Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
- Thread starter
-
- #81
Rutashubanyuma hatuwezi kuingia kwenye kinyang'anyiro bila kujiandaa toka tupate uhuru mwaka 1961 Tanzania tumepoteza muda mwingi tukisaidi nchi zingine kupigania uhuru na kuzikomboa toka kwa watawala wabovu nchi kama Angola, Msumbiji, Zimbabwe, shelisheli, Uganda na Afrika ya Kusini wakati wenzetu wakenya toka uhuru wanashughulika na biashara wanajua umuhimu wa ardhi na wanaelimu ya masoko ya hisa toka mwaka 63 wakati watanzania tumeanza juzi maana muda mwingi pia tulikuwa kwenye siasa ya ujamaa na kujitegemea
Kawhiyo haitakuwa haki kutuunganisha na watu wenye uzoefu undercover ya kuwa nasi tutapata bidii hakuna kitu kama hicho inabidi watanzania wapate muda wa kujiandaa ili kuingia kwenye shirikisho kitendo cha kulazimisha Tanzania kuingia sasa hivi ni sawasawa na mwanafunzi wa darasa la nne umpeleke kufanya mtihani wa darasa la saba eti atajifunza mbele kwa mbele bila kuandaliwa ili afikie kiwango cha mwanafunzi wa darasa la saba au ni sawaswa na kupeleka timu ya Olyimpic kwenye mashindano kabla haijafikia kiwango eti itajiongeza mbele kwa mbele itaishia kuwa msindikizaji
Wenzetu nchi za ulaya zina jiandaa kwanza kabla ya kuingia European Union haziendi kichwa kichwa halafu katika EU kuna nchi viongozi zimeset standard ili mwanachama aweze kuingia ili wanachama wawe ni member wanaofanana. sasa sisi tutaunganaje na madikteta kama Museveni? Kibaki au Kagame lazima wawe na mifumo yenye kuheshimu katiba bila kubalidi term limit kwa mtu kama Museveni na Kenya waondoe dhana ya kuwa bila wakikuyu nchi haitawaliki pia Kagame kujifanya nabii wa Rwanda kuwa bila yeye hakuna Rwanda
Mkuu, Rejea mfano huu:
Hivi kuna kiongozi yeyote wa Marekani, India au China asiyejua maana ya kutunza mazingira au madhara ya kutotunza mazingira katika ustawi wa viumbe duniani? Jibu ni hakuna. Wote wanajua, lakini unafikiri ni kwa nini viongozi wa nchi hizo hawataki kutekeleze kwa 100% Kyoto protocal (Rejea mkutano Wa South Africa,2011)?
Ukichunguza vizuri mfano huu utagudua kuwa Wawakilishi wetu(Sitta nawenzake huko EAC) walikuwa sahihi kwa uamuzi walio chukua.
Wewe ndio una bad reasoning, mbona wapo pia wawekezaji wakubwa Kutokea Kenya ambao wanamilikishwa ardhi kwenye baadhi ya strategic investments... Na hao wazungu uliowataja bado hawajachukua hata 1% ya ardhi yetu yote...Ambacho hatutaki ni kufungulia mlango kwa VIBAKA karibia milioni 70 (i.e., akina Njuguna, Nyangau na batabaire) kuja kugombea ardhi kiholela na watanzania wazawa kila sehemu....NO WAY
Mfano wako wa Zanzibar ni mfu kwa maana kule ardhi yenyewe haipo na ile iliyopo ni ya kugombea hata kwa wazawa wa huko, zipo sehemu za Tanzania bara ambazo zina ugumu wa kupata ardhi hata kwa wenyeji, kwa mfano mkoa wa Kilimanjaro...
Mfano wako wa wakoloni ni mfu pia...:lol: Hata Uingereza, Ujerumani, na Ufaransa (wakoloni wakuu) kuna baadhi ya mambo likiwemo la ARDHI hawakubalini nalo kabisa kwenye Jumuiya ya Ulaya (EU)...
Sikubaliani na Vasco kwa mengi ila kwa hili la ARDHI niko naye 100% siasa za kufuata sera zavyama naweka naweka kando utaifa mbele...😛oa
uchumi wa TZ umo mikononi mwa wasauzi na wakenya..........................amka kutoka kwenye usingizi.........................fuatilia takwimu za uwekezaji hapa nchini na utaelewa kinachoendelea......................................wewe subiri wakuajiri wewe na watoto wako.........................
Wewe ndio una bad reasoning, mbona wapo pia wawekezaji wakubwa Kutokea Kenya ambao wanamilikishwa ardhi kwenye baadhi ya strategic investments... Na hao wazungu uliowataja bado hawajachukua hata 1% ya ardhi yetu yote...Ambacho hatutaki ni kufungulia mlango kwa VIBAKA karibia milioni 70 (i.e., akina Njuguna, Nyangau na batabaire) kuja kugombea ardhi kiholela na watanzania wazawa kila sehemu....NO WAY
Mfano wako wa Zanzibar ni mfu kwa maana kule ardhi yenyewe haipo na ile iliyopo ni ya kugombea hata kwa wazawa wa huko, zipo sehemu za Tanzania bara ambazo zina ugumu wa kupata ardhi hata kwa wenyeji, kwa mfano mkoa wa Kilimanjaro...
Mfano wako wa wakoloni ni mfu pia...:lol: Hata Uingereza, Ujerumani, na Ufaransa (wakoloni wakuu) kuna baadhi ya mambo likiwemo la ARDHI hawakubalini nalo kabisa kwenye Jumuiya ya Ulaya (EU)...
Sikubaliani na Vasco kwa mengi ila kwa hili la ARDHI niko naye 100% siasa za kufuata sera zavyama naweka naweka kando utaifa mbele...😛oa
kama hatuamini juu ya malengo ya EAC si tujitoe tu kulikoni kuwakwamisha wale wanaotaka kwenda mwendo mdundo.......
ardhi ni ya mwenye pesa na ndiyo maana wakenya wanaendelea kuinunua hapa nchini....................kwa hiyo shirikisho kuwepo au kutokuwepo ardhi inakwenda tu kwa mwenye nacho..........................wewe tetea ardhi lakini ardhi haikusubiri wewe.................leo tunavyoongea nakumatt ya Kenya inafungua super market ya nguvu Moshi..........................ardhi kwani hawakupewa?
Sijui ni ardhi gani ambayo waiongelea ambayo inawazuia wakenya wasiipate.........................kila kitu kina thamani yake kwenye soko....................tutoke kwenye hizi ghiliba za wanansiasa za suala la ardhi kuwa halina uhusiano na shirikisho halafu tuangalie ni jinsi ipi shirikisho la EAC litasaidia kutokomeza umasikini hapa nchini........................huhitaji kumiliki ardhi kuondoakana na umasikini................soko la ajira tukiweza kulipanua na hili haliwezekani kufanikiwa ndani ya TZ pekee...........we have to look beyond the tiny box called TZ...............
Du! huyu jamaa anahitaji kupepewa ili akili zake za udadisi wa kimantiki zimrejee japo kwa dakika chache wakati anadadavua mada hii....Aliyekuambia uhuru ni kufuta mipaka ni kilaza. Ardhi ndiyo msingi wa uhai wetu na kinachohitajika ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anamilikishwa sehemu ya ardhi ili aitumie kwa ajili ya mustakabali wake ili kuondokana na dhana ya rais kuwa mmiliki wa ardhi yote kwa niaba yetu. Kwa hiyo usitegemee kupendwa km unawatilia ngumu raia wa nchi nyingine uhuru na fursa za kumiliki ardhi yetu kwa kisingizio cha shirikisho la afrika mashariki, wakati tukijua kuwa katika nchi hizo nyingine hakuna kipande cha ardhi kilicho wazi km ilivyo Tanzania.tatizo kwako huelewi ya kuwa uhuru maana yake ni kufuta urithi wa mkoloni ikiwemo mipaka aliyotuwekea.....................mkoloni alitugawa ili atutawale...............................hivi yawaje akija kaburu kutoka sauzi anapewa ardhi ambayo wewe unadai ni lulu...............................ululu huo uko wapi wakati umasikini wazidi kushamiri.....................sana sana watetea ubinafswi ambao hautupeleki popote.....................yawaje inap[okuja EAC tujione ni lulu lakini kwa wazenji tujione hatuna maana hata kuona aibu kujiita jina stahili la watanganyika?????????????
Hakuna wa kuniajiri mie ninaishi Marekani nina guarantee ya maisha yangu na wanangu pia nina miradi yangu ya kulima mashamba mkoani Rukwa na Morogoro labda wakuajiri wewe, ile wanangu kuzaliwa hapa na kuwa na social security numbe wnaweza kufanikiwa katika maisha sihitaji kuwaibia watanzania ili wafanikiwe kazi ni kwao sky is the limit
Ubaya wa kikwete ni kwamba sio mnafiki na anapenda kusema ukweli.kama nchi za jirani hawajahudhuria sherehe za miaka 50 za uhuru wa Tanganyika eti kwa kuwa wamenyimwa ardhi niko upande wa Jk.wewe endelea kulalamika na kunung'unika kwa ukale wa mawazo kuwabembeleza na kuwafurahisha kina Mwai na museveni....Mwache Kikwete atutetee sisi wanyonge.wew ungewahi kuzaliwa let say wakati wa ukoloni bila shaka ungekuwa MNYAPARA ie mkoloni mweusi.
Acha hoja za kitoto, sasa Nakumatt ya Kenya na hoja ya ARDHI vina uhusiano gani? mbona mtanzania Bakhresa ana shughuli zake Kenya, Rwanda, Uganda, Malawi, Burundi, Congo DRC lakini hatujadai haki sawa kwenye ARDHI yao...au mbona Ali Mfuruki ndio mwenye kumiliki Franchise ya WoolWorth Afrika Mashariki lakini hatujadai haki sawa kwenye ARDHI yao? Mbona wasauzi wameweka Shoprite sehemu mablimbali za bongo lakini hawajasema sasa raia wao wana haki sawa kwenye ARDHI yetu:tongue:
Kama wewe ni mwekezaji seroius toka Kenya, Uganda, US, UK, etc, etc unakaribishwa kuja kuwekeza bongo kwa mikono miwili. Lakini kama wewe ni Mungiki wa Kibera sahau kupewa haki sawa ya ARDHI yetu...Tutaendelea kuwa-Screen hivi hivi kwa sababu hatutaki kufikia hapo mlipo sasa ambapo wananchi wenuwa kawaida hawana hata mahala pa kulala!:tongue:
Ushauri wangu kwako kuanza kudai ARDHI yenu ambayo babu zenu wali-dhulumiwa na familia ya Kenyatta:lol: