Kwanini mwanamke akimtongoza mwanaume huchukuliwa kama malaya ?

Mgegedo

Member
Joined
Jan 19, 2018
Posts
91
Reaction score
89
Kuna wanawake ambao wameumbwa na ujasiri wa kumtongoza mwanaume pindi wanapoona wamevutiwa na mwanaume huyo kimapemzi.

Mwanamke mwenye ujasiri wa namna hii huwa hasiti kumfuata mwanaume na kumueleza ukweli pindi anapoona amevutiwa nae kimapenzi

Pamoja na ujasiri wa wanawake hawa kufanya hivi lakini jamii huwa inawachukulia tofauti kidogo na wakati mwingine huonekana kama wanawake malaya au wanawake ambao wanakiuka mila na desturi za kiafrika ambazo zinaamini kwamba mtoto wa kike ni lazima atongozwe na mwanaume na sio mwanaume atongozwe na mwanamke.

Ukiwa kama kijana ni upi mtazamo wako katika suala hili ?

Karibuni
 
Ikiwa Wanawake wa leo hii wanaweza kukupangia majukumu yako ktk ndoa kwa madai ya haki sawa basi hata kukutongoza hawataona soo yoyote.
 
Wakuu nyie mnaotongozwa tupeane mbinu... wengine tunatongoza tu toka tuzaliwe.

Rukeni mbinu ya kuwa na pesa hili limeshatukaa saana mahubiri yanatosha.
 
Sheria za asili ndivyo zinavyopelekea iwe hivyo kwamba mwanaume ndiye anayetakiwa kumuanza mwanamke!

Hii ipo tangu kungali kuumbwa kwa binadamu wa kwanza!

Adam ndiye alimuanza Hawa!

Adam ndiye alianza kumjua Hawa!
 
Ndo tabia walizoubwa nazo
Anaweza akakupenda sana lakini kusema ikawa ngumu japo ishara unaziona kabisa ndo pale utakapomtongoza kidogo t hawez kataa
 
Mitongozo yangu yote huioni....?
Wakuu nyie mnaotongozwa tupeane mbinu... wengine tunatongoza tu toka tuzaliwe.

Rukeni mbinu ya kuwa na pesa hili limeshatukaa saana mahubiri yanatosha.
 
Kuna wanawake ambao wameumbwa na ujasiri wa kumtongoza mwanaume pindi wanapoona wamevutiwa na mwanaume huyo kimapemzi.

Mwanamke mwenye ujasiri wa namna hii huwa hasiti kumfuata mwanaume na kumueleza ukweli pindi anapoona amevutiwa nae kimapenzi

Pamoja na ujasiri wa wanawake hawa kufanya hivi lakini jamii huwa inawachukulia tofauti kidogo na wakati mwingine huonekana kama wanawake malaya au wanawake ambao wanakiuka mila na desturi za kiafrika ambazo zinaamini kwamba mtoto wa kike ni lazima atongozwe na mwanaume na sio mwanaume atongozwe na mwanamke.

Ukiwa kama kijana ni upi mtazamo wako katika suala hili ?

Karibuni
Binafsi napenda kutongozwa na mwanamke
 
Back
Top Bottom