Kwanini Mazishi ya wazungu watu hawajai makaburini ?

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Salaam JF,

Nimejaribu kufanya uchunguzi na kugundua kwamba kunautofauti katika shughuli za mazishi katika nchi za kiafrika hasa ziliso kusini na nchi zilizo ulaya na hata Amerika na baadhi ya mataifa mengine ya watu walio na asili ya rangi nyeupe.

Kwamba ukifatilia shughuli zao za mazishi kuanzia nyumbani hadi makaburini watu huwa si wengi kivile si watu maarufu tu! bali hata wasio maarufu. Kuna dogo alinitonya na kuniambia kwamba huku ulaya wazungu huwa wanaogopa kufa kishenzi inafika kipindi hata kuchungulia kaburi hawataki na wengine hutoa walicho nacho na kukaa mbali na misiba na wengine huwapa maiti mashirika ya mazishi ili kuzika.

o-FUNERAL-facebook.jpg
funeral.jpg
funeral.jpg
o-FUNERAL-facebook.jpg
 
Watu wengi wanaishia funeral home, huko makaburini wanaenda familia ya karibu tu.

Mazishi watu wanaona ni too personal halafu watu wanaona kwenda funeral home inatosha.

Halafu watu wengi wako practical. As long as kuna uhakika wa kuzikwa mtu atazikwa tu, akizikwa na wengi au wachache practically hakuna tofauti.

Watu wanahesabu masaa.

Afrika watu wanaona muda upo tu.
 
Watu wengi wanaishia funeral home, huko makaburini wanaenda familia ya karibu tu.

Mazishi watu wanaona ni too personal halafu watu wanaona kwenda funeral home inatosha.

Halafu watu wengi wako practical. As long as kuna uhakika wa kuzikwa mtu atazikwa tu, akizikwa na wengi au wachache practically hakuna tofauti.

Watu wanahesabu masaa.

Afrika watu wanaona muda upo tu.
kweli waafrika ni wastarabu.
 
Haaa hapo watu kibao siwasiliani nao... zamani was easier i can go through my phone book mwanzo hadi mwisho ila sasa siwezi kabisaa
Aisee sisi tunajaza majina kuanzia kwenye line inajaa unaingia kwenye phone inajaa na bado unahitaji kuongeza na mengine tu.Cha kushangaza unaweza kuta kuna majina mengine hata miaka mitatu inapita hujapiga wala kupigiwa.

Tofauti na wenzetu wazungu.Nilikuwa na rafiki yangu mu-Israel yaani simu yake ilikuwa na majina 12 tu tena ya familia yake.Hata no yangu hakui-save japokuwa tulikuwa tunafanya nae kazi.
 
Wastaarabu kwa sababu ya ukarimu na ushirikiano wa kiudugu pindi wanapopata taarifa ya msiba hushughulika mwanzo mwisho katika shughuli hii.
Kwa nini tabia hii iitwe usta-arabu badala ya usta-afrika kama ipo kwa waafrika?

Neno ustaarabu linanasibisha tabia na uarabu.
 
Back
Top Bottom