Kwanini nenda polepole kwenye barabara ya kasi?

Kwanini nenda polepole kwenye barabara ya kasi?

Salu1

New Member
Joined
Dec 29, 2017
Posts
2
Reaction score
0
Matarajio ya popote pale ni kwamba kadri barabara zinavyoboreka ndivyo muda wa kutoka mahala kwenda mahala kwingine unapungua. Tanzania kadri barabara zinavyoboreka ndiyo muda wa kutoka sehemu moja mpaka nyingine ndio unaongezeka!

Nchi zingine ukiweka taa za barabarani zinaboresha upishanaj wa magari kwenye makutano ya mabarabara. Tanzania ukiweka taa za barabarani ajili na polisi wengi zaidi wa kuzidhibiti taa zisiudhi magari.

Hivi haya ndiyo Maendeleo?

Highways zetu, TANROADS, watakubaliana nami, design speed katika sehemu nyini ni 80km kwa saa, Tanzania speed limit ni 50km kwa saa kwenye highway.

Nchi nyingine unaweza kusafiri usiku na mchana Tanzania tumehalalisha ujambazi na kupiga marufuku kusafiri usiku baada ya saa 4 huku Polisi tulio nao mahiri sana, wakazi wa Kibiti wanalo faili la sifa hizi.

Basically lilikuwa linasafiri Dar Mwanza kwa masaa 16 sasa linachukua masaa 28. Ndiyo kusema ili asfirishe idadi hiyo hiyo ya abiriapale alipokuwa na basi moja sasa awe nayo mawili. Hivyo hivyo kwenye malori nk.

Ni kweli kwa speed hizo Maendeleo tunayoyatafuta tutayapata.

Kwa sera za namna hii ipo siku itabidi tutembee kwa mguu kwa usalama wetu.

Hii imeanza pale Busisi Ferry. Itakumbukwa kwamba kuna minibus ilitumbukia majini. Matokeo yake sasa kuna Sheria uliowekwa kilienda usalama wa abiria. Inabidi vyombo vya usafiri viteremshe abiria takribani nusu kilometa kutokana kwenye kivuko watembee kwa mguu wanyeshewe l ati kwa sababu kunamtermko mkali mno. Unajiuliza hivi kwenye milima ya Kitonga na Sekenke mbona abiria hatuteremshwi?

Watanzania lazima tu dhibiti mwenendo barabarani lakini lazima tumuige konokono au kinyonga hivi hatuwezi kujifunza kwa SWALA?
 
Watunga Sheria Mara nyingi haziwagusi mkuu.

Eti trafiki anakupiga mkono ume over speed (>50Km/h) Sasa muulize kwanini anakukamata? Atajibu anajali usalama wako eti anajifanya anakujali[emoji23]

Hivi ingekua anajali zile gari za msafara wa rais zingetembea mwendo ule? Au rais hapendwi?
Jibu ni kwamba Sheria zipo kutubana wanyonge.
 
Siku ukipoteza either baba, mama, kaka au Dada yako kwa mwendokasi ndio utajua serikali inamaanisha nini kuweka hizo speed limit bylaws.


Then kuweni na akili sio kila Kitu " Mbona ulaya wanafanya hivi" huo ni upuuzi bila kuangalia mazingira halisi ya nchi
 
Siku ukipoteza either baba, mama, kaka au Dada yako kwa mwendokasi ndio utajua serikali inamaanisha nini kuweka hizo speed limit bylaws.


Then kuweni na akili sio kila Kitu " Mbona ulaya wanafanya hivi" huo ni upuuzi bila kuangalia mazingira halisi ya nchi
Mbona safari za viongozi wana drive zaidi ya 50km/hr na hawapotezi maisha...
 
Siku ukipoteza either baba, mama, kaka au Dada yako kwa mwendokasi ndio utajua serikali inamaanisha nini kuweka hizo speed limit bylaws.


Then kuweni na akili sio kila Kitu " Mbona ulaya wanafanya hivi" huo ni upuuzi bila kuangalia mazingira halisi ya nchi

Sijui kama ni upuuzi kujilinganisha na mtu anayefanya vizuri kuliko wewe ili na wewe ufanye vyema zaidi hata kama si kumfikia huyo unayejilinganisha naye. Kuridhika na ulicho nacho kumbe hakina tija labda ni kuyakataa maendeleo.

Sasa hivi hatuna mabarabara ambamo magari yanaweza kwenda kwa speed ya 180 km/hr. Lakini tunayo yanayoweza kupitisha magari kwa sehemu nyingi kwa speed ya 80km/hr, sehemu korofi tu ndizo zikabaki na speed limit ya 50km/hr, 30km/hr n.k

Tukifanya hivi tunaweza kuwa na wastani wa speed ya 70km ambayo ingeliwezesha gari kutumia saa 16 toka Dar hadi Mwanza. Lingeliondoka Dar saa 12 asubuhi na kufika saa 4 usiku. Kesho yake asubuhi basi hilo hilo lingelitumika kubeba abiria toka Mwanza hadi Dar hivyo nchi kutumia rasilimali zake vyema zaidi.

Lakini hata kwenye traffic lights, hizi zina settings kutegemea na WINGI wa magari katika kila njia, settings hizi zikifanyika vizuri au zikawa computerised hakuna haja ya kuwa na polisi tena kwenye traffic lights.

Kuhusu kusafirisha usiku naamini polisi wakidhamiria kudhibiti ujangili barabarani wanaweza na magari yakawa yanasafiri usiku na mchana rasilimali zetu zikatumika vizuri zaidi.

Yote haya yanaweza hufanyika na huku njia zingine zikaendelea kutumika kuboresha usalama.

Na si ulaya tu walikoweza, mbona nchi zingine za kiafrika zimeweza. Kuna ubaya gani tukijifunza kw mfano kutoka Ghana?
 
Back
Top Bottom