Kwanini Husogelea Imani Ya Juu ya Mungu Zaidi Anapotaka kufariki.

Tempon

JF-Expert Member
Mar 14, 2017
234
382
Wanajamvi, Mimi ni mmoja wa watu wasio amini Uwepo wa Mungu huyu anaelezewa na Pande nyingi tu Hindusim, Christian, Muslim na Kadhalika Nimekuwa Atheist kwa Muda mrefu na nimekutana na Jamii za Atheist Haswa waishio nje ya Nchi kwa Nyumbani hapa ni changamoto sana Kujulikana Kama Huamini katika Mungu niko na Mwavuli wa Mungu(Undercover) Katika Dini fulani sita itaja, Back to the Topics

Nimekuwa karibu na Atheist wawili walio abroad ambao in real sense Walikuwa Hawaamini Uwepo Wa mungu kabisa Atheists hao Kwa sasa wameshapoteza Maisha ila kilichonishangaza Nilikuwa Karibu nao sana Wakati wakikaribia Kuaga Dunia Watu hao wote walifariki katika vifo tofauti wamenishangaza mno, Wamekufa Vifo asilia tu (Natural death) Kabla ya kila mmoja kupoteza Uhai wake Watu hawa walianza kujisogeza katika maandiko ya Mungu na Kuanza Sala tofauti na Za imani zao wanazo amini (secret) .Yani Sala juu ya hivi vitabu vinavyo sadikika ni Vya Mungu! Ivi kuna mtu anaekubwa na mauti asilia huku akiwa Bold atheist? Kwanini mwanadamu hujikabizisha kwa Mungu wa vitabu pindi tu jua linapoelekea kuzama(uzeeni). Mjadala ni Huru nakaribisha theists na non theist, Kujadili openly.
 
Mods nifanyieni edit kidogo , Kwanini binadamu husogelea zaidi imani juu ya Mungu anapokaribia kufariki. Cc@paw Invisible
 
Kwanza kimtazamo wangu maisha ya atheists ni sawa na mfano wa mtoto aliyetoroka nyumbani na kwenda club,hivyo pamoja na raha anazopata huko club ila bado nafsi inakosa furaha kila akifikiri itakuaje huko nyumbani akirudi baada ya kutoroka.

Kwa maana hiyo naweza kusema atheists ni kama hawana amani kwenye nafsi zao maana hakuna akili ya binaadamu ambayo inaweza kukubaliana na msimamo wao, hivyo pengine hiyo ndiyo sababu iliyopelekea hao kujisogeza kwenye mafundisho yahusiyo mungu pindi walipokuwa wanakaribia kufa.

Nafikiri hata vitabu vya dini vimegusia hali hii.
 
Hilo nifunzo kwako mleta mada kuwa mungu yupo nakuanzia sasa uanze kuutambua uwepo wamungu kabla umauti haujakusogelea karibu maana kuna vifo vingine nivyaghafla so unaweza usiipate hiyo nafasi kama waliyoipata hao wenzio
Asante ndugu
 
Ni somo kwako kuwa hivi vitu vyoote vya majani na nchi kavu kuna mtu aliyevitengeneza. Mungu kaleta somo karibu yako ili upate kumuabudu na kumsujudia.
 
Yaani wewe mleta mada una shida nyingi za kiakili.

Unaanzisha uzi kuwaponda Atheist, unafikiri Atheist wana akili za kikondoo?

Ajabu zaidi unakuja kukomenti kwa ID nyingine.

Mmeshindwa kwenye mijadala ya kuthibitisha kama Mungu yupo baada ya watu kupuuza vitisho vyenu sasa mmeamua kuji undercover kwenye Atheism?
 
Mwanadamu ni roho inayoishi katika jumba linaloitwa mwili.

Inapotokea roho ile inataka kuliacha jumba lake na kurudi inakotaka kutoka, hapo ndipo zile hadaa za mwili kuwa "hakuna Mungu" zinapofika kikomo.

Mara nyingi wengi kabla ya kufa wanapata neema ya kupata "perceptions" za kiroho na hivyo kuanza kumtafuta Mungu, japo si wote.

All in all Mungu yupo na ni vyema kutambua uwepo wake.
 
Yaani wewe mleta mada una shida nyingi za kiakili.

Unaanzisha uzi kuwaponda Atheist, unafikiri Atheist wana akili za kikondoo?

Ajabu zaidi unakuja kukomenti kwa ID nyingine.

Mmeshindwa kwenye mijadala ya kuthibitisha kama Mungu yupo baada ya watu kupuuza vitisho vyenu sasa mmeamua kuji undercover kwenye Atheism?
Mkuu Mimi sijaja na ID ingine naongea reality. Na mimi na Atheist pia
 
Yaani wewe mleta mada una shida nyingi za kiakili.

Unaanzisha uzi kuwaponda Atheist, unafikiri Atheist wana akili za kikondoo?

Ajabu zaidi unakuja kukomenti kwa ID nyingine.

Mmeshindwa kwenye mijadala ya kuthibitisha kama Mungu yupo baada ya watu kupuuza vitisho vyenu sasa mmeamua kuji undercover kwenye Atheism?
hahaha pumzi hii inatudanganya mno nahisi unaeza sema umejiumba.Ata shetan nae ana kiburi kuliko chako na ndo mana kakupata.Badilika nafas ni sasa kiburi cha kusema hakuna Mungu kitakupoteza milele hizo sayans zenu mpk leo hazijawajibu?
 
Wala siyo kiburi cha pumzi bali ni kwamba huyo Mungu anayeonekana kwa watu baada ya kufa sina shida naye maana hakuna ajuaye kama yupo.
Huyo Mungu wenu hamuwezi kumsapoti bila kumuhusisha Shetani.Mnatumia negativu force nyingi ili kuogofya watu, wakishaogopa basi ndio mnawaambia Mungu yupo na atawalinda. Watu wengi mnaamini Mungu yupo ili kujikinga na vitisho mlivyolishwa ambavyo navyo ni fake kama ilivyo idea ya uwepo wa Mungu.
 
Mkuu hata ukiondoa mambo ya mungu na dini bado maisha yetu binaadamu tumejiwekea sheria na adhabu kwa watakaoacha kufuata hizo sheria,hivyo ni vitisho kwa wasiotii hizo sheria kuwa watapata adhabu.
 
Mkuu hata ukiondoa mambo ya mungu na dini bado maisha yetu binaadamu tumejiwekea sheria na adhabu kwa watakaoacha kufuata hizo sheria,hivyo ni vitisho kwa wasiotii hizo sheria kuwa watapata adhabu.
Sheria za nchi tunazitunga wenye kupitia kwa wawakilishi wetu bungeni tuliowachagua wenyewe.

Zinabadilika kulingana na mazingira na kufanyiwa updations kulingana na wakati.Huwezi kulinganisha sheria za nchi na za Hugo dictator anayedhaniwa yupo.
 
mkuu kwa kawaidia kifo kinaogofya sana hasa ikitokea unaona umri umeenda na unajua siku zinavyozidi kwenda ndivyounavyosogelea kifo... binadamu tunatamani kujua siri iliyopo baada ya kifo kitatokea nini ? baadhi ya vitabu vya Mungu vinatumbia kuna maisha baada ya kifo ila sharti uishi katika utaratibu fulani ili uweze kuishi maisha mazuri... kutokana na hiyo hofu ya kifo na mioyo yetu ni dhaifu hasa tunapokaribia hatari fulani huwa tunatafuta unafuu fulani ndipo unapoona watu ugeukia Mungu kupata ahueni na kujipa moyo kuwa nikifa nitaenda mbinguni.. tofauti na wewe unayeamini ukifa unageuka mbolea na ndiyo mwisho wa story ya maisha yako.. sasa incase ukakuta kuna mbingu duh utajilaumu sana
 
Hawa watu eti! wanasema mwanadamu katokana na mada na mada ni ya tangu na tangu na haifi, yaani mafano uchimbe bwawa na kujaza maji na kisha maji uyaache kwa muda wa siku kadhaa na utakapoenda baada ya siku kadhaa kupita utakuta ndani ya bwawa kuna vijidu viavyoitwa ndubwi ambayo vimetoka kutokana na uwepo wa maji, ndio wanadamu walivyoanza.
 
Sheria za nchi tunazitunga wenye kupitia kwa wawakilishi wetu bungeni tuliowachagua wenyewe.

Zinabadilika kulingana na mazingira na kufanyiwa updations kulingana na wakati.Huwezi kulinganisha sheria za nchi na za Hugo dictator anayedhaniwa yupo.
Hoja iko pale pale kuwa kuna adhabu kwa asiyetii hizo sheria,hivyo kwa kuogopa adhabu inabidi ufuate tu sheria.
 
Sheria za nchi tunazitunga wenye kupitia kwa wawakilishi wetu bungeni tuliowachagua wenyewe.

Zinabadilika kulingana na mazingira na kufanyiwa updations kulingana na wakati.Huwezi kulinganisha sheria za nchi na za Hugo dictator anayedhaniwa yupo.
haha mnaemuona kelele msiemuona je.Uzur tumepewa choices so sishangai anayosema its matter of time.
 
Back
Top Bottom