Kwanini namwamini Zitto kuliko ninavyoiamini CHADEMA...!

Dijovisonjn

JF-Expert Member
Nov 14, 2011
466
125
Kwanza naomba niseme wazi kabisa kuwa mimi sio mwanachama wa CHADEMA lakini pia sijawahi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa, ila nakumbuka nilipokuwa form one (2003) (kipindi hicho naishi Muleba) Viongozi wa CHADEMA walikuja wilayani Muleba (mjini) (Nakumbuka alikuja Mbowe, Mzee Ndesamburo na wengine siwakumbuki) nakumbuka kuna mtu I think ni Mbowe alituomba tulikuwa pale uwanjani (Uwanja wa red cross Muleba) tukiunge chama mkono kwa kujiunga nacho kwa kununua kadi za uanachama ili tuwe wanachama kamili na nakumbuka huyo mtu (Mbowe?) alimuomba Mzee Ndesamburo atununulie kadi wana Muleba na mzee Ndesamburo alikubali hilo ombi.

Nakumbuka watu wengi sana tulienda kuchukua kadi ila sina uhakika kama wote waliopewa kadi bado ni wanachadema mpaka leo (Binafsi sikupewa kadi kwa sababu nilionekana bado mdogo sana ila niliambiwa nikifikisha miaka kadhaa nitapewa!) Na tokea siku ile nilitamani kuwa mwanachadema hali ambayo nahisi nitazidi kuwa nayo lakini mpaka sasa nikiwa na umri zaidi ya miaka 25 nikiwa na elimu ya chuo kikuu bado si mwanaCHADEMA japo ndoto zangu ni kuwa mwanachadema!!! KWA NINI MIMI SIO MWANACHADEMA MPAKA LEO HII?! Jibu ni moja tu SIJAWAHI KUIAMINI CHADEMA kama CHADEMA (as a political party) ila niliwahi kuwaamini baadhi ya wanachadema, niliwahi kumwamini Mbowe, Slaa Lissu n.k na mpaka leo ninamwamini Saana Zitto!

Kwa nini namwamini Zitto na siiamini CHADEMA?!

Kuna dhana inajengwa humu eti CHADEMA sasa hivi ni taasisi na kama kuna mtu alimfuata mtu ndani ya CHADEMA basi aondoke naye!!! kwanza kabisa sababu kuu iliyopo nyuma ya watu/mtu kujiunga na chama cha siasa si jina la chama, sera, kanuni wala taratibu za chama refer (http://ndialbania.org/files/Joining a Political Party - Recruiting and Keeping New Members.pdf) watu wanajiunga na vyama vya siasa kwa kufuata watu wenye ushawishi mfano Dr. Slaa, Zitto, Mnyika etc, watu wanajiunga na vyama kwa ajili kwa kupata maslahi fulani mfano Shibuda, na watu wanajiunga na chama kwa vile tu wenzake ni member wa kile chama mfano Wachanga!




Hivyo basi kuna watu ni wanachama wa CHADEMA kwa sababu ya Slaa, Mbowe, Zitto n.k.

Mimi ni shabiki wa CHADEMA mpaka leo hii kwa sababu ya Zitto, kwanza Zitto ndiye aliyekuwa kiongozi ndani ya CHADEMA anayeifunika dhana ya ukanda walau hata sisi tusiotoka kasikazini tulijiona tuna mwakilishi ndani ya CHADEMA, Zitto huyu huyu ndiye aliyeifunika dhana ya udini ndani ya CHADEMA kwa kutuonesha sisi waislamu kuwa tunayemwakilishi ndani ya uongozi wa CHADEMA, Zitto ndiye aliyetuonesha vijana kwa vitendo kuwa vijana we can do it! na ni Zitto huyu huyu anayeifunika dhana kuwa CHADEMA kinaongozwa na watu walioishia form four na wengine form six waliojitahidi sana basi wao wana degree za dini! Na ni Zitto huyu huyu aliayeiamsha serikali iliyokuwa imeisahau mikoa ya pembezoni mwa nchi sasa mpaka hapa ni kwanini nisimwamini Zitto bila CHADEMA na Niiamini CHADEMA yenye viongozi kama mchungaji Msigwa, Lema, Sugu na Mbowe?!

Ni kwanini nisimwamini Zitto anayetaka vyama vya siasa vikaguliwe matumizi yake niiamini CHADEMA inayoona kukaguliwa ni kuvuliwa nguo hadharani?! kwa nini nisimwamini Zitto anayetaka wale walioficha pesa nje wazirudishe nchini niwaamini CHADEMA wanaoshirikiana na wale walioficha pesa kumwadhibu Zitto?!

MWISHO: I TRUST IN ZITTO.
 
Ninachokiona kwenye hoja yako kwa mbali ni udini,ukabila na ukanda. Infact usimwamini binadamu mwenzie, muamini Allah, maana yeye ndo kila kitu! Pia zitto wa miaka ile sio yule!
 
Kila mtu ana story yake jamani! Mimi nilikuwa naiamini CDM ya Marehemu Mzee Eshton Nkala, huyu alikuwa mwanzilishi wa CDM wilayani Kasulu, nadhani ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa wilaya kipindi hicho.

Lakini hii ya Mwenyekiti wetu wa hapa Kasulu, Bwana Bujoro ni ya kimaslahi zaidi, maana Mw Bujoro mwenyewe ana kashfa za ujambazi, uzulumati na hata darasa la saba hajamaliza. Sasa nikiangalia viongozi wa wilaya kama ndio hawa, na wamekubalika kitaifa napata walakini wa huo uongozi wa kitaifa unaowakubali hawa.

Unajua sisi ambao hatujui huko Dar mnaishije ishije, maana hatujawahi kuja huko huwa tunajiuliza hivi mnapata taarifa za viongozi wenu wa huku? Maana tunashangaa jinsi ambavyo kuna watu wanajimilikisha vyama halafu hawana uadilifu unaozungumzwa na Chadema taifa.

Nawaza, je kama ndio zile za kama mwana kama baba (Like son like father)! Si ni balaa.
 
safi sana dogo ! utawaona wajinga walioaminishwa kwenye ujinga watakuja hapa kujifanya wanakukatisha tamaa-lakini ulichosema ndio ukweli na hakuna hata mmoja atakayekujibu kwa hoja, nakuhakikishia.
 
Mkuu hata mimi nakuunga mkono, kuna watu wana chuki binafsi na Zitto. Tuhuma zote zinazoelekezwa kwa Mwenyekiti na Katibu mkuu wa CDM toka enzi za marehemu Chacha Wangwe mpaka leo (rejea waraka wa Chacha Wangwe) hawazioni wao wanachoona ni Zitto tu. Hata kauli ya makamu mwenyekiti alipojiuzuru kwa kuchoshwa na unafiki ndani ya CDM hawaiongelei kabisa wao kutwa nzima Zitto!

Kuna ambao wana masilahi binafsi kama Lissu maana dada yake ni mbunge wa kuteuliwa hivyo siwezi kumshangaa , Lema siwezi kumshangaa maana ndivyo alivyo lakini wengine kama Mch. Msigwa tulitegemea busara zaidi ya tunayoyasikia toka kwake. Si vizuri kendelea kumchafua kiongozi mwenzako wakati maamuzi hayajatolewa, what if baraza kuu likitengua maamuzi ya kamati kuu, watasema nini? Unless wana uhakika kuwa atafukuzwa!

Nadhani wabunge wa CDM wanaotokea kanda ya ziwa wamesoma alama za nyakati na kukaa kimya juu ya mgogoro huu maana wanajua ambacho wapiga kura wao wanakifikiria. Ngoja wana CDM wachache waliopo makao makuu waendeleze propaganda kuwa CDM iko imara, kilio kitawaumbua 2015. Waenga walisema ajidhaniae amesimama na aangalie asianguke!
 
mkuu mimi ni mkristo wa kilutheli bhana! na mhaya toka kanda ya ziwa!
alaf hebu acheni kum-overwork Mungu wetu yaani unataka na maswala ya siasa nimwachie Mungu?!

Ninachokiona kwenye hoja yako kwa mbali ni udini,ukabila na ukanda. Infact usimwamini binadamu mwenzie, muamini Allah, maana yeye ndo kila kitu! Pia zitto wa miaka ile sio yule!
 
Ni kweli mkuu coz Slaa wa 2007 si Slaa wa 2013!
People do change mkuu ukimtumainia binadamu utapotea. Wapenzi wanaouana hawakutongozana kwa mtutu. Rafiki yako mkubwa aweza kuwa adui.
So jitafakari upya vinginevyo bado sana mkuu
 
'I TRUST IN ZITTO' hapo ndipo ulipokosea mkuu,trust in UWAJIBIKAJI WA ZITTO na don't trust in ZITTO...when you trust in uwajibikaji wake siku asipowajibika itakuwa rahis kutom-trust lakin when you trust in zitto maana yake hata afanyeje you will keep on trusting him...ushauri tu.!!
 
Kwa hiyo nisipomwamini Zitto ndo nitakuwa na uwezo mzuri wa kufikiri?!

ila mkuu, mleta mada ana point kiasi flani......tafakari, ni kwa nn tuhuma za usaliti za zzk ni za kihisia zaidi, sijawahi kuona vielelezo vya usaliti wenyewe.tutende haki wanaCDM, kama chama kina ushahd kiulete kwa wanachama ili muhusika ahukumiwa kihalali. imefikia mahali wengine tunaamini haya yote ni kwa sababu ya uchaguzi mkuu ujao ndani ya chama tuu!
 
Mkuu nilikuwa njiani kuandika uzi wenye maudhui kama ya kwako sema umeniwahi.
Hata hivyo mimi nikama wewe ulivyo mimi siamini katika chama bali naamini katika watu. Chadema kama chama changu tawala kimeanzisha na watu ambao wamejitahidi sana katika kuweka misingi mizuri inayoashiria kuwa ina lengo la kuwasaidia wananchi lakini wanaokwamisha mipango hiyo ni nani kama si walewale walioiweka? CCM ni chama chenye sera nzuri sana tena kupita chama cha demokrasia na maendeleo, kumbuka na hata DR SLAA alivyokuwa ulaya alihojiwa swali kuwa anataka kuifanyia nini Tanzania ambacho CCM hawajakifanya nae bila hiyana akasema CCM ni chama chenye sera nzuri sana ila kimekosa watu wa kutekeleza sera hizo. Hivyohivyo kwa CDM nao wanasera nzuri makaratasini lakini matendo ya baadhi ya viongozi wake ni tofauti na sera za chama. Hata wale waliojitokeza wazi na kuanza kuonyesha kivitendo ndio wanaoneeekana ni wasalii. Kwanini nisimuamini ZItto ambaye amesimama kidete kuwatetea wanyonge bila kujali hata dini,kanda,kabila wanazotoka na badala yake nimuamini Mtei aliyetoa kauli za kidini katika kamati iliyounda ya maoni ya katiba? nimuamini Lema aliyepeleka chuki za kidini mpaka bungeni? Anaelilia posho kinyume na msimamo wa chama chake? Kwanini nisiamini katika mtu na kuamini taasisi wakati taasisi hiyo inaacha misingi yake na kufanya kinyume na matarajio ya watu? CDM ina lipi la kuwaaminisha watanzania kuwa ina lengo la kuwasaidia wakati wale inaowatuhumu @ ni wala rushwa,wamehongwa brifcase n.k imeshindwa kuwashughulikia?

NINAZO SABABU NYINGI SANA ZA KUAMINI KATIKA WATU KULIKO TAASISI. NAKUAMINI ZITTO.
 
Yeah that true mkuu thanks kwa kunirekebisha!
 
Bottom line ni kwamba keep your trust intact na mchukue ukaishi naye muanzishe Chama cheni ambazo si cha Udini, Ukanda na mengiyo na atakuwa mwenyekiti wenu maana ana mvuto mtavuta na wengine waje mkae nao na muishi bila katiba wala nidhamu acheni kupoteza muda wenu hapa jf watu wako bize na issue bwana .Zitto ndiyo kitu gani ?
 
Kila mtu ana uhuru wa kumuamini mtu yeyote yule anayemtaka.
Hivyo, everybody, feel free to trust any one.
 
Pokea like yangu mkuu!
 
Wewe ni dini gani? unafuata mtu baadala ya sera ya chama husika msomi gani wewe unakuwa mbulula hivyo au umesoma udsm maana ndo wanaongoza kutoa mambulula siku.
 
Mkuu siasa haiendi hivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…