Kwanini Nassari atashinda kwa 65%? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini Nassari atashinda kwa 65%?

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by EasyFit, Mar 14, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Amezaliwa pale,
  Ni mwenyeji wa pale wazee kwa vijana wanamjua,
  Anakubalika hata na wazee wa CCM.

  .......................................[​IMG]
  Mfuasi wa CCM, Ester Leusha akimuombea dua Mgombea Ubunge Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari baada ya kumaliza kuongea na wananchi wa kijiji hicho jana na kuwaomba wampigie kura katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
   
 2. +255

  +255 JF-Expert Member

  #2
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Utabiri kama huu hata TMA wanafanya...
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Mar 15, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Huu utabiri kiboko aise!! Yaani kushikwa kichwani tu tayari atashinda kwa 65% hata Sheikh Yahya hakufikii.
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,030
  Likes Received: 2,677
  Trophy Points: 280
  (1)Anatokea chama makini kisicho na mafisadi,
  (2)Wananchi wamechoshwa na CCM kwa wizi,unyonyji,uuwaji,uonevu nk.
   
 5. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #5
  Mar 15, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hajatoboa sikio
   
 6. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #6
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Naona umemkumbuka sheikh Yahya mlinzi wa JK.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Mar 15, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  To be honest in relation to the current wave of politics and globe, these are not constructive logic and standing point.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  vice versa also is true
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Mar 15, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Kawaida ya waabudu mizimu siyo kosa lao. Na kama yule bibi ametumwa ili ammalizeje? au hilo haliwezekani? NASSARI KWISHA. SIOI JUU, JUUU, JUUUU ZAIDI.
   
 10. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #10
  Mar 15, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Kenge lisilotaga
   
 11. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #11
  Mar 15, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  MJANE wa mpigania Uhuru wa Tanganyika, Nderetwa Kirilo (85), amekutana na mgombea ubunge wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari na kumshika kichwa kama ishara ya kumkubali na kumtaka kulinda haki za Wameru kama alivyokuwa mume wake Japhet Kirilo.

  Akizungumza jana nyumbani kwake katika Kata ya Poli, mara baada ya kukutana na Nassari, Nderetwa alisema, atamkubali hata kama ni mgombea Ubunge kwa tiketi ya chama kingine ambacho sio tawala, ili mradi alete maendeleo kwa watu wa Meru.

  Alisema mume wake Kirilo aliyezaliwa mwaka 1921 na kufariki Mei 30, 1997 alishirikiana na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na hata wakati mwingine alilala kwake wakiwa katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika.

  Alikumbushia kuwa Wameru walichangisha fedha walizoweka ndani ya chungu maalumu na kumwezesha Kirilo kwenda Umoja wa Mataifa (UN) kudai haki ya ardhi ya Wameru.

  Alisema kuwa mume wake aliyeacha udaktari na kuingia katika siasa, alikuwa mwanaharakati wa siasa aliyetetea watu wa Meru, ambao walimchangia kwa moyo mmoja na kupata nauli ya kwenda UN kudai ardhi ya Wameru.

  "Nassari amejitokeza katika siasa na kugombea nafasi hii ya kutuwakilisha mimi nambariki ili Mungu amtangulie na akienda bungeni awe chachu kwa kutetea ardhi ya Wameru," alisema.

  Nassari alimshukuru Nderetwa na kumuahidi kuendeleza aliyoasisi Kirilo kwa kutetea haki za Wameru hasa katika suala la ardhi.

  Akiomba kura katika kata ya Songoro, katika kijiji cha Sura na kijiji cha Ndatu, alisema kuwa endapo atachaguliwa atawatetea bungeni kuhakikisha fedha zilizoliwa na wajanja za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Sh milioni 26 za ujenzi wa barabara ya Nkoakirika hadi kijiji cha Sura zinapatikana na kufanya kazi iliyokusudiwa.

  Gazeti la Habari Leo.
   
 12. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #12
  Mar 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,800
  Likes Received: 17,886
  Trophy Points: 280
  Matokeo mazuri ya Nassari tunayo kwenye Briefcase, tunaendelea kuya-edit tuuuuu
   
 13. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #13
  Apr 1, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Bado naamini Nassari atashinda kwa asilimia 65.
   
 14. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #14
  Apr 1, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  ushindi wa nassari ni asilimia 80,itapungua mpaka 65 kutokana na uchakachuzi.
   
Loading...