Mwanaoshimba
Member
- Mar 8, 2017
- 61
- 82
Huwa nashindwa kuelewa ni kwa namna gani watoto hukichukulia kifo. Maana mara nyingi kwenye misiba, watu wazima ndio hulia sana. Lakini watoto hata kama wamefiwa na mzazi, kaka, dada au ndugu mwingine wa karibu sana, mara nyingi huwa hawalii.
Je ni kwa sababu huwa hawaelewi mantiki yake? Huwa hawaelewi nini kimetokea? Au huwa wana mawasiliano mengine ya kiroho ambayo sisi watu wazima huwa hatuyapati?
Ukisema pengine huwa hawaelewi nini kimetokea au huwa hawaelewi mantiki yake nako unapata mashaka. Hivi kwa mfano mtoto wa miaka 6, 7 au hata 11 asielewe kweli nini kimetokea na mantiki yake? !! Lakini pia mbona ukimsema, ukikasirika au akiona kitu kingine cha hatari anaweza kulia na hata kukimbia? Kwa nini kwenye kifo ndio wasijali na kulia?
Wenye ufahamu wa haya mambo sijui ya kisaikolojia au kiimani naomba tufahamishane.