Kwanini kama taifa hatuendelei?

mkuu tuzangumzia maendeleo ya jamii kwa ujumla,sio kila mwanajamii ataweza kutumia fursa hyo kupata kipato maana hizo biashara ulizotaja haziwezi fanywa na kila mtu
 
"it is dangerous to be right when the goverment is wrong"
-VOLTAIRE-

sent from my SM-galaxy s8+ using jamiiforums mobile app
 
Reactions: 30P
unsustainable economic growth
 
Ndo swali gani hili sasa,
Haujakamilisha uchunguzi halafu unatuuliza swali,
Weka ccm kando wape miaka mitano wapinzani waongoze,halafu Pima maendeleo,ukiona hatuendelei ndo uje uulize kwa nini hatuendelei,
Fikiri unawapa nchi watu ambao Leo wanasema pesa si ya umma wanaigawana,kesho wanarudi kusema ni ya uma na wanarudisha pesa hiyo serikalini,halafu hata siku haijaisha wanarudi tena kuzichukua [emoji23]

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kaka trust me,somalia wakipata utulivu kwa miaka mitano tu watatuzidi mbaaaaaali,

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Utasubiri Sana Kama unataka chama kikusaidie bilionea bakhresa na Reginald mengi hajawezeshwa Na chama Chochote endelea kusubiri chama utakufa lofa
Hapa nlipo wee na kuwa chichiem ila kwa ulofa umenizidi

Ova
 
Pointless

Ova
 
La maana ni kujiuliza kwa nini Chadema hawajengi makao makuu yenye hadhi, hadi leo wako pale pale Mtaa wa Ufipa.
 
Adui nambari moja wa maendeleo ya Tanzania na Watanzania ni wahuni, wezi, majangili, watoa na wapokea rushwa wa MACCM.

 
Heading huwa ni sentesi inayoakisi maana nzima ya andiko. Maana yake kwa jinsi nilivyoelewa, kuna sehemu Fulani katika miaka hamsini ya uhuru tulitakiwa tuwe tumefika, ndiyo maana ukanijibu hivi,
Ndio maana nikakuuliza, wewe unatumia vigezo gani? Tumia takwimu na linganisha kati ya mataifa yaliyopata uhuru, mwaka 1961 na kuwa na population kama ya Tanzania. Pia kuwa na gdp kama ya Tanzania mwaka 1961 na sasa yamepiga hatua kubwa kuliko Tanzania.
Halafu ndiyo uulize sisi tumekosea wapi?
 
Kwanza Kobello nashukuru kwa mchango wako. Kipimo cha kwanza ni lazima tunapotaka kama taifa kujipima kama kasi ya maendeleo yetu inalingana na hapa tulipo, kwa mtizamo wangu si tu kuangalia nchi ambazo zilipata nasi Uhuru mwaka 1961 kwa sasa ziko wapi kimaendeleo kiuchumi na kijamii.

Kwa mtizamo wangu malengo ndiyo kipimo cha kwanza kuangalia kama tumefanikiwa ama la. Wewe unafahamu kwamba kupanga malengo ya maendeleo kuna vigezo vyake vya kisayansi hutumika. Huko nyuma na hata sasa huwa tunapanga mipango yetu ya maendeleo kwa miaka mitano mitano, na sasa tumeongeza na kitu kingine kinaitwa dira ya maendeleo.

Sangarara alinitahadharisha kwamba neno maendeleo ni kitu "Vague" na mimi nikamkubalia. Lakini kama taifa tunaweza kusema kwamba kwenye hili tumefanikiwa lakini katika hili hatujafanikiwa. Kuna mambo ya takwimu ambayo ni muhimu kwenye kupima maendeleo, lakini na takwimu nazo huweza kuchakachuliwa (Data manipulation) kunapokosekana uwazi.

Ukiachana na takwimu za kiujumula zinazotolewa na Benki Kuu na Idara ya Takwimu (National Bureau of statistics) takwimu zetu nyingi ni za kupika ana zinarudufiwa zile zile kwa lengo maalum. Kwa mantiki hiyo tunabakiwa na kigezo kimoja ambacho ni kuangalia kama tunapopanga mipango yetu tunafanikiwa ama la!
 
hizo ni fikra zilizojaa tope au mavi hivi Tanzania kuna kitu ambacho hawana ngoja nikutajiye kidogo : mito ya maji Zaidi ya 30 waziwa ya maji Zaidi ya 40 almasi, dhahabu, Shaba, chuma, tanzanite, uranium, makaa ya mawe, misitu, wanyama pori, gas, oil, ardhi ya kilimo, bahari,na kadhilika na kadhalika yaani Bongo inaweza kuilisha dunia yote lakini wapi wabongo wana akili kama zako.jini na nuksi ya nchii hii ni CCM full stop. Afya= 0 Elimu = 0 miundombinu = 0 kilimo = 0 maji = 0 umeme= 0 barabara= 0 ustawi wa jamii = 0 kila kitu ni =0 that is CCM miaka 56 ya utawala wake kila kitu ni = 0
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…