Dah haya mambo bana..ndo tujiulize kwanini Tanzania hamna corona kenya ipoWataalamu wa afya na watafiti wa mambo haya tuambieni
Mbu jike aina ya Anofelesi ana uwezo kwa kuambukiza mtu ugonjwa wa malaria kwa njia ya kuuma mtu kupitia damu
Hoja iliyopo, iweje mbu huyo aweze kuambukiza vijidudu vya malaria halafu ashindwe kuambukiza mtu vvu
wenye uelewa fungukeni kuna ukweli gani hapa?
Sent from my VFD 301 using JamiiForums mobile app
kana vvu ni myth ina maana ukimwi haupo?Humu Jf zimeshawahi kushushwa nondo za maana kuhusu VVU na jamaa anayeitwa deception...
Unajua maana ya UKIMWI? Nenda ukasome ukimwi unasababishwa na nini then urudi hapa tena.kana vvu ni myth ina maana ukimwi haupo?
Ukimwi upo..yaani ukosefu wa kinga mwilini..ukiwa na stress hofu ya muda mwingi kukosa chakula Borakana vvu ni myth ina maana ukimwi haupo?
Kauli za namna hii sio tu zinaonyesha kutojali mamilioni ya waathirika wa VVU bali zinataka kuaminisha umma kuwa watoa huduma za Afya wote duniani ni wajinga na hawajui wanalofanya, huyo unae msifia nilimpa changamoto kuwa kama kweli anaamini anachokisema basi tuandae utaratibu awekewe damu ya mtu aliethibitika kuishi na VVU na hakuwa tayari.Humu Jf zimeshawahi kushushwa nondo za maana kuhusu VVU na jamaa anayeitwa deception.
VVU ni myth tu, ni kirusi kinachosadikika ila hakijawahi kuonekana popote pale.
Wewe unashangaa kwa Mbu tu? Huko saluni za kiume ndo balaa lakini bado tunadunda.
duh haya bhanaUnajua maana ya UKIMWI? Nenda ukasome ukimwi unasababishwa na nini then urudi hapa tena.
hii n new Id ya wangari mathai?Wasomi walioelimika ndo wanaweza kujibu swali lako, hapa TZ tuna wasomi waliokariri.
Tunayo maabara ya kuthibitisha kuwa dawa fulani ni kweli imeundwa na vitu kadhaa wa kadhaa na vitu hivyo ndivyo vinavyohusika kutibu ugonjwa fulani?
Wenyewe watakuambia kasome article fulani, rejea research fulani...nani kafanya hiyo kitu? Lengo lake ni nini? Yeye kasomeshwa, anakuja kunilazimisha mimi nimuamini kwakuwa ana ma stashahada ya hayo makitu. Raw materials zinatoka huku, mbona hatuundi hivyo vitu?
Kila kitu tunamsingizia Mungu au Shetani...umempiga mtoto sindano sio, kafa...mipango ya Mungu, tena kuna Israel mtoa roho, umaskini wetu, ...aliyekuoa wewe ndo alioninyima mimi..., aaaaargh
Je nje ya sindano watamengenywaje ? Sio mbu tuu vip vifaa kama saluni cutters.Haiwezekan kwa sababu mbu hana receptor kwa ajili ya replication ya Virus,hivyo Basi wakiingia ndani ya mbu humegengwa kama chakula kingine ,
Zipo sababu kadhaa :Wataalamu wa afya na watafiti wa mambo haya tuambieni
Mbu jike aina ya Anofelesi ana uwezo kwa kuambukiza mtu ugonjwa wa malaria kwa njia ya kuuma mtu kupitia damu...
Hapana mkuuhii n new Id ya wangari mathai?
Sindano ya mbu ina nje na ndani je upande wa nje ambao ulizama ukagusa damuZipo sababu kadhaa :
1. Vimelea vya malaria ( Plasmodium ) vinapitia mabadiliko ya kimaumbile ndani ya mwili wa mbu kabla ya kuwa tayari kumwambukiza mtu mwingine, hii huchukua siku kadhaa kitu ambacho haiwezekani kwa VVU.
2. VVU haviwezi kuishi ndani ya mwili wa mbu hii ni kwa sababu mbu anapomaliza kunyonya damu ni lazima asafishe ile mirija yake (proboscis), la sivyo itaziba na atashindwa kula na hatimae kufa
Ukweli ni kwamba mbu hawezi kutoa damu kwa mtu mmoja na kuipeleka kama ilivyo kwa mtu mwingine, kwa maumbile ya mbu yalivyo kuna mengi yanayotokea kati ya mlo mmoja hadi mwingine , hata vimelea vya malaria vikishakamilisha mabadiliko ya kimaumbile ndani ya mwili wa mbu huenda kwenye tezi za mate ya mbu na ndio wanaweza kuambukizwa kwa mtu mwingineSindano ya mbu ina nje na ndani je upande wa nje ambao ulizama ukagusa damu
Ni elimu pana kidogo ,Je nje ya sindano watamengenywaje ? Sio mbu tuu vip vifaa kama saluni cutters.
Kuna ukakasi sana kwenye hili mkuu