Kwanini mchaga akiambiwa anatokea Kishumundu anang'aka?

Kwanini mchaga akiambiwa anatokea Kishumundu anang'aka?

UngaUnga

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
1,724
Reaction score
1,471
KWANINI MCHAGA UKIMWAMBIA WW WA KISHIMUNDU ANAKUWA MKALI! ZAIDI YA MBOGO! KWANI PAKOJE HUKO KISHIMUNDU?! AU WATU WA HUKO NI MAZUZU SANA?! AU PENGINE MM SIJUI! MISS CHAGGA KUJA HAPA UTUDADAVULIE!.
 
Ukitaka ugombane na mchaga mwiite wa kishumundu balaa lake ni kama shehe aliyelishwa kitimoto alafu akaja akajua!
 
Sasa ukimtania mwanamme wa kichaga kwamba katoka Rombo, anaweza kulia kabisa
 
kwani kishmundu kuna nini?halafu nilipataga mrombo alitaka kuniowa nilikataa kama nilijua vile
 
KWANINI MCHAGA UKIMWAMBIA WW WA KISHIMUNDU ANAKUWA MKALI! ZAIDI YA MBOGO! KWANI PAKOJE HUKO KISHIMUNDU?! AU WATU WA HUKO NI MAZUZU SANA?! AU PENGINE MM SIJUI! MISS CHAGGA KUJA HAPA UTUDADAVULIE!.
jamii forum imepoteza sifa yake kuu kwa sababu ya uwepo wako na hoja zako dhaifu
 
Mtoa hoja naona unacheza style ya regge kwenye mziki wa sebene. Jamii forum watu kama nyie mkiendelea kuleta hoja legelege kama hizi hakika tutakuwa na forum ya kipumbavu sawa na bastola asiyokuwa na magazine.
 
Nijuavyo mimi ni utani tu wa eneo flani, zamani ilisemekana wachaga wa maeneo ya kishumundu walikuwa washamba hata wakifika mjini round about iitwayo ymca na wakaona picha ya askari walikuwa wakisalimia, ila hilo swala ni utani wa zamani na hauna ukweli wowote kwenye maisha ya sasa, kwani kishumundu ni eneo lililopo uru na ni kilomita chache kutoka moshi mjini na pana maendeleo kama zilivyo sehemu nyingine za mkoa wa kilimanjaro,
 
Mimi mkibosho kbsaa wa Mango parish, kishumundu,kwa kikobosho sio jina zuri linaamaana Malaya nakadhalika,sasa sio kwamba waliopo wachagga wakishumundu ni masikini ila jina lao,mfano wachagga kama mboro,kimathi,na Mboya nikoo zenye mahusiano ambapo babu zao walikuwa ndugu ndio maana mboro wengi wakienda mjini wanajiita kimathi au mboya,pia kuna Moria na Kiria wanahusiano wakindungu ndio maana wakiria wengi wakija mjini wanajiita Moria,kwanini Kiria nikoo iliyokuwa rasmi kwa kufua vifaaa vya chuma ikabaki nyuma sasa akipata pesa Kiria anajiita Moria,kama walivyo Mushi sisi,kuna Mushi Kimboka ,Mushi matamuo,Mushi tarimo,mangi sina alikuwa na watoto wawili wakiume Mushi matamuo na Mushi Kimboka,hao Mushi Tarimo walikuwa mateka ya kivita ndio waliokuwa wakipewa jina LA Tarimo sasa ikikutana na Mushi Kimboka au matamuo ukamuita Tarimo mnagombana,pia mkumbuke kuazia Leo Mushi sahihi ni yakibosho,ya machame wale ni puppets wa Mangi sina kama mnakumbuka palitokea ugomvi mkubwa enzi za Mangi sina mkibosho na wamachame,na ikapelekea wamachame kuuwawa wengi sana na wakibosho,na baada ya vita mangi sina akawa na vibaraka wake wakimachame aliowapa ukoo wa Mushi, pia mkumbuke wakibosho na wamachame wameaza kuoana miaka ya 1995 kuja juu,pia mangi sina alilelewa machame kwa wajomba zake mama yake alikuwa mmachame,wakamtesa sana sana,ndio chanzo cha ugomvi mkubwa,
 
Mtoa hoja naona unacheza style ya regge kwenye mziki wa sebene. Jamii forum watu kama nyie mkiendelea kuleta hoja legelege kama hizi hakika tutakuwa na forum ya kipumbavu sawa na bastola asiyokuwa na magazine.


NINA UHAKIKA! USIO NA CHEMBE YA MASHAKA! KUWA ELIMU!,ELIMU! ELIMU! NI TATIZO KWAKO HATA DARASA LA 7 SIDHANI KAMA ULIFIKA! NGOJA NIKAFICHE KIDOGO KA MASTERS KANGU KA OXFORD, NISIONEKANE KAMA WEWE!
 
Back
Top Bottom