Kwanini mpenzi wangu anabadilika badilika mara leo hivi kesho vile?

5525

JF-Expert Member
Apr 6, 2014
5,412
6,273
Jamani nashindwa kumfahamu mpenzi wangu, tulionana na kuzoeana ghafla tukawa wapenzi kiukweli tunapenda sana na sasa tumefikia kuzungumza kuhusu ndoa.Siku 1 akanimbia niende kwao kwa posa mana kuna mtu ameenda kwao na huenda wazee wake wakampokea akanitaka mimi niwahi kabla ya jamaa, Lakini mimi nilimwambia ajitahidi kumkataa na awafahamishe wazazi wake kwamba anaye ampendae siku ikifika atajitokeza tu.

Lakini pia nilimweleza kwamba mimi na wewe tokea tupendane ni muda mfupi hadimwezi mmoja vipi mimi nitakuja kwenu bila kujipanga na maisha? Na kukamilisha angalau mambo yangu lakini pia kuwe na angalau muda kidogo kujuwana vizuri. Nashukuru alinielewa na akakubali akaenda akapambana na wazee wake lile tatizo likaisha jamaa akatolewa nje.

Mara akaja akaniambia kwamba mimi ninampango wa kwenda chuo na sharti langu uniruhusu nisome mana kabla niliwahi kuwa na boyfriend lakini tulikosana alitaka anioe lakini niache kusoma niwe mama wa nyumbani tukaachana.

Jibu nililompa ni kwamba mimi binafsi ni msomi na mimi pia sipendi mwanamke ambaye si msomi na hafanyi kazi, hivyo mimi nabariki kabisa usome ata ufike uchina lakini kuwe na uaminifu tu na penzi letu akafurai sana akaniambia wewe ndo mume wangu utakayekuwa.

Lakini nikamueleza kwamba mimi wazazi wangu wanataka nioe mapema sana kutoka sasa labd baada ya miezi 6 nikamuuliza vipi baada ya miezi fulani hivi nikakuoa then ukaendelea na chuo wakati tushakua mume na mke? Akanijibu mbona hakuna neno ni sawa tu mimi nimekubali na hivyo ndo nnavyotaka mana ata shoga zang wanasoma wengine wapo kwenye ndoa na wana watoto pia.

Bahati nzuri mimi binafsi nimemfanyia application ya chuo nje ya nchi na kuna muelekeo mkubwa chuo atakuwa amepata soon labda jan anaweza kuanza kusoma, sasa jana tulikuwa tunaongea kwa simu mambo mengine tu baada kukata simu akanitumia sms inasema ''Usijali mpenzi wangu mimi na wewe tutakuwa mwili mmoja ifikapo 2017 nikimaliza chuo tu tutaona'' ambapo kutoka sasa itakuwa bado miaka 2 ambayo itakuwa ni muda mwingi sana.

Nimeshindwa ata kumjibu mana simuelewi, vipi anabadilika badilika na kutamburikiwa.Nimeleta hapa wakuu mnisaidie mawazo huyo dem nampenda sana lakini kwa miaka miwili kumsubiri kumaliza chuo kwakweli ni mda mwingi kwa mimi ingawa namruhusu asome popote kama tulivyokubaliana kabla. Kwa nini anabadilika badilika hivi?
 
Kaza kaka. Ukilemaa utapigiwa. Maisha ya chuo ni mabaya sana na hasa kwa wasichana.
 
Fanya umuweke chini muyazungumze aelewe hitaji lako. Waliwekwa chini akina Kingunge na Sumaye atakuwa yeye?
 
Hauko tayari kwa ndoa bro. Jipe muda kwanza ukomae. Huwezi kuwa mume ikiwa issue ndogo kama hizi zinakusumbua.
 
Alipotaka ukajitambulishe hukuwa tayari.....

Ulipoona inakufaa ndio ukawa tayari....

Nyie wote hampo serious. ..

Mkae mzungumze mjithathmini mwangalie uelekeo
 
Mmmh wewe ushampa matumaini ya kusoma nje, halafu umletee kauzibe na ndoa. Kwanini msingetafuta chuo cha hapa nchini. hofu huyo asijekutumilia tu akakutupa baadae.

Hiyo ya mchumba wa mwanzo imekaa kama changa la macho, mwanamke alikuwa anataka kuona msimamo wako. Siamini karne hii kuna mzazi anaelazimisha binti yake kuoelewa akiwa hataki.
 
Unajua kabla ya ndoa mtaahaidiana mengi ambayo kwa upeo wenu mdogo wa maswala ya ndoa mtayachukulia rahisi na yataenda tu. Muache asome amalize ndiyo mfunge ndoa. La sivyo anaweza asije soma tena. Akishaanza kuwa mama mwenye familia.
 
Nilipost uzi humu kuwa kazi ya kusomesha ni ya mzazi sio mume/mchumba wala boyfriend .usirudie hilo kosa achana nae huyo bora uwe na mwanamke darasa la saba kuliko msomi uliyemsomesha ,take my word
 
Ahahaaaaaa.
Unamsomeshea mtu hapo.
Hebu hiyo pesa kamsomeshee nduguyo au peleka kwenye vituo vya kulelea mayatima.
 
Back
Top Bottom