Kwanini mnatumia Tangawizi kwenye mboga?

mathsjery

JF-Expert Member
Sep 26, 2015
2,208
1,755
Mimi binafsi naona mapishi ya aina hiyo hayafai kwakuwa radha ya Tangawizi si nzuri kwa vyakula ila vinywaji mara mia nitumie kitunguu swaumu kwenye mapishi ya mboga.

Vipi wadau wa Chefs mnasemaje kuhusu hili?
 
Ukiwa una utaratibu wa kuweka tangawizi ama kitunguu saumu katika moja ya chakula chako kwa kila siku upungufu wa nguvu za kiume pamoja na magonjwa mengine utaskilizia kwa wengine. talk from experience!!
Kila siku asubuhi baada ya Mazoezi natafuna Tangawizi, Ni nzuri sana.
 
Nyama ya kuchoma tangawizi sawa ili ilainike.

Lakini nyama ya kupika iwe supu mchuzi roast sijui nini na nini sielewagi wanaweka tangawizi.

Kitunguu swaumu, limao au ndimu, chumvi, curry powder, masala ya nyama au mchuzi inatosha wakati mwingine nadondoshea soya sauce japo si mara nyingi.
Nyama inakuwa laini na tamu sana nzuri mnooooo yaaani.

Tangawizi huwa naweka kwenye chai, baadhi ya juice na kwenye detox water tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom