MC babuu
Member
- Jun 19, 2012
- 69
- 10
Serikali hii iliyokuwa madarakani ni wafuatiliaji wazuri wa ushuru kwa akina mamantilie,wasakatonge na wachumia tumbo tunaacha kuwabana akina (MGM) ni kwanini serikali isikopi kutoka zimbabwe baadhi ya sheria za madini.hivi karibuni serikali ya zimbabwe imetoa tangazo kwa wamiliki wa kampuni za madini zilizowekeza nchini humo kwamba inatakiwa hisa za kampuni hizo kumilikiwa na wazawa kwa 51% chini ya sheria ya wazawa.wakati mwingine nafikiria nashindwa kupata majibu nchi hii ipo na wasomi kweli au ni wanasiasa waliona uchu wa kuingia madarakani ili waweze kufanya biashara zao haramu imefika wakati tunapitwa sasa hadi na zimbabwe ambayo tumekuwa tukidharau na kumwita shujaa mugabe eti ni dikteta kama kiongozi anakuwa anaweza kuona mbali huyo ndo anastahili kuwa madarakani lakini kama anafikiria hapo alipokanyaga hafai kuongoza ata kijiji wala kata.Mugabe kwa hilo nampongeza kwanza huwavutii wawekezaji, sababu kufanya hivyo ni kujichimbia kaburi mwenyewe. Pili alichokifanya ni tendo la kishujaa yaani alichokifanya ni baada ya makampuni ya kigeni kukita mizizi kwenye madini na ndipo akahamua kuweka sheria inayoyataka kuuza hisa kwa wazawa zaidh ya nusu kwa maana hiyo umiliki wa kampuni nyingi utakuwa chini ya wazawa(wazimbabwe) na itachangia kukuza uchumi wa wananchi wa hali ya chini kutokana kwamba kazi nyingi zitafanywa na wazawa na kuongeza pato la mwananchi.kwa nini sisi pia tusiige mtindo huu tuwatege wawekezaji wakishaweka mizizi kama sasa tubadili sheria zetu ili kuwamilikisha wazawa kampuni za uchimbaji madini na mwisho tuziendeshe wenyewe.naomba kuwakilisha asanteni wadau wa jf.