Wakuu habari
Hii kitu imenitokea juzi juzi nilikuwa na kimgahawa changu kidogo tu ila kilikuwa kinalisha watu wengi sana na ilhali mazingira hayakuwa rafiki kiafya na kifupi haikuwa sehemu yenye hadhi na kuvutia kabisa.
Nikajipanga nikapaboresha nikapajenga ili watu wakae ndani full feni na viti vizuri ila bei ikabaki ile ile.
Kilichotokea wateja karibia wote wamekimbia hawaji tena
Maandazi yanavunda kabatini ..chapati ndio usiseme zinakuwa kavuuuuu wadau nifanyeje au nilikosea kuboresha?
Sent using Jamii Forums mobile app
haya bwana.Tafuta vibinti vitatu vyenye mvuto au madem wenye chura uajiri kama wahudumu
Four Ps san change the dimenamic of the marketWakuu habari
Hii kitu imenitokea juzi juzi nilikuwa na kimgahawa changu kidogo tu ila kilikuwa kinalisha watu wengi sana na ilhali mazingira hayakuwa rafiki kiafya na kifupi haikuwa sehemu yenye hadhi na kuvutia kabisa.
Nikajipanga nikapaboresha nikapajenga ili watu wakae ndani full feni na viti vizuri ila bei ikabaki ile ile.
Kilichotokea wateja karibia wote wamekimbia hawaji tena
Maandazi yanavunda kabatini ..chapati ndio usiseme zinakuwa kavuuuuu wadau nifanyeje au nilikosea kuboresha?
Sent using Jamii Forums mobile app
Bei ile ile mkuuitakua wanaogopa mazingira yameboreshwa pengine na bei labda zimepanda af inaonesha ni uswazi sana huko waswahili wengi
Dah anyway mkuuYawezekana umasikini tumeuzoea, ila ni vyema ungewauliza wateja kwanza kabla haujaboresha wangekuambia wanahitaji nini? pili inawezekana hayo maandazi yaliyovunda kabatini ndio yanawakimbiza, tatu jenga tabia ya kutoa ofa ya chakula kwa walevi ili wakutukane kwa kukuambia mapungufu yako na uyafanyie kazi
Daah huenda mazingira uliyopo yanaogopesha, wanadhani ni sehemu ya watu high level, so wanajua hata bei imebadilika.
Weka menyu na bei nje mkuu.
Sent from my Nokia 6 using Jamii Forums mobile app
Hukutengeza Wateja, ulikuwa na wanunuzi ambao sio Wateja.
Biashara inakuzwa na Wateja na si wanunuzi.
Mteja ni MTU anayeacha Maduka/ migahawa yenye bidhaa kama zako na anakufuata wewe
Nzuri hiyoYawezekana umasikini tumeuzoea, ila ni vyema ungewauliza wateja kwanza kabla haujaboresha wangekuambia wanahitaji nini? pili inawezekana hayo maandazi yaliyovunda kabatini ndio yanawakimbiza, tatu jenga tabia ya kutoa ofa ya chakula kwa walevi ili wakutukane kwa kukuambia mapungufu yako na uyafanyie kazi