Kwanini hizi ndege hupita juu sana na kutoa moshi mwingi?

Restarting

Member
Jan 28, 2020
80
106
Jamani hizi ndege kwanini zinapita juu sana kutoka usawa wa ardhi, na kwanini huwa zinatoa moshi mwingi ukilinganisha na hizi tulizo zizoea kuziona hapa kwetu. Naomba kujulishwa wajuzi wa haya mambo?

IMG_20210530_181411.jpg
 
Nahisi ni roketi ila nitasahihishwa...sina uhakika

Pia moshi wake ni kwa sabbu ya kuwepo kwa mgandamizo wa hewa, kule juu kuna baridi ya laana, sasa hizo roketi engine zake zinakuwa so high temperature ndo maana unaona mivuke/mimoshi ile

Kama nimekosea naomba marekebisho.

Ila Mkuu kwa zoezi la kawaida siku kukiwa na baridi kali...nenda nje alafu uachame mdomo uone utakavyoachia mvuke/moshi mkali.
 
Jamani hizi ndege kwanini zinapita juu sana kutoka usawa wa ardhi, na kwanini huwa zinatoa moshi mwingi ukilinganisha na hizi tulizo zizoea kuziona hapa kwetu. Naomba kujulishwa wajuzi wa haya mambo ?View attachment 1802828
Ule sio moshi
Kitokana na joto kali la ndege na kule ni baridi inatokea kitu kama mvuke..kinachofanya tuone ni mwingi kwasababu ya miale ya jua tu..
 
Zile ni rocket na zinasifa ya kusafiri umbali mrefu ndo maana huwa zinatembea mbali sana pia kutokana na muungurumo wake lakini pia ndege hizo zinasifa ya kuchoma mafuta mengi ndo sababu ya ule moshi.
 
Hakikisha hapo ulipo kkuna IRON DOME kama hakuna taja ID zako zote ili ziwekewe RIP tukiona kimya
 
Wanaosema ni roketi nina uhakika tangu wazaliwe hawajawahi kuona roketi sehemu yoyote ile angani labda kama waliwahi kuishi nje ya Afrika.

Range ya kufyatua roketi ziko maeneo machache duniani kama Baikonur Cosmodrome ya nchini Kazakhstan inayomilikiwa na Russia kwa kukodisha. Nyingine maarufu ni Cape Canaveral ya Marekani.

Roketi inaruka kwa kupanda juu hivo hapa Afrika hakuna sehemu yoyote utaiona. Hizo ni ndege zimeenda masafa ya kawaida kwake ila kutokana na hewa ya juu kuwa ya baridi sana, engine zikichochea zinatoa hewa ya joto kali nyuma na kuacha alama inayoonekana kutokana na miale ya jua. Usiku hutoona hizo alama
 
Siyo Moshi.
Siyo Roketi.

Huo ni msuguano wa ndege na hewa ya huko ambako ni mbali sana. Hali ya hewa ya huko ni tofauti na huku chini zinakopita hizi ndege zingine ambako Oxygen ipo nyingi huku
 
Nahisi ni roketi...ila nitasahihishwa.

Pia moshi wake ni kwa sabbu ya kuwepo kwa mgandamizo wa hewa,kule juu kuna baridi ya laana...sasa hizo roketi engine zake zinakuwa so high temperature ndo maana unaona mimoshi ile

Kama nimekosea naomba marekebisho.

Sio lazima iwe rocket. Ndege zote kubwa zinazofanya safari za kimataifa zinapita juu sana (anga za kimataifa) kule joto la nje laweza kufika negative 50. so u can imagine, kwa hiyo exhaust ya ndege inapotoka japo haina moshi inapokutana na baridi kali kiasi hicho inatengeneza mgando ambao sisi tunauita moshi.
 
Wanaosema ni roketi nina uhakika tangu wazaliwe hawajawahi kuona roketi sehemu yoyote ile angani labda kama waliwahi kuishi nje ya Afrika.

Range ya kufyatua roketi ziko maeneo machache duniani kama Baikonur Cosmodrome ya nchini Kazakhstan inayomilikiwa na Russia kwa kukodisha. Nyingine maarufu ni Cape Canaveral ya Marekani.

Roketi inaruka kwa kupanda juu hivo hapa Afrika hakuna sehemu yoyote utaiona. Hizo ni ndege zimeenda masafa ya kawaida kwake ila kutokana na hewa ya juu kuwa ya baridi sana, engine zikichochea zinatoa hewa ya joto kali nyuma na kuacha alama inayoonekana kutokana na miale ya bbjua. Usiku hutoona hizo alama
Hivi Rocket sindio hizihizi anazorusha ELON MUSK kilasiku kama FALCON X maana neno Rocket nimeanza lisikia toka mdogo ila ukubwani nayaona ma Falcon X
 
Back
Top Bottom