Lagrange
JF-Expert Member
- Mar 7, 2017
- 2,441
- 2,878
Habari Wakuu !
Mimi ni kijana niliyezaliwa awamu ya uongozi wa Hayati Benjamin Mkapa, nimebahatika kusoma elimu ya msingi, upili na kuhitimisha elimu ya juu awamu ya John Magufuli.
Kabla ya kuhitimu elimu yangu ya juu nilijipanga sana, nipate kitu cha kufanya, nilinunua zana za kazi za kupasua mbao, nilinunua chain saw kwa Tsh 1,700,000 kinshen pale Iringa mjini, nikanunua na engine horse power 24 kwa 1,260,000 hapo hapo kinshen, nikachonga na benchi sehemu moja inaitwa usokami kwa Tsh 700,000, nikanunua na msemeno mkononi kwa mtu pale mafinga kwa 470,000 ,nikarudi iringa mjini nikanunua na vitu vingine vinavyohitajika kwa ajili ya kazi, nikavisafirisha hadi wilaya ya Kilolo kwa ajili ya kazi.
Mungu mwema nikifanikiwa kuanza kazi kwa kusua sua sababu ya mtaji mdogo na changamoto zaidi iliyonikumba ni malipo ya mzigo kutokuwa ya wakati, naandaa mzigo porini vizuri najaza forward napeleka sokoni saba saba, naambulia kupewa ya gari na hela kidogo ya kurudia porini tu, kwenye mbao hamna cash kabisa!!
Kutokana na kuwa hamna cash niliambulia kuwa na madeni mengi sana kwa mafundi na engine huwa ni nzito sana, huwa inakaa porini muda mwingi, engine sijui waliiweka nini siku tumewasha ili-burst kama bomu, blok ikatoboka. Nikaamua kusitisha hiyo shughuli na kuuza vitu, sikupata mtu wa cash kabisa, nikaviuza mpaka sasa nadai 1,300,000 hiyo hela kulipwa naona ni ndoto.
Nkaamua nibebe mahindi mabichi nipeleke Dar, mara ya kwanza sikupata faida yoyote, mara ya pili (trip) nikapata hasara ya 983,000. Nikaamua kusitisha kwenda Dar, nikapakia mahindi kwenye canter nikaleta Dodoma, nikapata hasara ya 716,000. Kwa kweli niliona dunia ngumu sana kwangu!
Nikaona mbegu ya pioneer ya Babati inapendwa sokoni zaidi ya hybrid 614 na 628, nikaanza kuleta hiyo mbegu sokoni mpaka kufikia kwenye mwezi wa nne msimu ulipokata, nikafanya tathmini nikaona hakuna chochote nilichokipata kwa kuzunguka kote Manyara na Iringa, nikaamua kutulia kwanza kwa kukaa kwa mzee ofisini kwake.
Mzee ana ofisi mbili mjini na ameajiri vijana basi mimi nikawa nakaa ofisi moja ambayo ina kijana, ni mkubwa kwangu kiumri kazaliwa 1992, nilikuwa namheshimu sana sana kama Kaka yangu.
Huyu kijana amekaa ofini amejenga nyumba kisiri siri pasipo Mzee kufahamu, kashapauwa, kashaweka na fensi kabisa bado geti na finishing ya nyumba.
Mimi kuja kukaa ofini ilikuwa changamoto kubwa sana kwake maana alishindwa kuendeleza ujenzi wake.
Kinachoniuma mimi ni huyu kaka kumwambia Mzee mimi ni mwizi na Mzee akamwamini, akamwambia
droo ichongewe ufunguo mpya, kwa hiyo droo ya pesa huwa inafungwa kwa sasa na huyu kijana ndiyo anayekaa na ufunguo na kwa kweli huyu kijana analaza pesa ndefu sana kwa siku maana vitu vya dukani ni vya kupatana na mteja, havina bei moja. Hata ufunguo wa dukani kwa sasa siruhusiwi kushika kabisa kabisa.
Inaniuma sana MTU ananiambia napaswa nimheshimu sana maana yeye ana akili za mtaani na mimi za darasani na wakati sijawahi mdharau, anaenda mbali na kuniambia sisi wachaga wa Marangu tumekaa kizembe sana kwa kuwa yeye ni wa Kibosho!
Nilipatwa na shida kidogo nikaazima laki, hii laki moja naiona kama kaburi kwangu maana nimeshindwa kuirejesha kwa wakati kila siku ananimba mzigo unashindikanika kuagiza, nimeshikilia hela!
Naye kijana wa duka jingine ni hivyo hivyo, kuna siku nilikuwa ofisi ya pale akauza speaker kwa 720,000 akaja akamwambia Mzee ameuza kwa 640,000 na huu ndio mchezo mzima wakiuza friji, TV etc . Yan Mzee anapigwa mashariki na magharibi na anawaamini sana hawa vijana sana. Hawa vijana nadhani wana extra power kidogo.
Hivi kweli mwizi wa mahindi gunia mbili ni sawa na mwizi wa mahindi mikono miwili kwa ajili ya kwenda kukaanga tu!
Kwanini dunia inakuwa hivi.!
Leo nasulubiwa maana nimeambiwa nisipotoa hiyo hela hadi saa nne, atamwambia Mzee ili anidai mwenyewe.