi huheshimiwi na hiyo ni ishara kwamba unadharauliwa, kwa mantiki hiyo itakuwaia vigumu kupata mwenzi,

MAPENZI YA MBALI
Fimbo ya mbalihaiui nyoka ndivyo wahenga walivyosema, lakini ngano hiyo ina ukweli wa asilimia nyingi mno, hujawahi kusikia watu wakinena ya kwamba ni wako akiwa kwako akitoka nje si wako?

Jibu, ndiyo basi huo ndiyo ukweli wa mapenzi ya watu wengi wa kisasa, ukiwa karibu na mwenzi wako ni rahisi kudumu naye kuliko kuwa naye mbali, si unajua tena “abiria chungu mzigo wako?”
Hata hivyo, ni ukweli kuwa wengi hujikuta wakiwa mbali na wapenzi wao kwa sababu za kikazi, kimasomo na nyinginezo hali hiyo huharibu mapenzi ya waatu wengi mno.
Kuishi mbali na mwenzi wako huondoa uaminifu kwa sababu huzua chembechembe za usaliti, kwahiyo kama unatkia kuwa na mwenzi wa kudumu unashauriwa kuwa naye karibu.3 UFAHAMU MDOGO; uelewa mdogo ni pointi nyingine ambayo huwakosesha watu wachumba na baadaye wenzi wa kuishi nao, kipengele hiki cha ufahamu kinajumusiha pia utambuzi wa hisia ili kujua namna ya kuishi nao hawajui jinsi ya kuwatunza na kuwapa faraja muda wote,
Amini kwamba endapo utamtunza vema mwandani wako hatofikiria kukuacha abadan! Lakini kama itakuwa ni kinyume chake hatokaa na usipojirekebisha utageuzwa kama daladala ambalo kila mtu aaweza kupanda na kushuka.

4USHIRUKIANO MDOGO
Ongea na watu upate viatu, kwahiyo usiposhirikiana vizuri na ndugu, jamaa au jamii inayokuzunguka, usitegemaa kupata mwenzi.
Kuwa mwepesi kushiriki katika shughuli za kijamii kama misiba, harusi, sehemuza ibada na nyingine ambazo zitakukutanisha na watu mbalimbali

5UMALAYA
Mtu mwenye sifa hii huwa haheshimiwi, kwa sababu kila mtu humuogopa kwa imani kwamba hajatulia, kwahiyo kitendo cha kukubaliana naye kufunga ndoa ni sawa na kujiua.
Je, unatabia hiyo? Kama ndiyo basi wewe si mtuwa kuoa/ kuolewa, wewe utatumiwa tu kama chombo cha mapenzi lakini ikifika zamu ya ndoa, mwenzio ataangalia kule kunakofaa.

UKOROFI
Amini usiamini hakuna mtu anayeweza kukukubali wewe uwe mwenzi wake wa maisha kama ni mkorofi ni kila mtu anakusema vibaya
Mwanamke gain anayeweza kukubali kupokea kesi za kugombana na wenzio siku baada ya siku, nani, atakayevumilia maisha ya ununda kwa kupokea vipigo kila kukicha?
Jibu hakuna kwa sababu nyota njema huinekana asubuhi, kama umeanza kuonesha dalili lazima utamhenyesha, hivyo hatakubalikujitosa katika ndoa na wewe, kwa kuogopa yasimkute makubwa.

Unadhani ni mwanaume gain anayeweza kukubali kuwa na mwanamke ambaye yuko mbele kusutana na wenzake kila siku? Ugomvi na majirani, ndugu na jamaa?
Jibu hakuna kwa hiyo kila mtu yupo macho sana katika kuangalia sehemu ya kuangukia, wakorofi wengi huwa hawapati wenzi wao wa maisha kwa sababu ubaguliwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom