HPAUL
JF-Expert Member
- Jan 18, 2011
- 410
- 567
Wapenzi wa michezo naomba mnijuze, kuna hii klabu inaitwa Yanga katika mechi zake 8 za mwisho za ligi kuu bara 2016, nne kati ya hizo wachezaji wa timu pinzani wanapewa kadi nyekundu na hatimaye Yanga inatumia fursa hiyo kupata ushindi, lakini kinachonishangaza katika ligi ya mabingwa Afrika, Yanga imeshacheza mechi 5 (2 na timu dhaifu ya Mauritius Cercle de Joachim, 2 na APR ya Rwanda na 1 Al Ahly ya Misri) hakuna kadi nyekundu timu ya upinzani imepewa na sasa dhahiri baada ya wiki moja inatolewa katika mashindano hayo na timu ya Al Ahly. Kwa nini ligi ya bara tu na sio ligi ya mabingwa Afrika?