Kwanini Membe asingesubiri 2025?

ngebe

JF-Expert Member
Jun 8, 2020
1,789
5,105
Siku zote mambo mazuri hayahitaji haraka. Ilikua ni uamuzi sahihi kama Bernard Membe angeamua kuvuta subira akasubiri 2025.

Ridhika na ulichonacho; haraka haraka haina baraka. Sikuona umuhimu wa wewe kuhama CCM ilihali unajua kabisa ukienda upinzani hauwezi kushinda iwe jua iwe mvua.

Hatimaye umejizika kisiasa; kuhusu urais sahau daima.
 
Unajifanya kujitoa ufahamu au? Hizi kelele za kubadilisha katiba watu waongezewe mihula huzisikii au? Hakuna guarantee kwamba angesubiri mpaka 2025 angepata hiyo nafasi
 
Umri umeenda,Binafs sioni sababu ya BM kuutaka urais kwa sababu kushinda hio nafasi ni ndoto. Angekaa tu kwake kama mstaafu wa serikali amalize uzee wake akiwa na amani
 
Kwa maneno yako yawezekana matokeo ya uchaguzi huwa hayaakisi maamuzi ya wapiga kura.
 
Yupo kazini Membe hv kusoma amjui mnashindwa hata picha kuona jamani km sio mwakani basi 2022 lazima lazima lazima atarudi nyumbani maana kazi itakuwa ameshamaliza...
 
Membe siyo mtu wa kuamini mwisho wa siku atakuwa kama Lowassa atarudi ccm na kuunga juhudi, ccm siyo watu wa kuamini wanna mbinu nyingi inawezekana katumwa
 
Membe siyo mtu wa kuamini mwisho wa siku atakuwa kama Lowassa atarudi ccm na kuunga juhudi, ccm siyo watu wa kuamini wanna mbinu nyingi inawezekana katumwa
Hili la kutumwa inawezekana kabisa, na wapinzani wataingia mkenge
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom