Kwanini kila niliempenda sidumu nae??

Kwanini kila niliempenda sidumu nae??

St Lunatics

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Posts
6,641
Reaction score
11,201
Wakuu leo nataka nijuwe hii ipo kwangu tu au hata kwa watu wengine.
Kuna ex-zangu 3 hawa ndio niliowahi kuwapenda kikweli kwenye maisha yangu na kuomba siku moja ndio awe mke wa maisha yangu.

1 Huyu wa kwanza ndie nilikuwa nampenda hatari sikuweza kumkosa hata kidogo. Tulianza kuwa wapenzi tokea shule wakati wote tupo pamoja, ilifikia rafiki zangu kuanza kumchukia huyu mdada kwasababu sikuwa nao kama ilivyokuwa zamani. Lakini mwisho niliondoka nchini na kwenda kusoma nchi nyengine hapa kuna rafiki yangu ndipo akafanya kutugombanisha na kuachana.

2 Wapili huyu aliweza kuzifuta hisia zote za yule wa mwanzo sikuwa hata namkumbuka tena yule wa mwanzo. Tulikuwa tukiongea masaa mengi tu kwenye simu, kwani yeye anakaa mkoa tofauti na mimi lakini ikitokea kukutana huwa tupo wenye furaha na kukumbatiana wakati wote. Nilimpenda sana huyu kwa kweli hadi kuna siku nilikuwa safarini nikiongea nae na simu ilikwisha charge na kuomba kutumia simu ya rafiki yangu. Nikiwa na dial namba ya huyu mwanamke wangu na kupress talk likaja jina lake kwenye cm ya huyu rafiki yangu. Nilishangaa sana na ndipo nikamuuliza kama anamjua huyu rafiki yangu? Kwakweli alikataa lakini nikamuuliza ilifikaje namba yako kwa huyu rafiki yangu? Hapo nilikata simu na kumuuliza huyu rafiki yangu ndipo akasema huyo mbona alikuwa mwanamke wake na aliachana nae baada ya kujua kama ana wanaume wengi tu anaongea nao. Nami ndio ulikuwa mwisho wangu nae

3 Hapa niwe mkweli nilimpenda zaidi ya wale wa mwanzo huyu alikuwa kama copy yangu, Yaani huyu kama moyo wangu ulikuwa ndio copy yake. Tuliendana sana mpaka rafiki zangu wote walimpenda hakuna hata mmoja alieonesha kumchukia. Kila wakati tulikuwa tupo pamoja ilifikia mpaka wazee wake wote wananijua na upande wangu pia wanamjua. Mama yake alifikia kuniuliza lini tutaowana na nilikuwa natamani niowane nae kwani huyu alikuwa ndio amani ya moyo wangu. Sikuweza kufikiria wale ex-zangu wala maumivu yaliopita hadi siku moja aliponiambia anataka kuongea namimi. Tukiwa tumekaa ufukweni mwa bahari upepo muruwa na akaanza kuongea kwa upole sana na nikiangalia usoni mwake jinsi alivyo pendeza lakini akiwa na huzuni ya mbali. Nikiwa namsikiliza alianza kwa kusema hakika mimi ndio tulizo la moyo wake na angependelea mimi niwe ndio mume wake wa maishani. Hajawahi kuijua furaha maishani mwake mpaka alipokutana na mimi ndio niliemfanya kujua furaha ya mapenzi. Lakini alikuwa na mpenzi kabla yangu mimi na alikuwa akimpenda sana zaidi yangu. Huyu mpenzi wake alikwenda ulaya kusoma na amerudi na anataka amtolee posa, kwahio hajui amchaguwe yupi kati yetu. Niliposikia maneno yale moyo ulipiga kwa nguvu sana lakini nilijikaza kiume na kumuuliza kwahio bado unampenda huyo jamaa?. Akasema ndio lakini nakupenda na wewe pia ndio nipo njia panda sijui nimchaguwe yupi kati yenu. Sikuwa nataka tena kuendelea kuongea nae nilimwambia twende zetu tutaongea kesho. Nilimrudisha kwao na usiku ule nilimblock kila kona ya mawasiliano yetu mpaka hii leo sijui lolote lake.

Ex-zangu hao watatu waliweza kuniachia na majaraha matatu Pombe,Uzinifu na Kutoamini upendo wa kweli. Lakini nimebaki kujiuliza jee hawa ninaotembea nao sasa Majeraha gani ninawaachia?
 
Mi pia
Niliedumu nae ni miez8, na mara nyingi nawaacha mwenyewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Ni kuwa unaempenda ndo unaehofia zaidi, na mtu ukimuhofia hutoish kwa raha, au ukimuhofia utahishi nae kwa furaha saana

Lkn awa wa kupotezea mda ad wanakulilia

Na kingine mara nyingi utaempenda ni kuwa katulia kiakili na ni mzr sana
Watu wa hvyo wanataftwa sana
 
Kutembea nao sio tatizo, tatizo mnaelekea wapi? Msije tu mkakutana na watu wasiojulikana.
 
Ukitaka kudum nae mchukulie kawaida na ishi nae kama mtu mwingine2 na wala usijiumize moyo kwake

Tatizo ni kat ya 15 unaodate nao ni moja2 utampenda
Hio kweli kuwachukulia kawaida lakini kuficha hisia mimi huwa siwezi kabisa mkuu
 
Wanaume wa sahv tumegoma kuoa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Na mimi nasema itokee tu!
Maan sio kwa mlolongo wa ma-ex
 
Pole sana mkuu
Huwa inatokea sana mtu kutoamini tena kama kuna mtu ataweza kuziba pengo lililoachwa lkn jaribu
Naamini kila kitu kinawezekana just take it easy usiwazie saaaaana future katik mahusiano machanga
Ukichukulia kawaida tu Mwisho wa siku utashtukia muda unaenda na ukishamzoea mtu inakuwa ngumu sana kumuacha na hapo ndipo upendo unapoongezeka

I hope utapenda tu Ila jaribu kuwaweka pending(watoe kabisa kichwani )toa hisia nao kabisaaaa hapo unaweza kupenda am sure
 
Hakuna cha ajabu hapo ,uumize uumizwe ndo maisha yenyewe.Hakuna kitamu bila kichungu
 
Usiharibu maisha yako ukabadili tabia yako ya dhati kwa sababu ya tabia za mtu mwingine.
Kumbuka madhara yote yapo kwenye maisha yako!! Jiulize kwanini ujile adhabu ya kulewa bila mpango, uzinzi maishani?
 
Mbaya sana kukutana na mwenza ambae yupo kwenye majaribio ya kupenda,had aje atulie sio leo,so we cha msing tafta mwanamke ambae yuko ready to settle down,ukitafta ambaye ndo dam inachemka,asee utabak unalia deile,ndomana kwasie wazoef wa hiz kaz tunamadem zaid ya m1,pia kat ya hao wapo ma singo maza yaan hawa hawanaga shida zaid ya vizinga,plus madem wengne ni wadada wale waliomaliza chuo wale washakaa sana wanasubiria mume sis ndo tunawalubun,ila ukitafta cha form six au chuo mwaka wa kwanza,utapotea
 
hizo ndio changamoto zenyewe za mapenzi kama huwa unazisikia, unataka urahisi ili uje usimulie nini? chamsingi songa mbele, ila badili mfumo wako wa kupenda na unavo wa handle wapenzi wako pengine ww ndo tatzo mkuu.
 
Back
Top Bottom