mommythebest
JF-Expert Member
- Oct 22, 2015
- 516
- 618
Heshima kwenu wanabodi,
Ni matumaini yangu mu buheri wa afya na mnaendelea vyema katika shughuli za kulijenga Taifa.
Mara kwa mara nimekuwa nikijiuliza hili swali kwa nini katika jamii zetu sisi waAfrica wanawake hawathaminiwi na kupewa heshima wanayostahili?
Ukianza na kuangalia wanawake ndio nguvu kazi kubwa, mashambani huko vijijini utaona wanawake wanavyofanya kazi kwa bidii, lakini mavuno yanakuwa mali ya mwanaume/mume.
Yeye ndio anayeamua kuyauza na kupangia matumizi ya fedha, wakati kipindi cha kulima mostly mwanamke mara nyingine na watoto wake ndo walikua mstari wa mbele katika kulima. Haya tukija kwenye heshima, yani mitaani wanawake wanabezwa, kutukanwa na wengine kudhalilishwa sana(reference; bar maids), hata mara nyingine kwenye ofisi kama bosi ni mwanamke lazma huwa kuna maneno maneno mengi, utasikia "bosi mwenyewe mwanamke".
Nashangazwaga sana kwenye michezo ya kuigiza vile mwanamke kupigwa makofi na mangumi huwa ndo inam-potray baba/kaka anavyokabiliana na makosa ya mke/dada. Hii inaakisi mambo ndivyo yanavyotendeka majumbani kwa watu. Violence kwa mwanamke ni jambo la kawaida mitaani, hata akienda kushitaki kwa mjumbe au polisi ataambiwa kamalizaneni nyumbani, mkashindwana ndo mrudi, huko nyumbani mwanamke atashinikizwa yaishe sababu yeye ni 'mwanamke'. Viungo vya siri vya mwanamke ndio tusi kuu linalopamba mazungumzo ya vijiweni, au ndo tusi linalolotamkika kwa urahisi sana.
Mara nyingi mwanamke amekuwa akionekana kama half person, sijui kwa nini. Tena vijijini hali ndio mbaya sana, mtoto mdogo wa kiume anaheshimika kuliko mwanamke aliyemzidi umri. Kaka Paskali Mayalla huwa anasema wao katika jamii yao "hawaamini katika mwanamke". Jambo ambalo huwa linanihuzunisha sana. Laiti wanaume mngebadilishana muwe wanawake hata kwa wiki moja tuu, nadhani mngeelewa how strong and hard its takes to be a woman, na hiyo wiki hata isingeisha mngekuwa mmeomba poo.
Tubadili mtizamo, tuthamini wanawake.