Kwanini mitambo ya dharura yote Dar? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwanini mitambo ya dharura yote Dar?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Muangila, Aug 21, 2011.

1. Muangila

Muangila JF-Expert Member

#1
Aug 21, 2011
Joined: Feb 24, 2010
Messages: 1,854
Likes Received: 196
Trophy Points: 160
Jamani kama tatizo la umeme lipo tanzania nzima inakuwaje mitambo ya umeme wa dharura yote inawekwa dar badala ya kuwekwa mikoani km mwanza arusha na mbeya? Je inawezekana kuna kaufisadi katika hili au ni sababu za kiutaalam.

Nawasilisha naona umeme unataka kukatika.

2. Alwatan

Alwatan JF-Expert Member

#2
Aug 21, 2011
Joined: May 19, 2009
Messages: 409
Likes Received: 1
Trophy Points: 33
Asilimia 80% ya makusanyo ya TRA yanatoka mkoa wa DAR, hii inaweza kuwa sababu moja. Naamini zipo nyingine...

3. E

Eddie JF-Expert Member

#3
Aug 21, 2011
Joined: Nov 28, 2008
Messages: 516
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Kwa sababu inaendeshwa na mafuta au gesi. Kwa kuwa bandari ipo Dar inapunguza gharama za usafirishaji. Gesi kwa kuwa bomba limefikia Dar

4. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#4
Aug 21, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

kwa nini isiwe mtwara ambapo gesi inazalishiwa na kuna bandari hapa ni ukilitimba ndo unatusumbua..

5. ndetichia

ndetichia JF-Expert Member

#5
Aug 21, 2011
Joined: Mar 18, 2011
Messages: 27,641
Likes Received: 236
Trophy Points: 160

yaani ukiwa unafikiria hilo ni sawa na yule anayefikiria kwa nini viwanda vya kusindika samaki viko mwanza na sio dar..

6. M

Mr.Right JF-Expert Member

#6
Aug 21, 2011
Joined: Jul 9, 2011
Messages: 408
Likes Received: 1
Trophy Points: 0
Unauliza nazi Kisiju?

7. K

KANAN Senior Member

#7
Aug 21, 2011
Joined: Aug 20, 2011
Messages: 124
Likes Received: 33
Trophy Points: 45
Dar ndo kila ki2 bwana wabunge wote wanahamia dar kwa nn wasipeleke mitambo huko.

8. Faru Kabula

Faru Kabula JF-Expert Member

#8
Aug 21, 2011
Joined: Mar 26, 2009
Messages: 10,642
Likes Received: 2,875
Trophy Points: 280
Mimi nitakujibu kitaalamu. Kwa kuwa mikoa mingi imeunganishwa ktk gridi ya taifa, basi popote pale penye member wa gridi ya taifa patanufaika regardless the location ambayo mitambo imefungwa. Kwa maana hiyo hata Mwanza kama ipo katika gridi ya taifa itanufaika tu na mitambo iliyofungwa Dar, kwani wote wa Dar na Mwanza wanachukua on the same bus system. Hapa nilitegemea malalamiko kutoka mikoa ambayo haipo ktk gridi ya taifa, haraka haraka niijuayo ni Ruvuma, Rukwa, Kigoma na mingine sijaifuatilia. Hata huu mgao huwa hauwahusu watu wa huko. Kwa mfano, wiki mbili zilizopita nilitoka Dar kwenda Sumbawanga, Dar niliacha mgao wa kufa mtu, lakini Sumbawanga nikakuta watu wanafaidi umeme na hata kukataliwa kwa bajeti ya Ngeleja hakuwahusu, kwani wao wanatumia umeme wa Zambia!

9. MwanaCBE

MwanaCBE JF-Expert Member

#9
Aug 21, 2011
Joined: Sep 23, 2009
Messages: 1,773
Likes Received: 544
Trophy Points: 280
Kwa sababu mipango ya wizi wa dharura hupangwa Dar.

10. Sikonge

Sikonge JF-Expert Member

#10
Aug 21, 2011
Joined: Jan 19, 2008
Messages: 11,503
Likes Received: 539
Trophy Points: 280
KWa Sababu Dar es Salaam ndipo yapo MASABURI ya Nchi ya Tanzania, hihihiiiiiii.................

11. E

Eddie JF-Expert Member

#11
Aug 21, 2011
Joined: Nov 28, 2008
Messages: 516
Likes Received: 1
Trophy Points: 0

1. Bandari ya Mtwara hakuna oil jet (sehemu ya kupakua mafuta )
2. Mtwara haiko connected na National Grid hivyo kufunga mitambo kule haiwezekani

12. Mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo JF-Expert Member

#12
Aug 21, 2011
Joined: Feb 3, 2011
Messages: 7,253
Likes Received: 244
Trophy Points: 160

Acha uongo...

13. F

FJM JF-Expert Member

#13
Aug 21, 2011
Joined: Apr 11, 2011
Messages: 8,088
Likes Received: 90
Trophy Points: 145
Kwa uelewa wangu hii inatokana na 'infrastrure ya umeme' ilivyowekwa. Cost wise ni cheaper kuwa na mitambo mingi Dar es Salaam ili kuweza kuingiza kwenye grid ya taifa kwa urahisi zaidi. Pia kumbuka unapokuwa na dharura inabidi ufanye maamuzi na utekelezaji katika hali ya dharura, hivyo si busara wakati wa dharura kuwekeza mitambo sehemu ambayo itachukuwa (a) muda kuunganisha kwenye grid ya taifa na (b) kuengeza gharama za kuunganisha kwa kuweka eneo jipya ambalo halina supporting infrastrucure.

Hata hivyo kwa mtazamo wangu nina hisi miaka kama 15-20 ijayo kuanzia sasa baadhi ya mitambo Dar es Salaam itaondolewa kabisa kwenye location za sasa, hasa baada ya upanuzi wa mabomba ya kupitisha gas ya songosongo. Kwa hali ilivyo Ubungo ni over crowded na hakuna expansion option ya uhakika kwa sababu wako katikati ya makazi ya watu. Inatakiwa ungozi wenye kufanya maamuzi magumu na kuanza mipango ya kuhamisha hii mitambo katikati ya makazi ya watu. Pia IPTL inatakiwa ifutwe (waondoe kabisa hii mitambo) ni very expensive na sio environmentally friendly. Lakini hii itategemea uwekezaji kwenye mitambo ya kutumia gas option ambayo ni a lot cheaper kwa sababu tayari tunayo gas.

PLANNING PLANNING PLANNING ndicho kitu kinatakiwa na sio hizi dharua!

Loading...