GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,656
- 109,056
Mimi huko nyuma nilikuwa nikidhani kwamba Watu wengi wanasoma sana na kuwa na ngazi mbalimbali za ' Kitaaluma ' labda ili wakiwepo katika Makampuni au Taasisi mbalimbali basi Watu wengine waweze kuona utofauti mkubwa wa Elimu zao hizo ila Utafiti wangu mdogo tu ( ambao siyo rasmi ) nimegundua kuwa kwa hapa Tanzania hali ni tofauti.
Je kama kwa hapa Tanzania ni vigumu Mtu kugundua Watu wenye Degrees, Masters na PhD's huko katika Makampuni / Mashirika mbalimbali sasa ni kwanini bado Watu wengi wanaenda Vyuo Vikuu Kusoma? Je Elimu yetu Tanzania ndiyo Tatizo au labda ' akili ' za Watanzania wengi ndiyo tatizo? au labda hao Wahadhiri wengi wa huko Vyuoni nao ni Changamoto / Tatizo?
Hali hii huwezi Kuikuta nchi jirani kama Kenya, Uganda na Rwanda achilia mbali zingine kama Afrika Kusini, Ghana na Zimbabwe.
Nawasilisha.