Kwanini masikini ndio wachawi?

moexaud

Member
Jun 26, 2016
51
40
Ifahamike katika miji mingi hapa nchini na nchi za nje haswa katika maeneo waishio wananchi wasiojiweza ndio hutajwa kuwa na wachawi.

Kwa hapa Dar es Salaam utasikia mchawi kakamatwa Tandale au Mbagala sijawahi kusikia mchawi akamatwe Masaki au Upanga.Utasikia Sumbawanga au Tanga kuna wachawi.

Pia katika maeneo ya wenye kujiweza kiuchumi hapo hapo katiyao yule aliyechini kuliko wengine utasikia "mchawi huyo mcheki alivyo ndio maana hafanikiwi"

Huwa na jiuliza hakuna mchawi tajiri?
Na je utajiri hauendani na uchawi?

Au sifa za kuwa mchawi ni umasikini?
 
Mbona matajiri wengi ndo wachawi. Matajiri wengi waliopo dunia ya sasa ni wachawi wakupindukia kutwa huwaza kuwauwa wenzao, kisa mali!

Au wee uchawi unautafsr vip?
 
Nijuavyo Mimi matajiri wengi ni washirikina au ushirikina ndio uchawi?
 
wale mandondocha wa madukani kariakoo unafikri wanatoka tandale

huku kwetu uchawi wetu wa kuchanjana chale michanga juu ya bati kupakana matope asubuhi huu ndio maarufu

kuna mikoa hapa tz uchawi ni kitu cha kujivunia
 
Sema unachoshindwa kutofautisha ni aina za uchawi. Masikini wengi uchawi wao ni ule wa kuua watu na kula nyama, Huu uchawi nadhani Una laana ndio maana haqafanikiwi. Ila kuna uchawi wa kutafuta pesa au kuzuia wachawi wengine wasiibe, hawa wengi wanamafanikio, hata mzungu Huu uchawi anao .Aina hii ya uchawi inaambatana na jitihada za kufanya kazi kwa bidii na usomi.
 
Uki kumbuka lile tukio mtu kumulikwa na CCTV CAMERA ZA BUNGE utabadilisha mawazo.
 
kweli ukiwa msikini duniani ni taabu juu ya shida. ona sasa mwingine huyu anawatukana masikini eti ni wachawi!!!!
 
Masikini ana tabu sana, nafikiri hawezi kuingia mbinguni kwa sababu kila muda anawawazia wenzake mambo mabaya
 
wale mandondocha wa madukani kariakoo unafikri wanatoka tandale

huku kwetu uchawi wetu wa kuchanjana chale michanga juu ya bati kupakana matope asubuhi huu ndio maarufu

kuna mikoa hapa tz uchawi ni kitu cha kujivunia

Itakuwa Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom