Kwanini Laptop hustuck au Kujizima yenyewe na kurestart yenyewe?

WatesiWETU

Senior Member
Jan 2, 2022
106
245
Mazee habarini

kama kichwa cha habari kinavyo sema hapo.

Laptop yangu nikiwasha inawak vizuri naingiza password fresh.. kisha nikitaka kuanza kufanya kazi tu ina jizima yenyewe alafu ndani ya sekunde 30 ina restart tena.. itafanya hivyo muda wote mpaka nachoka nzima na kuchomoa charge.

Alafu kuna saa nikiwasha.. ita ganda(Kustuck) tu mwanzon tu hata haika pata moto.

Je, hili tatizo ni nini? Nilipeleka kwa mafundi Machinga complex ila nimerudisha home leo no changes.. ipo vile vile.

Msaada wanatechnology nipeni wazi.

Laptop yangu ni yale Matoshiba ya zamani
 
"Toshiba ya zamani" hapo haujatoa taarifa yoyote itakayomsaidia fundi. Ulipoipeleka huko walikwambia tatizo ni nini na wamekarabati nini? Ni tatizo jipya au ndo ulivyoikuta?

Kagua matundu ya hewa, feni inazunguka? Puliza na mrija au nunua yale makopo ya upepo kutoa vumbi, iweke kwenye mazingira yenye AC au ipulizie feni ya mezani kwenye matundu ya hewa wakati inafanya kazi inapata angalau?

Kama unajua junsi ya kuingia BIOS fanya hivyo kisha kagua kama inaonyesha temperature pia kunaweza kukawa na utility za kukagua vitu kama RAM na HD, inategemea na PC. Jinsi ya kuingia BIOS inategemea na model tafuta youtube kama hii kipande cha BIOS Setup sio Boot Menu

View: https://youtu.be/pqaqAMro18k?feature=shared&t=61

Kama unaweza kuingia windows pia unaweza ukafanya RAM diagnostic humo. Kama kwenye hii video.

View: https://www.youtube.com/watch?v=kjeE2QbLgOM
 
Back
Top Bottom