Mzawa_G
JF-Expert Member
- Feb 27, 2014
- 667
- 1,467
Nadhani katika kipindi chetu cha utoto tulikiwa tunapenda kuziita ndege za Urusi, yaani ni zile ndege ambazo zinapita anga la juu zaidi huku zikichora kitu mfano wa mstari wa moshi mzito sana.
Sasa leo nakufahamisha ambapo mstari huo kwa kitaalamu unafahamika kama Condensation Trails (Contrails).
Nataka nikuelekeze ni vipi moshi huo hutokea nyuma pindi ndege hizo zinapopita katika anga la juu zaidi.
Injini za ndege huzalisha mvuke mkubwa sana wenye joto kali huku kwa nyuma ambapo hukutana na hali ya hewa ya ubaridi kwenye anga la juu huko angani, mvuke huo wa joto unapokutana na ubaridi huunda kitu kama chenga chenga za barafu ambazo huganda na kubaki angani. Huku duniani huweza kuona kitu kama mfano wa wingu au moshi linalotawala sehemu yoyote ile ndege inapopita.
Nadhani kwa namna moja ama nyengine suala hili hufanana na ule mchakato wa wingu kujitengeneza, ambapo mvuke hutoka ardhini na kwenda juu unapokutana na hewa ya ubaridi basi huganda.
Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili