CHOTABUSARA
Member
- Feb 6, 2012
- 47
- 48
Jana nilifika airport Dar nikaita Uber, baada ya kuingia kwenye gari nilishangaa watu wakavamia ghafla nakuanza kugombana na driver eti Uber hairuhusiwi Airport Dar, nilishangaa sana nikauluza kwani hawa wakina nani? Ni polisi au? Nikaambiwa ni madriver wa tax tu pale airport, sasa nachojiuliza Uber nao kampuni yao inafany kazi kinyemela kama ACACIA au? Pia kwanini awa watu wajichukulie hatua mkononi? Na kama ni hivyo na ma driver wa posta nao wakiunda umoja wao na kuzuia tax nyingine zisiingie posta na wengine na wengine biashara itafanyika tena hapa mjini? Maana hata hao ma driver wa aiport wataishia airport tu, na kwanini TAA wameruhusu vurugu zile pale airport, mi nimetumia uber sehemu mbalimbali duniani sijawai ona ule upumbavu, tunaomba jibu wahusika? Is it illegal to use uber in Tanzania?