Kwanini nahisi watu wote wa JamiiForums wapo Dar?

Mimi nipo Kijiji cha Itete, Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro
shughuli kubwa za kiuchumi katika eneo hili ni kilimo cha mpunga, na uvuvi wa samaki katika mto kilombero. Vile vile wapo ndugu zetu wakisukuma ambao wanajishughulisha sana na ufugaji wa ng'ombe ila kwa sasa wengi wao wamechangamka tofauti na miaka ile ya nyuma. Wengi wao kwa sasa wanamiliki frame zao za maduka maeneo ya Ifakara.
karibuni sana mje muwekeze kwenye Kilimo, maeneo ya kulima bado mengi mno.
 
Back
Top Bottom