Kwanini Lowasa hasomagi taarifa za kamati yake bungeni?

Kwanini Lowasa hasomagi taarifa za kamati yake bungeni?

MtazamoWangu

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2009
Posts
313
Reaction score
7
Miaka yote nimekuwa natamani sana kumuona Mh. Lowasa akisimama bungeni kusoma taarifa ya kamati yake ya ulinzi na usalama na mambo ya nje kwani viongozi wengi haswa wenyeviti hutumia nafasi hii kutoa mapendekezo ambayo huwa ni mwiba kwa serikali na kuonyesha utendaji wa serikali katika idara hizo.

lakini miaka yote taarifa ya kamati yake inasomwa kwa niaba, je ni kweli mh. lowasa anatatizo la afya la yeye kusimama muda mrefu kama wanavyosema wapinzani wake?
je anaficha udhaifu wake? maana hata bungeni uchangiaji wake haupo kabisa, na kumbukumbu zangu ni kwamba kwenye bunge la 2010-2014 amesimama mara moja tu kuongea bungeni.

Hii ni tofauti sana na viongozi wengine kama Mzee Samweli Sitta ambaye ni mzee zaidi ya hata Mh. Lowasa, Mzee Sitta ameongoza bunge la katiba na bado ni waziri na utendaji wake unaonekana kwamba bado ana nguvu.

Hata Mzee Wasira, ambaye kiumri ni mdogo kuliko mzee Sitta, ila mzee wasira amekuwa ndio nguzo ya chama na serikali nje na ndani ya bunge, mzee huyu pamoja na mengine ameonyesha uwezo mkubwa sana katika kujenga hoja na kutetea kanuni na taratibu za nchi kwa kuonyesha uzalendo zaidi.

wanaomshabikia Mh. Lowasa mimi ningependa wanionyeshe mifano ya yale aliyofanya japo ndani ya 2010-2014 zaidi ya kufanya kampeni ya uraisi kwa kugawa pesa na kuwezesha wapambe wake, kwa kweli tusipokuwa makini tutashabikia jambo tusilokuwa na ujuvi nalo.

Hata Mzee Warioba ni bora zaidi kuliko Mh.Lowasa.
 
Kwani ana nguvu hata ya kushika karatasi? Ajaribu siku mona aone jinsi atakavyotetemeka hovyo. Na yale mate anayochuruzika nadhani karatasi zote zitalowa
 
1423042798537.jpg 1423042811983.jpg
Kuhusu mwenyewe anasema yupo fiti
 
ningependa kujua anasumbuliwa na ugonjwa gani hasa wakuu??? pia hivi na yeye alienda kwa babu 2011???
 
Ukiona chanukia ujue chalika. Hali kadhalika, kama chanuka hakiliki labda jibini ya Gruyere.
 
Simply jamaa uwezo hana ila money talks!!!
 
Pozi la picha! Huyu ni mgonjwa kama unavoona anafuatwa nyuma na gari humo kunakuwa na daktari na nurse kwa ajili dharura akidondoka ghafla! Binafsi nimemuona live barabara ya pale kwake Ngarash akielekea Monduli juu akifanya zoezi la kutembea akiwa na mlinzi na watu wa afya huku gari ikimfuata kwa karibu sana.

Cc ocampo four
 
Last edited by a moderator:
mi sioni rais ccm zaidi ya lowassa...mwigulu siku hizi kajivika ngozi ya kondoo lakini ni savimbi wa arusha na ni mratibu wa magaidi wa g.guard.

kuliko apewe membe ni bora j.k ale bata miaka mingine mitano coz ni type ile ile.

makamba ana ndoto kama alizokua nazo j.k kipindi kile akiitwa mtoto lakini too bad sidhani kama ccm itadumu mpk ifikie hatua afae urais.

tibaijuka kwishnei, migiro labda ugombea mwenza tz bado kumpa urais mwanamke.

kigwangala , ngeleja nchimbi maigizo hawana hata support.

sitta labda lakini litakua ni kosa la kuangusha utawala wa ccm sababu ya katiba yake...atawapa wananchi hasira.

pinda sawa lakini hakubaliki kama lowasa na ni mtu wa kulia lia tutegemee serikali na rais dhaifu.

sumaye he must be joking mda wake umepita na hana ushawishi.
 
Lowasa akisimama dakika tano anaweza kuzimia ni mgonjwa anatakiwa kumpuzika kwenda kuchunga ng'ombe huko monduli raisi wetu mtarajiwa tunamjua atatoka nje ya ccm
 
mi sioni rais ccm zaidi ya lowassa...mwigulu siku hizi kajivika ngozi ya kondoo lakini ni savimbi wa arusha na ni mratibu wa magaidi wa g.guard.

kuliko apewe membe ni bora j.k ale bata miaka mingine mitano coz ni type ile ile.

makamba ana ndoto kama alizokua nazo j.k kipindi kile akiitwa mtoto lakini too bad sidhani kama ccm itadumu mpk ifikie hatua afae urais.

tibaijuka kwishnei, migiro labda ugombea mwenza tz bado kumpa urais mwanamke.

kigwangala , ngeleja nchimbi maigizo hawana hata support.

sitta labda lakini litakua ni kosa la kuangusha utawala wa ccm sababu ya katiba yake...atawapa wananchi hasira.

pinda sawa lakini hakubaliki kama lowasa na ni mtu wa kulia lia tutegemee serikali na rais dhaifu.

sumaye he must be joking mda wake umepita na hana ushawishi.
Mnasumbuka bure raisi ajaye anatoka nje ya ccm
 
Back
Top Bottom