Kwanini ndoa nyingi zinavunjika nyakati hizi?

laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
541
Points
1,000

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
541 1,000
Sehemu ya kwanza

N-njoo
D-Duniani
O-Ongeza
A-Amani

Kwenye amani kuna upendo, kwa hiyo mnapoingia kwenye ndoa mnaongeza Amani na mnaongeza Roho zitakazopingana na shetani pindi mtakapopata uzao. Shetani na wafuasi wake hawapendi ndoa hata kidogo.

1. Wakorintho 13

1. Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo na upatu uvumao.

2. Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama sina upendo, si kitu mimi.

3. Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4. Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;

5. haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;

6. haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;

7. huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.

8. Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.

Ndoa ni nini? Ni muungano Kati ya mwanamke na mwanamume kuishi pamoja kama mime na mke muda wote wa maisha yao,iwe Kidini, kisheria au kimila.

Kidini ni mpango na utaratibu wa Mungu kwa wanandoa. "Bwana Mungu akasema si vema mtu huyu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye (Mwanzo 2:18)

Hapa tunaona kuna suala la kimamlaka katika ndoa, kwamba mke ni msaidizi.
Ambapo dunia ya sasa ni tofauti kidogo, baadhi ya watu wanatamani wakute maisha yameshaandaliwa anapoingia kwenye ndoa akute nyumba, magari, biashara au mwenza ana kazi nzuri.

Hii inapelekea vijana wengi wanaogopa kuoa wakisubiri kujipanga. Yap anaweza akajipanga akawa na biashara, gari na nyumba ya kupanga au yake sasa akili inawaza kuoa na mara nyingi misukumo inatoka kwa wazazi, ndugu au marafiki wanaokuzunguka unaamua kuoa binti uliekua nae kitambo au mliokutana kipindi maisha yamechangamka juzijuzi tu hapa, kama tunavyojua biashara kuna kupanda na kushuka, ile mmetoka ukumbini kama hamkujipanga vyema kuna madeni acha madeni kuna biashara yenyewe kuyumba.

Bahati mbaya biashara ikaanguka, ukaamua kuuza gari unyanyue biashara aa wapi mambo yanagoma(hapa shetani yuko pembeni anacheka tu hihihihi (anakungojea kwa hamu)

Mara nyingi mwanaume anaanza kupata msongo wa mawazo kuhusu mke atamwonaje, majirani, ndugu na marafiki watamwonaje kosa linaanzia hapa, ukiwa na mawazo (uta-lose confidence) utapoteza kujiamini kua wewe ni baba na ndo kichwa cha familia unatakiwa ukae chini na mkeo muangalie mlokosea wapi kama ilikua ni bata sana mnapunguza.

Mawazo yanakupelekea kukosa hamu ya tendo la ndoa (loss of libido) kwa mkeo, dawa ya mawazo cha kwanza ni kujikubali kua ilishatokea ndo hali yako na kukaa pembeni ya mwili wako kujiuliza kwa nini imetokea hivi (something like meditation) ukishindwa hii, mshirikishe rafiki yako wa karibu, ndugu au mzazi hakika utapata suluhisho.

Kwenye kipindi hichi ndo utagundua upendo wa mwenzako na kwa bahati mbaya mwanamke awe mpumbavu-hana hekima ya Kimungu au kidunia, ataanza kumdharau mumewe na kutafuta (comfort area) sehemu ya kupumzikia hapa ndo wanatoka nje ya ndoa na aina yeyote ya mtu, iwe kijakazi wa kiume au mtu mwenye kipato hapa kuna vitu viwili anatafuta kufurahishwa kingono au kupata vyote viwili starehe ya kingono na ya kidunia ambavyo vyote kavikosa kwa mume wake na ikumbukwe mwanaume hakufanya makusudi.

Rejea mwanamke mpumbavu huiharibu ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe. Akianza kutoka dharau zinaanza ndani ya nyumba, kumbuka pia mumeo ana marafiki, ndugu wanaomzunguka watamtonya tu, mwanaume na yeye anaona kama mbwai mbwai bana anavunja uhusiano.

Mwisho hua mbaya mara nyingi, si mara zote mwanamke akiachwa kuna mawili mchepuko kumkimbia au kuendelea nae, Kwa bahati nzuri wakiendelea atakuja kugundua alivyotegemea kuvipata kwake havipo anatoka hapo anaenda kwa mwanaume mwingine mwisho wa siku anakua mdangaji (ikumbukwe magonjwa yapo)

Kwa mwanaume baada ya kuachana ataendelea kua na msongo wa mawazo japo akiwa mbele za watu atajifanya anafuahia maisha mapya, ila kiukweli yanamtafuna rohoni kimyakimya utasikia mtu kawa kichaa ghafla, kaanguka pressure ghafla, kupelekea kujiua au kuvizia muhusika na kumuua-iwe kilozi au (physical) kwa mikono yake mwenyewe au kutumiwa watu tumeshuhudia matukio ya aina hii mengi (mke wa mtu ni sumu).

Kuepusha haya wazee wa zamani walikuwa na 'signo' zao wakifika home either aimbe, apige mluzi, agonge miguu chini kutoa vumbi au apite bar ya jirani apige moja alafu amtume mtoto wa jirani apeleke mzigo wowote home hapa mama atajua mzee yupo jirani kama kuna mchepuko ataondoka zake sasa turudi kwetu vijana wananyata kabisa kuingia kwao aisee!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
541
Points
1,000

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
541 1,000
Tuendelee sehemu ya pili...

Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja”. Mwanzo 2:24.

Hapa tunaona kusudi la MUNGU katika suala la kuachana na kuambatana. Wanandoa wanatakiwa kuachana na wazazi wao katika maeneo matatu.

i) Kimwili – wawe na makazi yao wenyewe

ii) Kihisia – wategemeane na kutiana moyo na kusaidiana

iii) Kiuchumi – wajitegemee kwa mahitaji yao ya kila siku.

TENDO LA NDOA

Ukizingatia kanuni za MUNGU kibiblia kuhusu tendo la ndoa kwa wanandoa;-

i) Ni tukio dogo lenye umuhimu mkubwa.

ii) Kusudi kubwa la tendo la ndoa ni uzazi.

iii) Ni kinga dhidi ya majaribu.

iv) Ni burudani/starehe.

v) Ni suala la kuwa na uvumilivvu na kujitoa.

NDOA -TAASISI TAKATIFU

Ndoa yenye furaha na kuheshimika ni ile ambayo kila mmoja anafahamu na kutimiza wajibu wake katika ndoa kwa mujibu wa nafasi yake. Na hii ndio sharti la msingi kutupelekea kwenye ndoa yenye mafanikio.

i) Kumheshimu mwenzi wako kutokana na hadhi aliyonayo kama MUNGU alivyoagiza.

ii) Heshima inasaidia kutuepusha na ubinafsi na kuongozwa na hisia.

iii) Heshima katika ndoa inachochea mapenzi.

NDOA NI KUTOA

1. Ndio sio mkataba wa kijamii bali agano la kiroho. Waefeso 5:31-33 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja. Siri hiyo ni kubwa, ila mimi nanena habari ya KRISTO na Kanisa. Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe, wala mke asikose kumstahi mumewe.

Hapa tunajifunza

i) Ndoa ni fumbo la ajabu la kiroho linalowaunganisha watu wawili, mwanamume na mwanamke (mst.31)

ii) Ndoa ya kikristo inaliganishwa na uhusiano uliopo kati ya KRISTO na Kanisa (mst.32)

iii) Mpango wa MUNGU katika ndoa unahitaji upendo wa kujitoa sadaka kama KRISTO anavyofanya kwa Kanisa (mst.33)

2. Ndoa ya Kikristo ni kujitoa sio kupokea. Wafilipi 2:3-4 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno, bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenzie kuwa bora kuliko nafsi yake mwenyewe. Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe, bali kila mtu aangalie mambo ya wengine.

Hapa tunajifunza

i) Kutokuwa wabinafsi

ii) Unyenyekevu

iii) Roho ya kutoa na kujitoa.

Wewe mume/mke, mahusiano yako na mwenzi wako yakoje? Unampenda mwenzi wako kama KRISTO anavyolipenda Kanisa lake? Kama wewe ni mmojawapo wa wasiofuata kielelezo cha KRISTO katika ndoa usijisikie vibaya kwani hakuna aliye mkamilifu. Hata hivyo wajibu huu haukwepeki kwani ni agizo la MUNGU na lazima kutii maagizo yake, kumpenda MUNGU kwa moyo waklo wote na kwa roho yako yote na kwa akili zako zote na kwa nguvu zako zote. Na kumpenda jirani yako kama nafsi yao. Marko 12:30-31. Hivyo, hii ni nafasi yako ya kumwonyesha mwenzi wako upendo ambao wa muda mrefu ameukosa, upendo ambao KRISTO ameuonyesha kwa kanisa lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
adolay

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Messages
10,908
Points
2,000

adolay

JF-Expert Member
Joined Dec 8, 2011
10,908 2,000
Wala hakuna au wachache tu ndo wanaelewa maana ya ndoa

Wengine wanajuwa kula mtibwa sugar kama kila shamba lote na popote.
 
laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
541
Points
1,000

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
541 1,000
Maana ya ndo kisheria-MAANA YA NDOA
Kwa mujibu wa kifungu cha 9(1), cha Sheria ya Ndoa, sura ya 29 ya sheria za Tanzania, ndoa ni muungano wa hiari kati ya mwanaume na mwanamke unaokusudiwa kudumu kwa muda wa maisha yao yote.

Hata hivyo, muungano huo ili uweze kukamilika kisheria ni lazima mambo ya msingi yafuatayo yazingatiwe, nayo ni:

1. Hiari-kuwe na makubaliano.
2. Kudumu-muungano uwe wa kudumu.
3. Jinsia tofauti
4. Maharumu-hawa ni ndugu wa karibu hawaruhusiwi kuoana.
5. Umri-uwe juu ya 18,ikiwa chini ya hapa kuna maelekezo.
6. Kusiwe na ndoa inayoendelea.
7. Kuwe na mashahidi.
Wazee wa sheria naomba mje mjazie nyama na wazee wa ndoa za kimila hali kadhalika japo mimi naamini kwenye ndoa moja tuu ya Kikristo, Kanisa Moja Takatifu Catholic.

Makala hii sehemu nimeandaa kwa utashi wangu, sehemu nimechukua Maandiko Kutoka katika Bibilia Takatifu na sehemu kutoka katika mamkala ya Jane Lawi Sijaona.

Ni matumaini yangu umepata kitu.

Wasalaam

L. A. I. I
 
BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Messages
710
Points
1,000

BradFord93

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2017
710 1,000
Kosa tulifanyalo n kuoa watu ambao wameshapitia wanaume zaidi ya wawili...!!wengi tunaoa wake za watu...!!yan ukiona hvyo jua umerukia ndoa za watu

Sisemi tuoe walio sealed but angalau tuangalie mwanamke mwenye connection ndogo ya relationshp zlzopita...!!mwanamke akishaachwa na wanaume zaidi ya wawili....fikra na mtazamo kuhusu mwanaume na ndoa hubadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
541
Points
1,000

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
541 1,000
Unaonekana kukata tamaa mkuu, wanaofanya sherehe za miaka 50 ya ndoa waliwezaje. Pitia mafundisho mbalimbali ongea na watu waliokuzidi umri kwenye ndoa watakusaidia. Hakuna ndoa isiyo na mikwaruzo,wanagombana mapacha ije kua huyo mmlielewa familia tofauti, tamaduni tofauti, kabila tofauti
ukifika sehemu ya 100 uni-tag
Sent using Jamii Forums mobile app
 
laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
541
Points
1,000

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
541 1,000
Inategemea ntu na ntu mkuu, kuna watu walipita njia hizo kimakosa na huenda mapungufu hayakua yao, hawa hua wanatulia mno kwenye ndoa
Kosa tulifanyalo n kuoa watu ambao wameshapitia wanaume zaidi ya wawili...!!wengi tunaoa wake za watu...!!yan ukiona hvyo jua umerukia ndoa za watu

Sisemi tuoe walio sealed but angalau tuangalie mwanamke mwenye connection ndogo ya relationshp zlzopita...!!mwanamke akishaachwa na wanaume zaidi ya wawili....fikra na mtazamo kuhusu mwanaume na ndoa hubadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Messages
710
Points
1,000

BradFord93

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2017
710 1,000
Yap wapo lkn co hawa wa sasa....wapo lkn n nadra sana kuwapata....!!mara nyingi alotulia anapata pasua kichwa...!!ndo maana wengi wanasema kuchapiwa mke kupo....ila heshima tu iwepo....sasa tofauti ya hawa wa sasa heshima hawana....unachapiwa na dharau juu

Inategemea ntu na ntu mkuu, kuna watu walipita njia hizo kimakosa na huenda mapungufu hayakua yao, hawa hua wanatulia mno kwenye ndoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
laii

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2016
Messages
541
Points
1,000

laii

JF-Expert Member
Joined Oct 10, 2016
541 1,000
NDOA YA KWANZA YA BABU NA BIBI YETU ADAM NA EVA NA YALE TUNAYOWEZA KUJIFUNZA TOKA KWAO KUIMARISHA NDOA ZETU.

Nikiiangalia na kuitafakari kwa kina ndoa ya kwanza kuna mengi sana najifunza toka kwenye ndoa hiyo ndoa.
Kwanza kabisa hii ndoa ya Adamu na Eva ilitengenezewa mbinguni tungesema kwa kingereza tungesema a marriage made in heaven.
Wazo la hiyo ndoa lilikuwa la Mungu. Mke alitafutwa na Mungu. Infact Mungu alimwambia Adamu mke kwa viwango na mahitaji mahususi ya Adamu. Eva alikuwa ni mke mahususi kwaajili ya Adamu. Ningesema kwa lugha ya wenzetu ningesema Eve was a perfect match for Adam and Adam was a perfect match for Eve. Yaani kwa msingi wa hii ndoa hapakuwa na shida yoyote wala mushkir wowote. Hakika Eva alikuwa mke wa kumfaa sana Adamu na Adamu alikuwa mume wa kumfaa sana Eva. Sio tu walikuwa a perfect match, sio tu ilikuwa ndoa made in heaven, lakini pia waliwekwa kwenye mazingira perfect na hapakuwa na uhitaji wowote.
Katika kuitafakari sana hii ndoa nikafunguliwa macho kuona pamoja na yote haya hata hii ndoa nayo ilikuwa na changamoto zake, changamoto ambazo matokeo yake mabaya wanadamu wanayavuna mpaka leo maelfu ya vizazi baadaye.
Ndoa ni taasisi nyeti kiasi kwamba changamoto zozote ndani ya hiyo ndoa zisiposhughulikiwa vema, athari yake itaendelea kuwepo vizazi na vizazi.
Lakini pia nikagundua kuwa haijalishi mlianza vizuri kiasi gani katika ndoa yenu au mpo vizuri kiasi gani na mnapendana kiasi gani changamoto hazitawaogopa kwa sababu hiyo. Cha muhimu ni ninyi kujitambua na kuwa tayari kukabiliana na hizo changamoto na msiruhusu hizo changamoto zimgeuze mmoja kinyume na mwingine. Kuna mambo ya kina sana nimeyaona kwenye hii ndoa ya kwanza na natamani kukushirikisha. Ila leo nataka nitafakari na wewe jinsi shetani alivyokuja na kuitumia taasisi ya ndoa kuangusha kusudi la Mungu kwa ajili ya mwanadamu.
Katika kuifuatilia hii habari kwenye sura tatu za Mwanzo za kitabu cha Mwanzo, utagundua kuwa Mungu alikwisha kumpa mwanaume wajibu wake yaani assignment yake na mwanaume alipokuwa katika utekelezaji wa assignment aliyopewa na Mungu, Mungu akaona si vema huyo mwanaume awe peke yake akaona amfanyie msaidizi wa kumfaa atakayefanana naye. Wazo la Mungu la kumleta mwanamke kwa mwanaume haikuwa kwa ajili ya kushughulika na upweke wa mwanaume ilikuwa ni kwa ajili ya kujibu hitaji la msaidizi maishani mwake. Huyu mwanaume kwa sababu ya majukumu ambayo alikuwa amepewa na Mungu angehitaji kusaidiwa. Mwanamke aliletwa mahususi maishani mwake kumsaidia Adamu ambaye alikuwa amepewa jukumu mahususi la kuitunza na kuilima bustani. Kwa hiyo Adamu angeilima na kuitunza bustani wakati Eva anamsaidia na kila anachohitaji kwa ajili ya kutekeleza jukumu lake hilo.
Hiyo ndo sababu ya msingi kwanini mwanamke anakuja kwenye maisha ya mwanaume, kumsaidia. Ndani ya nyumba hakuna ndoto kumi. Kuna ndoto moja na hata kama mwanamke atakuwa na ndoto yake sio kwamba ataiua bali ajue hiyo ndoto yake ni kwa ajili ya kusaidia kutimizwa kwa ndoto ya mume wake. Ni muhimu sana haya mambo yafikiriwe kwa kina kabla watu hawajaoana laa sivyo yatakuwa chanzo cha mtafaruku mkubwa sana ndani ya ndoa.
Sishauri kuwa mwanamke auwe ndoto yake ili kumsaidia mumewe ila najaribu kuonyesha wazi kwamba kama mwanamke una ndoto yako basi kwa vyovyote vile Mungu atakuunganisha na mwanaume ambaye ana ndoto zinazohitaji au inayohitaji ndoto yako iisaidie.
Kufanya maamuzi ya kuoa au kuolewa kwa sababu tu ya hisia ya upendo au kwasababu tu umezimia muonekano wa mwanaume au mwanamke haijakaa poa. Itakuja kuleta majanga mbele.
Unapenda anachofanya sawa lakini je una kile kinachohitajika kwa ajili ya kumsaidia afanye anachofanya kama mke?
Sawa mwanaume umempenda huyo mdada, umependa sura yake, umependa umbo lake, umependa ucheshi wake, umependa tabia zake lakini je kila unachotamani mke akusaidie unakiona ana uwezo nacho huyu mdada?
Tukisogea kidogo napenda tukumbushane jukumu na masharti na vigezo la hilo jukumu Mungu alimpa Adamu kama kiongozi wa ile nyumba. Adamu alitakiwa kumwambia mke wake lakini inaonekana hakupata muda mzuri sana wa kumwambia au alimwambia lakini mke wake hakuwa makini sana na vipengele vidogo vidogo vya hilo agizo.
Sasa siku moja wakati Adamu akiwa ameenda kazini na mke wake yupo katika majukumu ya nyumbani kwao, nyoka akaja kumjaribu.
Akamwuliza swali Hawa, eti.....,?
Siku zote shetani akija kwenye ndoa atakuja kuchallenge maagizo ya Mungu na mamlaka ya mume juu ya mke na namna ambayo atafanya hivyo ni kumfanya mke aanze kutilia mashaka agizo ambalo Mungu kalileta kwake kwa njia ya mume wake.
Sasa Hawa hakuwepo wakati Mungu anatoa hili agizo. Ni Adamu ndo alipewa hili agizo ila Adamu alimshirikisha mke wake baada ya mke wake kuja maishani mwake.
Akamwuliza mwanamke:
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? (MWANZO 3:1 ).
Mungu alitoa maagizo mahususi juu ya mti mmoja tu matunda yake yasiliwe. Mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Ila ili amchanganye mwanamke nyoka alimwuliza swali kama elekezi hivi ni miti yote?
Mwanamke akajibu:
Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa. (MWANZO 3:2,3).
Jibu la mwanamke lilionyesha kuwa anajua agizo la Mungu lakini halijui vizuri sana na hapo ndipo shetani alipoona mwanya wa kuingiza ajenda yake. Mungu ni kweli alisema wasiyale lakini Mungu hakusema wasiguse. Athari ingetokea kama wakila sio wakigusa lakini kwa kuwa mwanamke anaamini hata ukigusa utapata athari kama shetani akifanikiwa kumfanya aguse basi na pasitokee madhara yoyote basi atafanikiwa kumshawishi ale ili madhara yaachiliwe.
Akamamshawishi mwanamke kula:
Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya. (MWANZO . 3:4, 5 ).
Yapo makosa mawili makubwa sana yalifanywa na huyu mwanamke wa kwanza ambayo tunaweza kujifunza tusiyafanye ili yasije yakagharimu nyumba zetu na ndoa zetu.
Kwanza kabisa huyu mwanamke alifanya maamuzi katika jambo ambalo alikuwa na maelekezo mahususi kutoka kwa mumewe asifanye. Jibu sahihi la Hawa hapa lilitakiwa kuwa ngoja mume wangu arudi toka kazini ntamshirikisha hili alafu wewe njoo kesho ntakuwa na jibu la ndio au la. Hawa akafanya kosa la kufanya maamuzi bila ya kumshirikisha mwenzie na zamu hii uamuzi aliyoufanya uliwagharimu sana na uliigharimu historia nzima ya mwanadamu.
Mama, upo kwenye ndoa sasa. Acha kuwa na deal za siri. Acha kufanya maamuzi peke yako. Mshirikishe mume wako. Pata mtazamo wa mume wako. Pata opinion yake. Kwa nafasi yake kuna vitu hiyo nafasi yake inampa kujua na kusaidia ili usije ukaingia kwenye matatizo yasiyo ya lazima.
Kosa lingine ambalo tunaliona lilifanywa na mwanamke ni:
Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. (MWANZO . 3:6 ).
Alifanya uamuzi kwa kuzingatia tu vile anavyojisikia bila ya kujali kile anachojua.
Ndo maana ni muhimu sana mume na mke kushauriana. Maamuzi ya wamama mengi ni ya kihisia na ya wababa mengi ni maamuzi yanayosimama kwenye taarifa zilizopo. Ni tulivyoumbwa na ndo utaofauti wetu. Uamuzi mzuri siku zote kwenye nyumba unahitaji vyote hivi viwili, hisia na kufikiri na kuchakatua taarifa zilizopo.
Laiti angemwambia nyoka angoje ashauriane tena na mumewe sijui leo tungezungumza nini maana hata kama Hawa asingeelewa Adamu angetumia sasa nafasi yake kama kichwa kusema sitaki kuliona hili wala kulisikia tena na hilo soo lililotokea lingezuiliwa kwa njia hiyo.
Shetani alifanikiwa kwa kuwa hapakuwa na kushauriana katika kufanya maamuzi na mwanamke akadanganyika.
Sasa huyu mdada alipokuja kwa mkaka, cjui nini kilikuwa kinaendelea kwenye kichwa chake maana yeye hakudanganywa. Alikula tunda huku akijua wazi anafanya nini. Iko kama alisema basi kama ndo ushaharibu, tufe wote. Sitaki kulisemea sana hili leo ntakuja kulisemea wakati mwingine.
Mama usifanye maamuzi kwa kumficha mumeo. Pata opinion ya mume wako usije ukafanya maamuzi ambayo yataigharimu nyumba yenu na ndoa yenu. Kama uamuzi wako unajua wazi utaiathiri nyumba yako usiifanye peke yako shauriana na mumeo hata kama hajaokoka maana ni mume wako na hiyo ni nafasi, ni ofisi na huyo mwanaume yupo hapo.
Tafuna na mnofu huo ukishameza ntakuletea na mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Andie

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Messages
436
Points
1,000

Andie

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2011
436 1,000
Uzi bora wa week

mzushi flani

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2020
Messages
267
Points
500

mzushi flani

JF-Expert Member
Joined Jan 20, 2020
267 500

mkuu hao waliwekana ndani bana, hawakufunga ndoa.
 
youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Messages
2,894
Points
2,000

youngkato

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2014
2,894 2,000
"Kuepusha haya wazee wa zamani walikuwa na 'signo' zao wakifika home either aimbe, apige mluzi, agonge miguu chini kutoa vumbi au apite bar ya jirani apige moja alafu amtume mtoto wa jirani apeleke mzigo wowote home hapa mama atajua mzee yupo jirani kama kuna mchepuko ataondoka zake sasa turudi kwetu vijana wananyata kabisa kuingia kwao aisee!"

Kweli shetani hapendi ndoa,
Maana nikijitahidi kuoa nakutana na vikwazo vingi sana
 
Brain-app

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Messages
2,494
Points
2,000

Brain-app

JF-Expert Member
Joined Jul 22, 2018
2,494 2,000
Na kosa wanalofanya wanawake ni kuolewa na wanaume waliopita kwa wanawake zaidi ya wawili,wanaolewa na wanaume za watu wengine.
Kosa tulifanyalo n kuoa watu ambao wameshapitia wanaume zaidi ya wawili...!!wengi tunaoa wake za watu...!!yan ukiona hvyo jua umerukia ndoa za watu

Sisemi tuoe walio sealed but angalau tuangalie mwanamke mwenye connection ndogo ya relationshp zlzopita...!!mwanamke akishaachwa na wanaume zaidi ya wawili....fikra na mtazamo kuhusu mwanaume na ndoa hubadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app
 
jogi

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2010
Messages
24,007
Points
2,000

jogi

JF-Expert Member
Joined Sep 25, 2010
24,007 2,000
Mnaopewa vyeti vya ndoa kabla ya kuufanya mtihani wenyewe (kuyaishi maisha ya ndoa) ndio mnakuja na manadharia meeeeengi!

MAISHA HAYANA KANUNI MOJA ITUMIWAYO NA WOTE.
 
Forum statistics

Threads 1,389,758
Members 528,022
Posts 34,033,839
Top