Kwanini mtoto aliye na umri wa chini ya miaka 10 hapaswi kupelekwa shule za bweni

Sema Tanzania

JF-Expert Member
May 18, 2016
251
465
Zipo sababu lukuki kwanini tunawapeleka watoto wetu shule za bweni ikiwa ni pamoja na kufiwa na wazazi wao, majukumu ya kusaka riziki kwa wazazi, elimu bora na zingine kadha wa kadha. Leo tutajadili athari za shule za bweni kwa watoto wenye umri mdogo. Umri wa chini ya miaka kumi na vipi elimu ya bweni inaweza kuwa ama chachu ya maendeleo ya mtoto au kumdidimiza kabisa kimaendeleo.

Tuanze kwa kuangalia nini mtoto anaweza kufanya kulingana na umri wake na tutahitimisha na maoni yetu kuhusu umri wa shule ya bweni.Kuanzia umri wa miaka miwili hadi minne, mtoto huwa hajawa na ufahamu wa kutosha kujua mabaya na mema. Anachokipenda yeye ndicho kizuri na asichokipenda sio kizuri. Ni muhimu mzazi kuelewa hili ili kutoa muongozo na uangalizi kwa mtoto kwa upendo pasipo kumuhukumu kuwa ana tabia mbaya kwani bado uwezo wa kupambanua baya na jema ni mdogo mno.

Ingawa bado hajawa na uwezo binafsi wa kung’amua mwenyewe mambo mema na mabaya, mtoto mwenye umri wa miaka mitano hadi sita anaweza kufuata maelekezo ya mzazi vyema zaidi. Mtoto wa umri huu anaamini kila anachosema mzazi. Bado hana uwezo wa kujua kwa utashi wake mwenyewe lakini anao uwezo mkubwa wa kufuata maelekezo ya mzazi/mlezi. Wataalamu wa makuzi wanashauri wazazi wawe makini katika kutoa maelekezo katika umri huu kwani unachomweleza huwa ni kama mbegu unayoipanda maishani mwake. Misimamo yako katika yale unayoyaamini kama ibada, aina za vakula, nk. kwake hupokelewa kama kilivyo.

Umri wa miaka saba mpaka minane, mfumo binafsi wa kung’amua jema na baya wa mtoto unaimarika. Anaanza kujua mifumo ya maisha ya jamii husika na anao uwezo wa kuelewa madhara ya kutenda mabaya. Mara nyingi katika umri huu, wataalamu wa makuzi wanaeleza kuwa kutotenda makosa hujengwa katika uoga wa adhabu zinazotolewa na si kwa sababu nyinginezo. Kwa mfano, mtoto anajua kuwa sababu kubwa ya watu kutokuiba ni kukamatwa na polisi na si kwa sababu maadili mema yanaelekeza hivyo. Mara nyingi unaweza kusikia watoto wa umri huu wakitishiana kuwa wakifanya hivyo watakamatwa na polisi au mzazi atawaadhibu. Kama mzazi, ni vyema kumuelewesha mtoto kuwa watu hawaibi kwa sababu wanaogopa polisi tu bali wizi ni tabia mbaya na si maadili mema.

Jambo jema katika umri wa kuanzia miaka tisa na kuendelea, ni mtoto anaanza kuelewa maumivu ya kutenda kosa na faraja ya kutenda mema. Kadiri alivyolelewa, mtoto huumia anapotenda jambo analohisi si jema. Uelewa wa dhana ya kuwa ‘watendee wengine vile ambavyo ungependa utendewe wewe’ huingia, kwahiyo ni vyema mzazi/mlezi kuwa mfano mwema kwa mtoto. Usimtendee vitendo vya kionevu mtoto ukidhani kuwa haelewi, anaelewa. Jitahidi kutenda haki kwani utamuandaa kupenda kutenda haki kwa wengine. Hii ni kutokana na ukweli kwamba watoto wanajifunza kwako zaidi kuliko mtu mwingine. Muongoze mtoto awe na uelewa wa kung’amua jema na baya pasi kushurutishwa.

Kutokana na mifano hiyo ya kitaalamu kuhusu uwezo wa mtoto sanjari na umri wake, inakuwa rahisi kwetu kushauri kwamba iwapo sababu za kumpeleka mtoto shule ya bweni kabla ya umri wa walau miaka zaidi ya 10 zinaweza kuepukika, muache asome shule ya kutwa. Hii ni fursa adhimu kwako kupanda mbegu ya matarajio yako katika maisha ya mwanao kwani unapata kujenga ukaribu siku hata siku. Ikishindikana kuwa naye katika shule ya kutwa, basi hakikisha unajenga ukaribu na waangalizi/waalimu wake huko anakoishi ili angalau ujue namna bora ya kuhakikisha makuzi kwake.

Kwa maoni na ushauri tupigie simu namba 116, ambayo ni maalumu kwa huduma za mtoto nchini. Huduma hii haitozi malipo toka mitandao yote nchini. Vilevile unaweza kutupata kupitia ukurasa wetu wa Facebook: Sema Tanzania; Twitter: @SemaTanzania na www.sematanzania.org
 
Mchango mzuri sanaa.....ila ni 'too theoretical' and 'bookish type' maisha ya binaadamu hususani sisi wa Africa ni complicated sanaa hayako set kihivyo.........kwa mfano watoto wanao soma English medium za bweni tangu darasa la kwanza wana nidhamu utii kwa wazazi wao na wengi wanafanikiwa kimasomo, ukilinganisha nahao wanao soma shule za kayumba, wanazurura vibaka na wengine wakike wapata ujauzito wakifika darasa la sita au saba wakati wanaishi na wazazi wao nyumbani......
 
Unaonekana km ni mzazi ni mzazi wa dot com,ulimbukeni na mtu wa mikogo.
Ushauri wa bure tu,nidhamu ya mtoto hajengwi shuleni bali nyumbani
 
Mchango mzuri sanaa.....ila ni 'too theoretical' and 'bookish type' maisha ya binaadamu hususani sisi wa Africa ni complicated sanaa hayako set kihivyo.........kwa mfano watoto wanao soma English medium za bweni tangu darasa la kwanza wana nidhamu utii kwa wazazi wao na wengi wanafanikiwa kimasomo, ukilinganisha nahao wanao soma shule za kayumba, wanazurura vibaka na wengine wakike wapata ujauzito wakifika darasa la sita au saba wakati wanaishi na wazazi wao nyumbani......

Wazazi wote wanaopeleka watoto wadogo Bweni ni evil people na wanafaa kuondolewa vizazi, kwa maana wamelaaniwa, kama huwezi kumfundisha mtoto wako nidhamu iweje utegemee wengine wafanye hiyo kazi?

Shule za Bweni ni kwa watoto yatima tu!
 
Hahaha zamani nami nilidhani shule ni lazima, nilipotoka nje nikakuta mfumo wa home schooling unafanya kazi vizuri na,watoto wanaweza kujua kusoma na kuandika na wana compete mitihani ya kitaifa sawa wale waendao shule, nikasema kumbe shule na ada ni sawa na muuza duka tu, zote biashara.
Kumbe akili haziletwi na shule, ndio maana labda Bili Gate aliachana na ujinga huo akaanzisha biashara.
 
Ndo uwe na miundo mbinu ss ya home schooling ili wapate uelewa tarajiwa ama wawe zaidi ya wengine

Je hawatokua anti social?..
Kuna dhana ya kuchangamana na watoto wa rika yake na wa jinsia tofauti shuleni
 
Wazazi wote wanaopeleka watoto wadogo Bweni ni evil people na wanafaa kuondolewa vizazi, kwa maana wamelaaniwa, kama huwezi kumfundisha mtoto wako nidhamu iweje utegemee wengine wafanye hiyo kazi? fvck you!

Shule za Bweni ni kwa watoto yatima tu!
Si kweli
Inategemea na malengo mahsusi na mazingira
On average bora shule ya kata day anapanda daladala ama bora boarding?..

Akiwa day hakikisha usafiri wa school bus kwa usalama zaidi wa mtoto

Shule za seminari boarding zina afadhali kuliko zisizokua na mrengo wa dini
 
Kama kweli unampenda mtoto wako, ungependa kuwa naye na kumuona kila siku, nje ya hapo haustahili kuwa mzazi na wala hauna mapenzi na mwanao.

Shule za Bweni ni sawa kama mtoto ni yatima na hana mtu tena wa kumwangalia yaani yuko Mtaani, hivyo ni bora kwake angalau awe na sehemu ya kulala na kusoma pia klk kulala barabarani.

Mimi sina mtoto bado lkn kama ningekuwa naye hakuna siku ningelala bila ya kumuona hasa akiwa mdogo bado hivyo nashindwa kuelewa mzazi kuruhusu mtoto wake wa kuzaa alalelewe mbali na bila ya kumuona, mwisho wa siku huyo mtoto atakuwa kalelewa Shule na siyo wewe, hivyo ni sawa na yatima tu.
 
Ndo uwe na miundo mbinu ss ya home schooling ili wapate uelewa tarajiwa ama wawe zaidi ya wengine

Je hawatokua anti social?..
Kuna dhana ya kuchangamana na watoto wa rika yake na wa jinsia tofauti shuleni
Hahaha kuchangamana huku mtaani hili suo tatizo, tatizo hilo liko magetini kule masaki.
Mfumo huo hapa kwetu haupo na haukubaliki lakini huko kwa waliotuletea mambo haya ya mifumo ya shule waliisha uweka upo.
 
Mchango mzuri sanaa.....ila ni 'too theoretical' and 'bookish type' maisha ya binaadamu hususani sisi wa Africa ni complicated sanaa hayako set kihivyo.........kwa mfano watoto wanao soma English medium za bweni tangu darasa la kwanza wana nidhamu utii kwa wazazi wao na wengi wanafanikiwa kimasomo, ukilinganisha nahao wanao soma shule za kayumba, wanazurura vibaka na wengine wakike wapata ujauzito wakifika darasa la sita au saba wakati wanaishi na wazazi wao nyumbani......
Sidhani kama umemuelewa mtoa mada.
 
Ni kweli sana wazee wanahitajika kuwa karibu sana na watoto na hii itasaidia kumuelekeza kwa karibu sana yale yote ambayo angehitaji maelekezo au kujiona anafanya sawa kumbe sivyo ilivyo. Tupendelee kutimiza wajibu kuandaa vizazi vyenye maadili kwa kuhakikisha hatuwanyimi malezi wanayostahiki kupatiwa na wazazi.
 
Kweli boarding kwa mtoto hukengwa na fikra kuwa nipo huru na makatazo ya wazee huwa hayapati na ni wachache wanaoweza kujigomba wenyewe na mtoto mwenye umri huo sirahisi kukuta anajisimamia vizuri katika mambo yake
Nope huo ni uongo ndio anapata njia yakuepuka naanakuwa mjanja huko bwemi tumejionea mengi ni tuliepushiwa mengi tu.
 
Wazazi wote wanaopeleka watoto wadogo Bweni ni evil people na wanafaa kuondolewa vizazi, kwa maana wamelaaniwa, kama huwezi kumfundisha mtoto wako nidhamu iweje utegemee wengine wafanye hiyo kazi? fvck you!

Shule za Bweni ni kwa watoto yatima tu!

Well said
 
Boarding ilikuaga ni zamani wakati shule za day zilikuwa chache na zilikua sio nzuri kiaalum, kwa sasa mambo yameboreshwa vizuri kwenye elimu, siku hizi shule za day zipo nyingi tu na zinafanya vizuri.

Binafsi nilisoma day o level shule ya boarding nkipata division 3, nikaja kusoma day nikiwa Advance (form 5&6), nakumbuka mama yangu alikuwa anamlipa Mwalimu kila wiki elf 30, hii ikanifanya nipate dision 2 nikiwa day.
 
Back
Top Bottom