Kwanini namba 5 kwenye batani za simu ina vinundu viwili?

fundibaskeli

Member
Nov 9, 2016
84
115
Kwanini simu zote za battani kwenye namba namba tano huwa kuna doti mbili...

Hizi zina maanisha nini
a67982d14ac6038b01dc24afb9053f67.jpg
 
Hio alama pia zipo kwenye keyboard za PC kwenye J na F, kwenye simu unajua uko katikati ya keypad yako na hata bila kuangalia unaweza kujua au kwa wenzetu wenye matatizo kwenye kuona. Kwenye PC hizo herufi ndipo vinapokaa vidole vya shahada hivyo inaweza kumsaidia mtu kubofya bila kuangalia.
 
Hyo ni kwa ajili ukiwa unatype msg bila kuangalia buttons ujue upo sehem gan ili usikosee kuandika hata kwenye keyboard ya computer zipo hizo alama lengo kama unatype bila kuangalia thn ukaipoteza picha ya keyboard kichwan ukizigusa zile unajua pakuanzia
 
ni Guidance kwa wasioona, hata kwenye PC , key F, J na 5 kwenye number pad huwa zina alama
 
Hio alama pia zipo kwenye keyboard za PC kwenye J na F, kwenye simu unajua uko katikati ya keypad yako na hata bila kuangalia unaweza kujua au kwa wenzetu wenye matatizo kwenye kuona. Kwenye PC hizo herufi ndipo vinapokaa vidole vya shahada hivyo inaweza kumsaidia mtu kubofya bila kuangalia.
Sawa kaka nashkuru nmekupata
 
Kwahiyo hata namba tano 5 ya touch screen nayo ina vinundu viwili?
Kuwa specific na aina ya simu unayoizungumzia kupunguza wingi wa wachangiaji wasiokuwa na eksipiriensi na simu hizo.
 
Back
Top Bottom