Suala la Lissu kunyimwa chakula na Magereza limegusa na kuumiza wengi

Suala la Lissu kunyimwa chakula na Magereza limegusa na kuumiza wengi

Chakaza

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
41,009
Reaction score
74,643
Hivi hawa ni watu kweli? Au serikali hii inaongozwa na Mashetani ila hatujui?

Mtu unamfungia jela miezi 10 ili hali ukijua kuwa Hana kesi ila unamkomoa, halafu una mleta mahakamani anakopambana na timu kubwa ya Mawakili wa serikali na chakula unamnyima?

Hivi watu wakishangilia vifo vya watu hawa bado mtasema wachekaji wameishiwa utu?

Mie nasema sio kucheka na kukejeli tu bali hata kuombea dua WAFE ni haki yao.

Na Malaika mtoa Roho ikimpendeza leo akichikua hata wanne kwa mpigo tutamshukuru ili kutupunguzia watu wenye roho mbaya ulimwenguni.

Kuhusu mwenendo wa Kesi

Baada ya session ya jioni kuanza Lissu ambaye anashitakiwa kwa uhaini amesema, hajala kwa kuwa magereza ndio wenye wajibu wa kumleta chakula hawajaleta.

Lissu: Mhe. Jaji nipo tayari kuendelea ingawa sijala, Hawa Mawakili wa Serikali na nyie majaji nafikiri mmekula mchana huu.

Jaji Ndunguru: Sasa Mshitakiwa tuambie nani mwenye wajibu wa kukuletea Chakula ni akina nani? Ili tumwambie akuletee Chakula.

Mhe. Lissu: Ni Magereza hawa ndio wana wajibu na hela zangu kwa ajili ya chakula nimewapa wanazo.

Jaji Ndunguru: Sasa tu breki dakika 20 ili wakakupatie Chakula.

Mhe. Lissu amesema yuko tayari maana sheria inasema mahabusu anajinunulia chakula na hela zake wanazo wenyewe za Chakula. Na huu ndo utaratibu wa wafungwa wote kwenye nchi hii. Wakienda Mahakamani wanashinda njaa. "Mimi lazima niseme ili mambo haya yabadilike sio kwangu tu na kwa watu wote".
 
Kama wanaweza kufanya mauaji ili wakae madarakani, nini kula? Tusipofanya machafuko makubwa hakuna lolote watajali. Na wanafanya hivyo ili kumfanya Lisu awapigie magoti, hatimaye kumaliza upinzani. Tena wakisikia hivyo hajala ndio wanasikia raha maana wanajua unyama wao unafika kwa usahihi.
 
Saa 8 mchana, tarehe 12 February 2026

Imepigwa High Courtttttt

Majaji wameingia.

Mhe. Lissu alivyoingia anauliza mmekula? Mimi mwenzenu sijala kabisa.

Majaji wamewasha kipaza sauti pale na karani anasoma namba ya kesi.

Anasimama Renatus Mkude anajitambulisha na kusoma anaoambatana nao na kusema Mshitakiwa yupo.

Shauri lilipangwa na tunae shahidi P6 tuko tayari.

Mhe. Lissu anasema na mimi niko tayari. I ngawa sijala mnapofunga watu mjue hilo.

Renatus Mkude anasimama anasema kula ni haki yake ya msingi kama hajala tuahirishe maana kula ni haki yake. nashangaa kwanini hajala.

Mhe. Lissu anasema nimesema niko tayari maana sheria inasema mahabusu anajinunulia chakula na hela zangu wanazo wenyewe za Chakula.

Na huu ndo utaratibu wa wafungwa wote kwenye nchi hii.

Wakienda Mahakamani wanashinda njaaa. Mimi lazima niseme ili mambo haya yabadilike sio kwangu tu na kwa watu wote.

Hawa Mawakili wa Serikali na nyie majaji nafikiri mmekula mchana huu.

Huyu atakuwa ni shahidi wa tano yaani PW5 lakini jina lake ni shahidi P6 kwa Mujibu wa yale majina.

Hili jambo limewachanganya sana Majaji wanajadili kule juu sana.

Hii kitaalamu nimeambiwa inaitwa Equivocal plea yana unakubali jambo wakati umechanganya mambo humo ndani, hujakubali direct ndio maana imewavuruga.

Mh. Lissu anasema niko tayari kuendelea lakini mimi sijala.

Majaji wanaogopa.

Jaji Ndunguru: Sasa Mshitakiwa tuambie nani mwenye wajibu wa kukuletea Chakula ni akina nani? Ili tumwambie akuletee Chakula.

Mhe. Lissu: Ni Magereza hawa ndio wana wajibu na Dada yangu yupo hapa wanaweza shirikiana nae.

Jaji Ndunguru: Sasa tu breki dakika 20 ili wakakupatie Chakula.

Inapigwa Courttt kesi inaahirishwa.

Wananchi walioingia Mahakamani wanawaka kinouma. Wanasema hao Magereza na serikali wanamuonea Lissu kwanini hawampi Chakula. Wakinamama wanalia sana.

Yanapigwa sana maombi humu, Watu wamepandisha mori kesi imeahirishwa.
 
Hivi hawa ni watu kweli? Au serikali hii inaongozwa na Mashetani ila hatujui?
Mtu unamfungia jela miezi 10 ili hali ukijua kuwa Hana kesi ila unamkomoa, halafu una mleta mahakamani anakopambana na timu kubwa ya Mawakili wa serikali na chakula unamnyima?
Hivi watu wakishangilia vifo vya watu hawa bado mtasema wachekaji wameishiwa utu?
Mie nasema sio kucheka na kukejeli tu bali hata kuombea dua WAFE ni haki yao.
Na Malaika mtoa Roho ikimpendeza leo akichikua hata wanne kwa mpigo tutamshukuru ili kutupunguzia watu wenye roho mbaya ulimwenguni.
Unamjua mkuu wa ulimwengu huu ambae huweka watawala wa kitaifa kwenye nafasi zao? Ukimjua hutashangazwa na vitu kama hivi, na utaelewa kwa nini dunia hii imekuwa na watawala kama Hitler, Musolini, Trump, Idd Amin na hata hiyo mifano ya hapa kwetu
 
Nimekuelewa sana.. ndio maana viti vya mamlaka yao vinanuka damu zisizo na hatia
 
Back
Top Bottom