Kama wanaingia katika ndoa ili kufurahisha jamii inayowazunguka hakika ni rahisi pia kwao kuachana kutokana na kukosa mtoto/watoto.
Ila kuingia katika ndoa kwa mtindo huo, sio bora kabisa. Mimi naamini ili muweze kudumu katika ndoa katika tabu na raha, lazima masuala ya upendo wa dhati na "kuoana" kati ya wanandoa yawepo. Hapo nimetumia neno "kuoana" kwa makusudi; ndoa haiwezekaniki bila ya wanandoa kuoana. Yaani lazima angalau wafanane na kushabiana kitabia fulani kwa kiwango cha juu; na hizi tabia ndizo msingi wa upendo wa dhati.