Kwanini Mbowe asiombe msamaha?

Kwanini Mbowe asiombe msamaha?

Modestproposal

Senior Member
Joined
Jan 6, 2022
Posts
127
Reaction score
230
Nakumbuka mwaka 2001 nikiwa kijana mdogo nilienda arusha kwa mjomba wangu kwa ajiri ya kutafuta maisha.kwa bahati mbaya sana na tena bila kutegemea nilishitakiwa na binamu zangu kwa mjoba eti nimesikika namsema vibaya kwamba eti HANITISHI KWA LOLOTE na akinichezea nitachukua pesa yangu na kurudi kwetu.ukizingatia kweli wakati nafika pale arusha nilikuwa nimebakiwa na tsh 25000 kwa wakati huo ilikuwa hela kubwa kidogo.

Mjomba aliamua kumuita kaka yake ambae ni mjomba wangu pia ili kunishitakia wakati huo mimi sijui lolote.ila wakati niko kwenye kibarua changu cha kuchimba mashimo ya kupanda migomba mana tulikuwa tunaishi ndani ya compus ya shule fulani,bibi kizaa mama,alikuja kunisihi kuwa ntakapoitwa kuhojiwa na wajomba zangu nikili na kuomba msamaha.maana alisikia wakisema nitarudishwa kijijini kwa mama yangu.

Kwa kweli nilifadhaika sana ukizingatia sikufanya kosa kama hilo.nilijisemea moyoni kamwe siwezi kukili kosa amabalo sikulifanya kama ni kijijini bora nirudi.hata hivyo nilikuwa nishatoka kijijini kitambo nilikuwa niko zangu jiji la mashishanga kwa miaka hiyo napiga umchinga.i encouraged myself that better i go back to my previous job.

Jioni baada ya sala mana wasabato kwa kusali ni kama dawa,kikao kianza na nikahojiwa kweliweli,kwakuwa nilikuwa nafahamu maamuzi yaliyofikiwa kupitaia kwa bibi sikuwa na hofu.nkajisemea moyoni yakuwa sitakili jambo ambalo sikulifanya.(kusema ukweli sikumsemea mjomba wngu vibaya)

Baada ya kikao hicho cha usiku maazimio yakawa nirudi kwa mama kijijini.na kwakuwa nilikuwa nimechoka na kazi ya umachinga sikutaka tena kurejea kwenye kazi hyo,nilimuomba mke wa mjomba pesa niyompa anitunzie na asubusi sana na bila kuaga nikaenda stand kupanda gari kuelekea dar.

Kwa wakati ule nauli kutoka arusha hadi dar ilikuwa tsh 7000.nilipanda gari majira ya sa nne hivi na nikafika dar kama saa12 jioni.kengo niende kwa baba zangu wadogo ambao walikwa wanaishi kurasini shimo la udogo.nakumbuka nilishauriwa na abilia mwengu nishukie kimara ili nipande gari za kwenda kariakoo,nilifanya hivyo.nilifika kariakoo kama sa mbili hivi za usiku na sijui pa kuelekea.

Nilimuomba dereva tax anipeleke kurasini lakini usiku ule nisingeweza kufika nilikupowa nakwenda na ukizingatia hakukua na simu enzi hizo.basi nikamwambia dereva tax anipeleke guest yoyote pale kurasini.akinipeleka mivinjeni hapo kilwa road nikalala.

Kufupisha story asubuhia niliwasaka baba wadogo hadi nikwapata lakini maisha yao yalikuwa ya kubangaiza.wakanifundisha kazi ya kuiba mafuta hapo bandarini na pale leli ya tazara...pale malawi cago,zamcago maeneo ya kurasini nikawa mwenyeji sana.

Hatimae yakanishinda nikarudi shuleni. Mpaka sasa nauona mwanga.

Kengo la kisa hiki ni kuonyesha ni kwa namna gani Mungu hamtupi mja wake.kwa kuwa nilisingiziwa Mungu aliniongoza hata kama nilipitia mapito ya hatari hakuniacha nife bali nitimize kusudi lililokuwa moyoni mwangu.
Kamwe mbowe usiombe msamaha.
 
Kesi za kisiasa zina maslahi kisiasa.
Hangaya katambua alikokosea anatafuta huruma za machifu!
Very soon DPP atatoa tamko lake...!
 
Nakumbuka mwaka 2001 nikiwa kijana mdogo nilienda arusha kwa mjomba wangu kwa ajiri ya kutafuta maisha.kwa bahati mbaya sana na tena bila kutegemea nilishitakiwa ...
Safi sana ! bila shaka pale mivinjeni ulilala SIKU GUEST HOUSE au ulilala kule relini ambako kulikuwa na KATA KIU GUEST HOUSE ?
 
Back
Top Bottom