Zamani wakati nasoma niliwaona waliofanikisha muungano watu wa maana sana kweli kweli. Hata hivyo, baada ya kuanza kufuatilia nikagundua kinachoitwa muungano si muungano bali ni kitu ambacho hakijapata jina lake. Na hii ilikuwa baada ya kugundua yafuatayo:-
1. Muungano gani unakuwa na ma - Rais wawili? Muungano wa kweli kabisa Rais ni mmoja tu kwasababu kinachoungana kinakuwa kimoja
2. Nilishangazwa kusikia eti kuna katiba mbili!? Hii ni maajabu!
3. Mbaya zaidi eti wao wanalo bunge lao na wabunge wao, halafu huku hamna bunge letu ila lililopo na wao wamo! Kama sio utahira ni nini?
4. Laikini pia, wao huku wamejaa kwenye kila ofisi, kwenye kila sekta lakini sisi kule hatupo? Kwanini?
5. Ukichaa mwingine, kumbe hadi syrabus zao ni tofauti na za kwetu.?Tuliungana nini?
6. Uhayawani mwingine, huku kwenye baraza la mawiziri wamo, wakuu wa mikoa wamo, ma-Das na ma- Ras wamo lakini wa huku hawavuki maji kwenda kuwa viongozi kule, kuna muungano kweli hapa?
Nadhani Mzee Warioba na timu yake walifanya kazi kubwa sana. Kama kweli sisi ni kitu kimoja, tuchukue yale maoni tuunde Taifa moja lenye Rais mmoja, katiba moja, baraza la mawaziri moja na jina libaki moja tu, Tanzania!!
Watakuja kuzaliwa watoto huko mbeleni watawatukana sana walioamua haya mambo na sisi tulioshindwa kuyasahihisha wakati yalishaonyesha dalili mbaya.
Wazee wetu walianzisha wazo la kuwa na muungano, ni kazi yetu kufanyia maboresho ya lazima ili kuleta maana ya kweli ya muungano. Kilichoungwa nusunusu ipo siku kitavunjika na huenda kikavunjikia pabaya kikaleta madhara