Kwanini matajiri wengi wana roho mbaya?

Kwanini matajiri wengi wana roho mbaya?

okoyoko

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2014
Posts
2,664
Reaction score
3,653
Hello guys

Nimepata chance ya kukaa na watu wa class tofauti tofauti, nime-observe kuwa watu wengi ambao ni matajiri ni wabinafsi pengine kuliko hata watu ambao ni maskini

Matajiri wengi wanapenda kujionesha mbele ya umma kuwa wao ni wema (kwa kutoa fedha) lakini moyoni sio watu kabisa, matajiri wengi husaidia huku rohoni wakiwa na ulterior motive eg; kuiba nyota za watu, kukwepa kodi, kujenga image etc. Baadhi yao kukutoa uhai ili kulinda reputation yao ni kitu rahisi mno.

Wengi wao wanaishi kwa hofu, na mashaka, kuugua presha ni kama maji kwao, matajiri wengi pia ni wateja wakubwa wa waganga na hutoa kafara za kutisha ili kulinda/ku-maintain biashara zao zisilogwe, coz sio matajiri wote wametajirika kwa kupitia njia ya uchawi

NB: kuna few exceptions, Sio matajiri wote wana roho mbaya kama nlivolezea hapo juu
 
Inategemea na mtu mwenyewe je amewekeza kwenye nn mpaka akawa hapo alipo. Ila kwa maono yangu ni kwamba kila mtu ana mahitaji na malengo yake linapokuja swala la kwann wenye pesa hawatoi au ni wagumu kusaidi
NI KWAMBA WAKATI WEWE UNAENDA KUOMBA MSAADA KWAKE na yeye unakuta ana magumu anapitia kimyakmya atakusaidiaje sasa?.. Utofauti ni kwamba wengi wenye mafanikio hua ni wastahimilifu sana...
 
Kuna mtu aliwahi kusema kuwa siri ya utajiri kuendelea ni ubahili. Sijui kama ni kweli?
 
Hiyo roho ndo imewafanya wafanikiwe
Bila hivyo wasingekuwa matajiri
 
Hello guys

Nimepata chance ya kukaa na watu wa class tofauti tofauti, nime-observe kuwa watu wengi ambao ni matajiri ni wabinafsi pengine kuliko hata watu ambao ni maskini

Matajiri wengi wanapenda kujionesha mbele ya umma kuwa wao ni wema (kwa kutoa fedha) lakini moyoni sio watu kabisa, matajiri wengi husaidia huku rohoni wakiwa na ulterior motive eg; kuiba nyota za watu, kukwepa kodi, kujenga image etc. Baadhi yao kukutoa uhai ili kulinda reputation yao ni kitu rahisi mno.

Wengi wao wanaishi kwa hofu, na mashaka, kuugua presha ni kama maji kwao, matajiri wengi pia ni wateja wakubwa wa waganga na hutoa kafara za kutisha ili kulinda/ku-maintain biashara zao zisilogwe, coz sio matajiri wote wametajirika kwa kupitia njia ya uchawi

NB: kuna few exceptions, Sio matajiri wote wana roho mbaya kama nlivolezea hapo juu
Matajiri wengi wana siri kubwa SN kwenye UTAFUTAJI WAO,,,unakuta ALISHADHALAULIWA,,ALINYANYASWA,,yote hayo yanampa MACHUNGU SN KWENYE KUSAIDIA WENGINE...ni wachache sana husahau MACHUNGU YA UTAFUTAJI
 
Mwanadamu hata umjali atakuumiza tu bora kuwa kauzu na kufanya yako
 
Ukipata hela utaona kawaida,halafu atatokea mwingine atakusema kwa yote hayo uliyoyasema kwenye uzi wako!
 
Kwasababu siri ya utajiri wao wanaijua wao.

Amin nakuambia Tajiri wa haki hawezi kua na roho mbaya isipokua anakua Mkali ,nahii nisababu Ukali husaidia kuendeleza mali.

Nb..ukali sio roho mbaya.
 
Si kweli,fanya tafiti yako upya. Matokeo ya roho mbaya tunayaona kwenye jamii zetu kila siku wizi,ubakaji,uporaji nk vitu vinavyofanywa na maskini wengi

Na matokeo ya roho nzuri tunayaona mahospitalini wanaotoa misaada mbalimbali,kwenye vituo vya watoto yatima nk vitu vinavyofanywa na matajiri wengi

Kwa haraka chukua orodha ya matajiri na maskini 10 popote pale unapoishi alafu anza kuchunguza matendo mema/mabaya yao,utapata jibu la kweli.
 
Inategemea na mtu mwenyewe je amewekeza kwenye nn mpaka akawa hapo alipo. Ila kwa maono yangu ni kwamba kila mtu ana mahitaji na malengo yake linapokuja swala la kwann wenye pesa hawatoi au ni wagumu kusaidi
NI KWAMBA WAKATI WEWE UNAENDA KUOMBA MSAADA KWAKE na yeye unakuta ana magumu anapitia kimyakmya atakusaidiaje sasa?.. Utofauti ni kwamba wengi wenye mafanikio hua ni wastahimilifu sana...
Hilo ndo jibu. Maskini wana tabia ya ulalamishi kama wa mleta mada. Mara zote wao hujiona ni wa kusaidiwa na siyo kusaidia. Ni nadra kusikia wenye pesa kulalamika kutosaidiwa pamoja na kwamba nao wana matatizo yao pia.

Hebu fikiria unayemdhania ni tajiri unaona physical assets alizonazo...wakati huo anaandamwa na mikopo ya benki. Maskini ni vigumu kulieelewa hili bali huona wamenyimwa na ndiyo maana wao ni rahisi kulalamikia matajiri. Wao hawajawahi kupitia hali kama hiyo.

Lingine tukumbuke matajiri wengi ni hard workers. Ni watu wako busy muda wote. Kinyume chake maskini wengi wameridhika na umaskini wao na wepesi kulaumu waliofanikiwa. Na hata wengine kutamani matijiri wafilisike ili wafanane.

Mwisho, maskini mara nyingi ndo wabinafsi kwa kupenda kupata vya bure bila kutoka jasho wakifkiri matajiri walifanikiwa wakiwa wamelala vitandani. Hakuna maskini anayeamuka saa 11...wengi hupenda kupumzika muda mwingi kuliko ule wanaofanya kazi.
 
Back
Top Bottom