kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 16,252
- 16,170
Mafanikio haya tunayoyaona Sasa nchini hayatokani na ujanja Wala akili za Karia, bali jitihada za wafanyabiashara walioamua kwenye mpira wetu na Rais wa nchi kupenda michezo.
TFF ya Karia ameonyesha udhaifu mkubwa katika kusimamia kanuni za mpira kwenye usajili wa wachezaji, uhamaji wa wachezaji kutoka timu Moja kwenda nyingine, kupanga ratiba zisizo na malalamiko na viporo vingi, kutoa zawadi za washindi, ubora wa waamuzi, na kuahirisha mechi kiholela.
Kazi zake nyingine ilibidi zifanywe na watu wengine wakiwemo mawaziri na Rais wa nchi ili kurekebisha mambo mpira uchezwe.
Karia ameshindwa kabisa kushirikiana na wadau muhimu wa mpira kama timu anazoziongoza na wadau wengine. Alitumia authoritarian/dictatorship (yaani Fanya ninachokuambia) kama njia yake ya kuongoza taasisi, hakuruhisu mijadala na maoni kutoka kwa wadau.
Kama sio busara za wawekezaji, viongozi wa timu, mashabiki, wachambuzi, serikali na Rais wa nchi mwenye huenda maafa makubwa na uharibifu wa mali ungetokea mkubwa sana. Mfano, unaona timu pamoja na uwekezaji wake mkubwa unaona inashika daraja kwasababu za waamuzi, ratiba mbaya na adhabu zisizokuwa na kichwa Wala miguu.
Kwanini asijitafakari kutuachia mpira wetu?