Kwanini HESLB isikope benki kusomesha wanafunzi?

Kwanini HESLB isikope benki kusomesha wanafunzi?

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Posts
8,658
Reaction score
15,814
Taifa lisilo na wasomi ni taifa mfu!

Nawashauri bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuangalia uwezekano wa kukopa pesa benki ili waweze kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili ikiwa pesa walizo nazo hazitoshi.

Kuna benki za serikali nyingi tu zina fedha ambazo zinaishia kupotea kwenye mikopo chechefu. Kwa nini Badru na wenzako msifanye mchakato wa kukopa benki ya wanawake, TIB, NMB and the like ili mkopeshe wanafunzi wa elimu ya juu?

Najua mkiamua kukopa bilioni thelasini hadi hamsini ili kufadhili masomo ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao elfu thelasini, hilo jambo linawezekana.

Loan board imekuwa ikijinasibu kufanya makusanyo ya mikopo iliyokwisha tolewa, kitu ambacho kinaipa uiwezo wa kukopa kwenye mabenki, kufadhili wanafunzi na kasha kukusanya pesa hizo accordingly.

Ninawashauri wizara ya elimu ya juu kwa kushirikiana na bodi ya mikopo ikae na wadau ambao ni mabenki ili kupata loan syndication kutoka benki zilizo tayari. Angalau zikipatikana benki tatu zilizo tayari ambazo zinaweza kutoa mkopo wa bilioni kumi kumi loan board haiwezi kushindwa kukusanya bilioni thelasini na zaidi.

Pia kwa wanafunzi watakaopata mkopo kwenye second selection, wapewe mkataba tofauti na wale watakaopata pesa za loan board.

Yani wanafunzi hawa wasaini mkataba wa kulipa pesa hizo pamoja na riba isiyozidi asilimia 20. Wale watakaokubali wachukue, wale wasiotaka waaache, lakini katika hili loan board itakuwa imewasaidia wanafunzi hao.

Ikumbukwe kuwa wanafunzi hawa mmoja mmoja hawawezi kwenda kwenye benki kukopa fedha za kusomea masomo ya juu, lakini loan board ikilibeba jukumu hilo na kufanya kwa niaba ya wanafunzi, hawewezi kushindwa ku raise kiwango cha pesa kinachohitajika ili kuwawezesha wanafunzi wa kuanzia daraja la pili na la tatu kuweza kupata mkopo na kujiunga na masomo ya elimu ya juu!
 
helsb yenyewe ina mikopo chefuchefu kibao... wadaiwa sugu kibaooo... hizo hela za kuzilipa benki na riba watazitoa wapi?
 
Back
Top Bottom