Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Huwa sijawahi kuelewa huu mfumo wa karibia kulazimishana kwamba ni lazima sijui ujenge kwenu, ili nini? Unakwenda kupoteza fedha na rasilimali kuwekeza sehemu ambako hauwezi kuja kuishi tena maisha yako yote? Kwa nini usijenge unapoishi wewe na Familia yako?
Acha wanaoishi huko wajenge, kama wewe ni tajiri na una uwezo wa kujenga nyumba zaidi ya 2 hapo labda inaweza kuwa sawa kujenga huko kijijini kama nyumba ya likizo, lakini kama uwezo wako ni nyumba 1 ambapo wengi wetu ni hivyo kama wewe siyo corrupt, ni ujinga kwenda kujenga hiyo nyumba kijijini, jenga unapoishi wewe na Familia yako.