Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,842
- 31,073
Watanzania tumestushwa sana na taarifa iliyotolewa na msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Mutungi, siku 2 zilizopita, kuwa amewapa siku 14 chama cha ACT wazalendo wajieleze ni kwanini asikifute chama hicho kwenye usajili wa kudumu kutokana na ukaguzi wa hesabu za chama hicho za mwaka 2013/2014 na kitendo kinachodaiwa kutendwa na wafuasi wake za kuchomwa kadi za CUF
Sasa ndiyo tutaanza kuelewa ni kwanini wadau mbalimbali hapa nchini waliipinga vikali sheria mpya ya vyama vya siasa nchini, kuwa inaenda mpa mamlaka makubwa ya kuingilia mambo ya kisiasa ya vyama, jambo ambao litasababisha avifutie usajili vyama "serious" vya upinzani kwa sababu zisizokuwa za msingi
Hata hivyo wabunge wa CCM hawakuelewa kilio cha mamilioni ya watanzania na badala yake wakaipitisha sheria hiyo kutokana na uwingi wao wa wabunge tena kwa kishindo!
Hayo yameanza kujitokeza kwa msajili huyo kuonyesha nia ya kutaka "kukinyonga" chama hicho cha ACT wazalendo kwa sababu zisizokuwa na mashiko!
Kama kweli yeye msajili yupo "fair" kama mlezi wa vyama kama anavyoitwa, basi akifute chama cha CCM kwanza, kutokana na vitendo vyake vingi inavyofanya ambavyo haviendani na mfumo wa uendeshaji wa vyama vingi
Hivi kama sababu zake zingekuwa na mashiko, tunashangaa ni kwa vipi msajili hiyo wa vyama vya siasa, hajaonyesha nia ya kukifutia usajili wa kudumu chama cha CCM ambacho mara kadhaa kimekuwa mstari wa mbele katika uchomaji wa kadi za vyama vya upinzani kwa wanachama wao wapya wanaojiunga na CCM??
Hivi ni kwa vipi chama cha CCM kimeamua kupora bila ridhaa ya wananchi mali zisizohamishika, mathalani viwanja vya kuchezea mpira na kuviita vya CCM wakati wakijua kuwa viwanja hivyo vilijengwa na wananchi wote bila kujali itikadi zao za kisiasa??
Hivi mtanzania gani ambaye hajui kuwa chama cha Sisiyemu, ndicho kinachoongoza kwa kupewa hati chafu kila unapofanyika ukaguzi na ofisi ya CAG??
Hivi ni kwanini chama cha ACT wazalendo kianze kufanyiwa visa baada tu ya Maalim Seif kuhamia chama hicho baada ya kukitosa chama alichokiasisi yeye mwenyewe cha CUF, baada ya mzozo wa muda mrefu na Profesa Lipumba, ulioasisiwa na msajili wa vyama kumtambua yeye Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti halali wa CUF wakati kila mtanzania anajua kuwa Profesa Lipumba aliandika mwenyewe barua za kujiuzulu uenyekiti wa CUF??
Hivi dhambi ya Maalim Seif ni kufuatwa na maelfu kwa maelfu na wafuasi wake kwenye chama alichohamia cha CUF??
Hivi ni mtanzania gani ambaye hajui kuwa msajili wa vyama vya siasa nchini alikuwa "akimbeba" Profesa Lipumba katika mgogoro uliochukuwa muda mrefu wa CUF, ambao hatimaye Maalim Seif akaamua "kumbwagia" chama cha CUF huyo Profesa Lipumba ili akiongoze??
Hivi kuna kosa gani alilolifanya Maalim Seif kwa kumwachia, Profesa Lipumba, chama alichokiasisi yeye mwenyewe cha CUF ili akiongoze??
Katika Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, ibara ya 3(1) inatamka wazi kuwa nchi yetu itakuwa ya kidemokrasia na ya vyama vingi.
Sasa ni kwanini nchi yetu inayoendeshwa kwa mfumo wa vyama vingi zinatungwa sheria ambazo zinampa madaraka makubwa msajili wa vyama aweze kuamua hatma ya vyama vya siasa nchini??
Kama ambavyo Rais Magufuli alivyogusia suala la kutekwa kwa mfanyibiashara maarufu hapa nchini Mo hapo mwanzoni mwa mwezi huu kwa kusema kuwa watanzania siyo wajinga ambao hawajui namna sakata la Mo lilivyofanyiwa maigizo!
Vivyo hivyo nimwambie msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Mutungi, kuwa watanzania siyo wapumbavu na malofa wasielewe "mchezo mchafu" anaowachezea wapinzani "serious" wa nchi hii
Nimtahadharishe tu msajili wa vyama vya siasa kuwa ingawaje alivyotegemea kuwa kwa kufanya mbinu na michezo michafu za kuiua CUF basi angekuwa pia amemzika Maalim Seif kisiasa, haikuwa hivyo badala yake "amestukizwa" na Maalim Seif kuibuka upya, tena kwa ari mpya na kwa kasi mpya, akiwa na chama chake kipya cha ACT wazalendo, awe mpole na akubali kushindwa!
Kitendo chake cha kutaka kuifuta ACT wazalendo ni kitendo cha hatari kubwa kwa amani ya nchi hii na ambacho kitaweza kuleta machafuko makubwa hapa nchini na tusingependa yeye msajili wa vyama aiingie kwenye vitabu vya historia nchini kuwa ni yeye aliyeisababishia nchi hii iliyokuwa ikifahamika duniani kote kuwa ni kisiwa cha amani, yeye ndiye awe chanzo cha kuitokomeza amani hiyo hapa nchini!
Mungu ibariki Tanzania